Mkuu,Kwanini CUF wasiungane na CCM kumsimamisha mgombea wao mmoja? au wewe hujui kuwa CUF na CCM lao ni moja?
Kamati kuu ya chama cha chadema kuweni makini na mamluki wa chama tawala,Kumbuka ktk msafara wa mamba na kenge wapo.Asante kwa taarifa Regia, tunategemea hekima,umakini na utashi mkubwa katika mchakato wa kumpata mwakilishi. Ikumbukwe kua uchaguzi huu ni kipimo cha mabadiliko na ukuaji wa nguvu ya chama baada ya uchaguzi wa mwaka jana na kasi ya kuelekea uchaguzi mkuu 2015.
Kamati Kuu ya CHADEMA inatajiwa kufanya kikao chake kesho katika jimbo la Igunga.Kikao hicho ni maalum kwaajili ya kupitisha jina la mgombea Ubunge katika uchaguzi mdogo unaotarajiwa kuanza tarehe 7 Sept 2011. Vile vile kikao hicho kinatrajiwa kupitisha mkakati na bajeti ya uchaguzi huo katika kuhakikisha kuwa jimbo hili linachukuliwa na CHADEMA.Dalili zote za awali zinaonesha kuwa jimbo hili kuchukuliwa na CHADEMA.Kutoka njiani Manyoni tukiwa tunaelekea Igunga.Nawasilisha.

Asante Regia kwa taarifa. Nje ya mada hii sisi wananchi tumesononeshwa sana na kuumia mno na kauli ya mbunge mwenzenu Mh Shibuda. Yaani nilitamani kupiga simu yangu kwenye screen wakati huyu mbunge akichangia mambo ambayo yanaonekana wazi wazi kuwa si mwenzetu kabisa. si mimi tu ila wananchi wengi wapenda haki na usawa wameumia sana.

Nakuomba Regia fikisha suala hili mbele ya kamati kuu, sisi tunapendekeza mtu huyu apumzishwe maana si mwenzetu. ni vyema tukatibu ndonda leo badala ya kulifuga cause linaweza lisitibike tena badala yake kama lipo mguuni basi lazima ukatwe kuokoa maisha. sisi hatutaki tufike huko.

