Kamati Kuu ya CHADEMA yakutana Igunga

Msisahau kuwa kikubwa ni kulinda kura kama Nyamagana, Ilemela, Mbea Mjini na Arusha. maana magamba wameshagombana wao kwa wao kuwa ama kwa dola au kwa pesa lazima jimbo lirudi CCM, hawataki kusikia lugha za kina Bashe kuwa "nataka tushindwe Igunga tuheshimiane"

Dada Regia, mimi binafsi nina wasiwasi na common sense na reasoning capacity ya Magale Shibuda, inaonekana kasi yetu haiwezi ni bora apumzishwe hata kama ni kupoteza kiti cha ubunge na jimbo la maswa kwa ujumla.

Na nyinyi msiifanye CHADEMA kama si chama kisichostahili kupitia misukosuko. Kuna kazi nzito Igunga mnaleta habari ya Shibuda. Mnadhani akiondoka Shibuda watakosekana wa aina hiyo. Kwa ninavyowajua CHADEMA suala la Shibuda sidhani linawaumiza kama chama.

Wao wachukue hansard kisha wamuite kwenye chama apate nafasi ya kufafanua lengo la anayoeleza bungeni na magazetini. Kesi ya Shibuda ni rahisi sana kwa sababu ina ushahidi mzuri wa maneno yake moja kwa moja.

Muhimu ni kujua nia yake ni nini hasa na ikibidi afanye hivo kimaandishi.
 
WEWE Regia mTema umechanganyikiwa, Igunga utaisikia hewani na usizani kelelel za chura zinamzuia mbuzi kunywa maji.Igunga itabaki kuwa jimbo la ccm na kama kutoka kwa rostam kumewafanya mzani jimbo liko wazi mmechelewa jimbo linawenyewe.

Nakusikitikia kwa kutumia lugha isiyostahili na tambo za kichakachuaji; pamoja na kwamba ndivyo Mungu alivyokujalia
 
Asante Regia kwa taarifa. Nje ya mada hii sisi wananchi tumesononeshwa sana na kuumia mno na kauli ya mbunge mwenzenu Mh Shibuda. Yaani nilitamani kupiga simu yangu kwenye screen wakati huyu mbunge akichangia mambo ambayo yanaonekana wazi wazi kuwa si mwenzetu kabisa. si mimi tu ila wananchi wengi wapenda haki na usawa wameumia sana.

Nakuomba Regia fikisha suala hili mbele ya kamati kuu, sisi tunapendekeza mtu huyu apumzishwe maana si mwenzetu. ni vyema tukatibu ndonda leo badala ya kulifuga cause linaweza lisitibike tena badala yake kama lipo mguuni basi lazima ukatwe kuokoa maisha. sisi hatutaki tufike huko.

Fikisha ujumbe wa hao wapiganaji-- tunawaombea mafanikio. najua wananchi wakakuwa barabarani kila mnapita cause mmebeba sura ya Tanzania mpya - Tanzania yenye Tumaini Jipya. Mungu awababariki sana tupo pamoja nanyi kwenye sara na dua zetu. Peoples Poweeeer.


kwa kuwa shibuda anachezea juhudi za watanzania wapenda haki na mabadiliko apewe adhabu moja tu,nayo ni kuachwa kama alivyo kwa miaka mitano ijayo,asifukuzwe kwa sababu ndio anachotafuta,akiachwa kama alivyo itakuwa ni adhabu kubwa zaidi
 
naona unajipa moyo reg hautaki kusema ukweli jinsi CUF ilivyoshikilia jimbo na jinsi LEOPARD MAHONA mgombea wa CUF anavyozidi kuungwa mkono na wanaIGUNGA bila shaka mbunge anayefuata baada ya rostam ni LEOPARD MAHONA wa CUF.
 
kwa hali ilivyo, Igunga inakwenda CUF, CDM wamepokelewa na wafuasi wa CUF kwa wingi wao na hii ni ishara mbaya kwa CDM.
 
Wait a minute..... kwa hiyo lile jina la mwalimu tulopewa limetoka wapi ikiwa hii kama ti haijafika hata Igunga ndio kwanza wako safarini kuelekea huko?

Huyo mwana JF aliyetuletea habari za kura za maoni anaweza kutueleza ni kina nani walioendesha kura hizo maanake isijekuwa tumelishwa myamafu ili watuchekke baadeye kamati itakapochagua jina jingine.. Mchezo huu umefanyika sana ili kuleta vurugu ndani ya vyama hasa nikifuatia chaguzi zilizopita wa vijana CCM na CDM.
 
Bila upinzani kuungana,
jimbo la Igunga ni ndoto kulipata,
la sivyo ni kutaka kujifurahisha.
 
Wait a minute..... kwa hiyo lile jina la mwalimu tulopewa limetoka wapi ikiwa hii kama ti haijafika hata Igunga ndio kwanza wako safarini kuelekea huko?

Huyo mwana JF aliyetuletea habari za kura za maoni anaweza kutueleza ni kina nani walioendesha kura hizo maanake isijekuwa tumelishwa myamafu ili watuchekke baadeye kamati itakapochagua jina jingine.. Mchezo huu umefanyika sana ili kuleta vurugu ndani ya vyama hasa nikifuatia chaguzi zilizopita wa vijana CCM na CDM.
&
Mkuu kwa mujibu wa katiba ya chadema kura za maoni husimamiwa na uongozi/kamati ya utendaji ya wilaya/jimbo chini ya uangalizi wa uongozi wa mkoa/taifa. Baada ya zoezi la kura za maoni kukamilika kwa maana ya wajumbe wa mkutano mkuu wa jimbo/wilaya kupiga kura ikifuatiwa na maoni ya uongozi wa wilaya/jimbo,taarifa rasmi hutumwa uongozi wa taifa ofisi ya katibu mkuu kwa ajili ya uamuzi wa mwisho toka kwa kamati kuu.

