Kamati Kuu ya CHADEMA Kukutana Kesho Kupitisha Wagombea BAVICHA

we huna jipya wala la maana tofauti na kujaribu kuleta uchochezi ndani ya chama, hii habari yako mimi binafsi naitafsi kama upuuzi na upumbavu maana unaongelea mambo ya kusadikika ambayo hayana ushahidi wowote au naweza kuita unafanya uchochezi!

nadhani ungeweza kuongea mambo ya kujenga au kukosoa kwa kutupa kasoro na wasifu wa wagombea maana wote wana haki ya kugombea kama wana-cdm; hayo unayoongea hayana nafasi tena maana kila mtu na kila mwana chama pia ana haki ya kumpigia kampeni anayemwona anafaa kwa muono wake na kwa mtazamo wake.
jitahidi msiwape nafasihawa kuvuruga uchaguzi
 
jamani wana chadema, watakopiga kura. Mimi binafsi namuunga john heche, kwa sababu zifuatazo:
1. Nimesoma naye, namafhamu tabia yake.
2. Ana msimamo, akisoma saut, aliwaongoza wanafunzi kudai haki zao, kama mikopo.
3. Ni mwanzilishi wa tawi la saut{chadema} mwanza, na amekuwa mweneyekiti pale
4. Aliwahi kukataa milioni 22 kutoka kwa makamba, ili amuachie kiti cha udiwani tarime zakaria
5. Amesaidia chadema kupata wanachama wengi katika mkoa wa mwanza, na mkoa jirani.
6. Hapendi ufisadi.
Hii ni kutokana na experince yangu kwa kipindi nikisoma nae saut
bwana sarwat umemnadi mtu wako vema unavyo mjua na sio kuenaza uzushi. Ndo maana unajitabulisha kwa jina lako na siyo la kihuni. Na wengine wakiwaandikia wanao wapenda hivyo tutapata uwanja mzuri wa kuwachagua.
 
Mchange anafaa kwa sababu ni Muislam,Greyson pia ni kutoka kanda nyingine.Saanane hafai kwa sababu chama kitaonekana kimedhamiria kukumbatia uchagga.Hata akichaguliwa atakuwa na makundi,atalipa visasi kwa watangulizi wake na wapinzani wake hasa hawa wabunge vijana ambao hawajamuunga mkono.Anaweza kuwalipizia kisasi kwenye uchaguzi wa ubunge 2015.Nimesoma nae india namjua.pia kuna mdau huku anaitwa Sizinga,mtetezi wangu nilipofungiwa na mods huku wengi mkiwa kimya.Ilikuwa ni njama ya kumlinda huyu jamaa nisimwage dataz zake,na siku hiyo kwenye uchaguzi nakuja
Hata kama ana CV nzuri,hatutaki tena tuonekane chama cha wachagga.Kwenye masters yake ya international Relations hana first class,nimesikia mtu mmoja akiwa anasema huyu jamaa ana first class kwenye international Relation,huo ni uzushi.

Ukweli ni kwamba kwenye uchumi ana First class.Kwani masters moja ilikuwa haimtoshi hadi akaenda kujiharibia CV? Nitamwaga dataz zote.Uchafu wake wa kutembea na mwalimu wake,hautoi picha nzuri kimaadili.Uchafu wake wa Kuvuruga chaguzi za watu wa kenya tutauweka hapa.Kwanza inabidi mumwangalie sana kwenye uchaguzi huu,hasa kesho.Hizo ndizo mbinu zake

Hapo kwenye red hapo,
Mnyika na Chadema wamekosea sana. Walipaswa kusema kwamba mtu ye yote ambaye ni mchaga asigombee ili CCM wasisema chadema ni ya wachaga. Ndicho ulichomaanisha mkuu? Sijakupata vizuri
 