Fikisha ujumbe wa hao wapiganaji-- tunawaombea mafanikio. najua wananchi wakakuwa barabarani kila mnapita cause mmebeba sura ya Tanzania mpya - Tanzania yenye Tumaini Jipya. Mungu awababariki sana tupo pamoja nanyi kwenye sara na dua zetu. Peoples Poweeeer.
Msisahau kuwa kikubwa ni kulinda kura kama Nyamagana, Ilemela, Mbea Mjini na Arusha. maana magamba wameshagombana wao kwa wao kuwa ama kwa dola au kwa pesa lazima jimbo lirudi CCM, hawataki kusikia lugha za kina Bashe kuwa "nataka tushindwe Igunga tuheshimiane"
Na nyinyi msiifanye CHADEMA kama si chama kisichostahili kupitia misukosuko. Kuna kazi nzito Igunga mnaleta habari ya Shibuda. Mnadhani akiondoka Shibuda watakosekana wa aina hiyo. Kwa ninavyowajua CHADEMA suala la Shibuda sidhani linawaumiza kama chama. Wao wachukue hansard kisha wamuite kwenye chama apate nafasi ya kufafanua lengo la anayoeleza bungeni na magazetini. Kesi ya Shibuda ni rahisi sana kwa sababu ina ushahidi mzuri wa maneno yake moja kwa moja. Muhimu ni kujua nia yake ni nini hasa na ikibidi afanye hivo kimaandishi.
Kwa hiyo hata ukimtukana rais matusi ya nguoni bungeni hansad inakulinda........labda mimi sielewi.Hapo kwenye red. Kwa mujibu wa Katiba, Mbunge ana kinga ya ajabu sana kwa lolote atakaloongea AKIWA KWENYE VIKAO RASMI NDANI YA UKUMBI WA BUNGE. Hakuna mamlaka yoyote, hata Mahakama ya Rufaa, yenye uwezo wa kumhoji Mbunge kwa kauli zake "ndani ya Bunge". Labda kwa kujua hilo, ndio maana Shibuda anafanya mizaha anayoifanya.
Kwa hiyo hata ukimtukana rais matusi ya nguoni bungeni hansad inakulinda........labda mimi sielewi.
Nyie mnaolazimisha CDM iungane na CUF kwanini CUF wasiungane na CCM halafu mtuambie ni wapi wapinzani waliungana wakashinda,
Nadhani swali lako limejibiwa vizuri na Mwita Maranya.....Wait a minute..... kwa hiyo lile jina la mwalimu tulopewa limetoka wapi ikiwa hii kama ti haijafika hata Igunga ndio kwanza wako safarini kuelekea huko?..Huyo mwana JF aliyetuletea habari za kura za maoni anaweza kutueleza ni kina nani walioendesha kura hizo maanake isijekuwa tumelishwa myamafu ili watuchekke baadeye kamati itakapochagua jina jingine.. Mchezo huu umefanyika sana ili kuleta vurugu ndani ya vyama hasa nikifuatia chaguzi zilizopita wa vijana CCM na CDM.
Kwa mujibu wa habari za uhakika ni kwamba chadema itashika nafasi ya
tatu katika uchaguzi huo,....na kama chadema isipo simamisha mgombea
basi cuf itashinda lakini kwa kua vyama vya upinzani vinaenda kugawana
nusu ya nyama huko igunga,basi mzee kafumu ataingia mjengoni kwa mbwembwe sana.
Unaongea sana kama kasuku kila kitu wewe unakijua ah waache wana Igunga wachague wanayemtaka kwani tatizo lako nini mbona unaumia sana kuna nini, kwani kuhama chama ni dhambi kwa taarifa yako karibu asilimia 80 ya wapinzani walikuwa CCM hata hao unaowaona viongozi wa CDM walikuwa huko huko.Mheshimiwa Regia nakubali CDM mko serious lakini jambo dogo tu huwa tunamalizwa na CCM, mimi ni mzaliwa wa igunga na nimeishi igunga muda mrefu sana kwahiyo nafuatilia kwa karibu mchakato wa igunga tangu kujiuzulu kwa rostam, nawajua wafuasi wa CCM na CDM. weakness ya CDM Igunga hakuna uongozi imara wa CDM, nasema hivyo kwasababu mwenyekiti wa wilaya Majimoto, Kashindye na Pili mnene (amekuwa mwenyekiti wa wanawake wa chadema wilaya tangu kujiuzulu kwa rostam kabla ya hapo alikuwa ccm) walikuwa wakala wa rostam uchaguzi wa 2010.
Majimoto alijitoa kugombea ubunge kwa kupewa fungu na rostam, Kashindye alteuliwa kuhamasisha kura za uraisi kwa jakaya kwa kauli mbiu aliyokuwa anawambia wanaigunga vijijini kuwa DR. SLAA ni fisadi wa mapenzi ili wanawake wasimpigie kura. Pili Mnene amejengewa nyumba na rostam na mpaka sasa anasomesha mtoto wake chuo kikuu. Mheshimiwa diwani wetu wa chadema kwenye vikao vya council anapokea posho anayotoa RA ili kuweza vikao vya madiwani vipitishe matakwa yake kwa remote wakati yeye anakula raha jijini.
Sasa kabla ya kupitisha mgombea wenu kesho mheshimiwa kashindye muhakikishe mmesafisha jambo hilo kwani walimu wote wanajuwa kuwa alikuwa kibaraka wa rostam kufanya kampeni za ccm 2010 sasa wapiga kura wenu watakuwa na imani nae vipi kwasababu wanamtambua kama CCM na kwataarifa nilizo nazo hadi sasa wamekorofishana na DC igunga kwa kuwa wanajuwa kilichofanyika mwaka jana. Na siku chache baada ya kujiuzulu RA, Bashe alivyokuja igunga alimtumia Kashindye kuwapelekea wenyeviti wa kata salamu kutoka kwa rostam na kuwajulisha kuwa yupo nao pamoja fungu alilopewa alimficha boss wake DC na badala yake akatumia gari la ukaguzi na mafuta ya serikali bila kumgawia boss wake fungu.
TUPO NJIA PANDA wanaigunga kwa maana kwamba tutapata bora mbunge kwa maslahi yake mbunge na kuongeza fungu la posho kwenye chama au tunapata mbunge ili kuweza kuwatumikia wanaigunga? NITOE NJIA PANDA KESHO
Kamati Kuu ya CHADEMA inatajiwa kufanya kikao chake kesho katika jimbo la Igunga.Kikao hicho ni maalum kwaajili ya kupitisha jina la mgombea Ubunge katika uchaguzi mdogo unaotarajiwa kuanza tarehe 7 Sept 2011.
Vile vile kikao hicho kinatrajiwa kupitisha mkakati na bajeti ya uchaguzi huo katika kuhakikisha kuwa jimbo hili linachukuliwa na CHADEMA.Dalili zote za awali zinaonesha kuwa jimbo hili kuchukuliwa na CHADEMA.Kutoka njiani Manyoni tukiwa tunaelekea Igunga.Nawasilisha.