Bila shaka huo ndio utaratibu uliotumika huko igunga katika hatua za awali,na sasa kamati kuu inakwenda kukamilisha zoezi la uteuzi wa mgombea wa chama kutoka miongoni mwa waliogombea na kupigiwa kura na kwa kuzingatia maoni na mapendekezo ya kamati ya utendaji ya jimbo/wilaya na ama taarifa nyingine ambazo chama kinakuwa nazo juu ya wagombea.
 
Hossana Tech,
Hii kama nia yao kweli ni kupeleka jimbo la Igunga upande wa upinzani,
La sivyo ..... nambalii wani ni sisiemu!
 
Wakuu.Tuemshafika Igunga na kupokelewa na mamia ya wakazi wa hapa nakufanya mkutano mdogo wa hadhara wa ukaribisho.aKwa kweli hali inatia moyo. Naona kuna watu wanabeza kuwa CHADEMA haiwezi kushinda wakilinganisha na uchaguzi wa Biharamulo na Busanda.

Kuna wengine wanadai CHADEMA kuwa ya tatu. Ndugu zangu kila chama lazima kiwe namatumani ya kushinda vinginevyo basi tusingeweza kushiriki kwenye uchaguzi huu, CHADEMA inajiamini na imeshafanya utafiti wa awali na inaonekana kuelekea kushinda. Duniani kote huwa kuna opinion polls. Time will tell.

BTW Am so happy kuwa Igunga leo, kumechangamka.
 
Tunategemea mazuri katika kumpitisha mgombea!!!!apatikane kwa haki,mwenye mawazo ya mageuzi!!!!Mteueni mtu makini asiye kuwa kigeugeu!!!mwenye kudumisha upendo,na uimara wa CDM kwa maendeleo ya wananchi wa Igunga na Tanzania nzima!!!!!!!VIVAAAAAAAAAAAAAAA CHADEMAAAAAAAAAA
 
wakuu.tuemshafika igunga na kupokelewa na mamia ya wakazi wa hapa nakufanya mkutano mdogo wa hadhara wa ukaribisho.akwa kweli hali inatia moyo.naona kuna watu wanabeza kuwa chadema haiwezi kushinda wakilinganisha na uchaguzi wa biharamulo na busanda.kuna wengine wanadai chadema kuwa ya tatu.ndugu zangu kila chama lazima kiwe namatumani ya kushinda vinginevyo basi tusingeweza kushiriki kwenye uchaguzi huu,chadema inajiamini na imeshafanya utafiti wa awali na inaonekana kuelekea kushinda.duniani kote huwa kuna opinion polls. Time will tell.btw. Am so happy kuwa igunga leo,kumechangamka.
poleni kwa safari ndefu!!!!tupo pamoja nanyi!!!mungu awalinde daima!!!!!!
 
Kwa mujibu wa habari za uhakika ni kwamba chadema itashika nafasi ya
tatu katika uchaguzi huo,....na kama chadema isipo simamisha mgombea
basi cuf itashinda lakini kwa kua vyama vya upinzani vinaenda kugawana
nusu ya nyama huko igunga,basi mzee kafumu ataingia mjengoni kwa mbwembwe sana.
Kwanini CUF wasiungane na CCM kumsimamisha mgombea wao mmoja? au wewe hujui kuwa CUF na CCM lao ni moja?
 
@Fuso..viongozi wa chadema wanajua jinsi gani wanachama/wapenzi tusivyo mhitaji shibuda maana cc ya chadema walipo fanya mkutano hapa Arusha..mbowe alipata wakati mgumu pale wanachadema walipotaka atoe msimamo wake kwanini shibuda hajafukuzwa lakini mwenyekiti alisema kunakamati ambayo inachunguza hivyo asingeweza kutoa msimamo wake kwani chadema inaongozwa kwa kufata katiba...hivyo huyu jamaa na vyo endaenda hana mda
 
Wakuu.Tuemshafika Igunga na kupokelewa na mamia ya wakazi wa hapa nakufanya mkutano mdogo wa hadhara wa ukaribisho. Kwa kweli hali inatia moyo.

Naona kuna watu wanabeza kuwa CHADEMA haiwezi kushinda wakilinganisha na uchaguzi wa Biharamulo na Busanda. Kuna wengine wanadai CHADEMA kuwa ya tatu.

Ndugu zangu kila chama lazima kiwe namatumani ya kushinda vinginevyo basi tusingeweza kushiriki kwenye uchaguzi huu,CHADEMA inajiamini na imeshafanya utafiti wa awali na inaonekana kuelekea kushinda.Duniani kote huwa kuna opinion polls. Time will tell.

BTW. Am so happy kuwa Igunga leo, kumechangamka.
Kwakuwa kamanda Mwita Mwikwabe pamoja na bavicha wamekuwa igunga kwa muda wa kutosha basi nina imani kwamba ground work imefanyika vizuri na kampeni zikianza basi ni mwendo mdundo hadi mjengoni.
Ninawatakia kila la kheri.
 
Back
Top Bottom