Nimekuwa nikisoma threads mbalimbali hapa JF zinazojaribu kuonyesha kuwa viongozi wa CHADEMA wana wagombea katika uchaguzi wa vijana. Sitaki kuwasemea wenzangu. Isipokuwa mimi sina mgombea na nimekataa katakata kuwa na mgombea yeyote kwa faida ya chama. Mgogoro uliotokea wakati wa David Kafulila baada ya kuwa amemshinda ndugu John Heche na hatimaye Kafulila kuondoka katika chama ulikuwa ni mgogoro mkubwa ambao ulikiyumbisha chama. Niliapa kwa mungu wangu kutojihusisha tena na kwa namna yeyote ile na makundi ya chama ili chama kiwe salama na tujiandae vema na uchaguzi ujao.
Ninaomba nisihusishwe kabisa na uchaguzi wa BAVICHA. Wagombea wote waliokuja kuniomba msaada nimewaambia kuwa sitaki kwani sitaki makundi. Kama kuna wengine na hasa wabunge wanasaidia baadhi ya wagombea miye siwezi kuwasemea.

Kuhakikisha sijihusishi na uchaguzi huu, niliamua kutohudhuria kikao chochote cha chama kitakachojadili majina na sijahudhudhuria na hata Kamati Kuu ya suala hilo sijahudhuria. Pia niliamua kutohudhuria uchaguzi wenyewe ingawa mimi ni mpiga kura. Sitahudhuria.

Nitafanya kazi na kiongozi yeyote ambaye vijana watamchagua kwa matakwa yao na nainaomba watu wanaogozwa na mazoea tu kuwa Zitto na Mbowe wana makambi waondokane na mawazo hayo kwani mimi sina kambi wala kundi and i have submitted myself to the existing leadership.

Wenye ugonjwa wa Zittophobiasis watafute dawa tu as i wont give you the lines to attack. All my efforts are directed towards party building.

Mgombea yeyote ambaye atajisema eti ni wa Zitto nawaomba vijana wamkatae na wachague mtu wa CHADEMA na sio mtu wa kundi lolote.

Nawatakia wagombea wote ushindi mwema na ninawatakia vijana wote wa CHADEMA uchaguzi makini utakaoonyesha sura chanya ya chama chetu.

Zitto Kabwe
Naibu Katibu Mkuu Taifa
Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni
Waziri Kivuli Fedha na Uchumi
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma.
 
At last you have said it all.
Bravo Zitto.
 
Ben nadhani kila mtu ana mapungufu yake na hakuna aliyekamilika ila mapungufu yanazidiana kulingana na aina ya kashfa pia.

Kwa upande wangu sitaki kuamini kuwa wewe ni kiongozi ambaye unaonewa wivu na wengine na kwamba ni kampeni za ccm ambapo hapa watu wanamwaga ukweli wanaufahamu ili kutusaidia sisi wanachadema kuwa na uhakika wa yule tunayetaka kumpa dhamana ya kuongoza
maana kama wengine wangekuwa na mapungufu kama yako watu wasingenyamaza hata kidogo wangeleta habari zao na kukijenga chama tunawahitaji watu makini ili kupunguza mashambulizi ya ndani ya chama na kama kuna kiwingu chochote cha kashfa ni vizuri kukaa pembeni mwenyewe na uwapishe ambao hawana shutuma kubwakubwa nina imani kubwa na wewe na uongozi mzima wa CDM hasa mwenyekiti na katibu wake Dk. Silaa na ki ufundi wa mambo ya kisiasa utakuwa umemsaidia hata mwenyekiti wetu kusemwa kwamba anakupendelea kukubeba ingawa hauwezi kuwazuia watu kusema ubaya wa wengine lakini swali linakuja je kwa nini wakuseme wewe na siyo mtu mwingine yeyote tumia busara zaidi kuepusha makundi ndani ya chama chetu ubora wako uko palepale na itafika wakiti mzuri wa wewe kuipata nafasi unayoitaka kama utatumia busara muda huu kuliko kuja kuenguliwa baadaye.

Mungu ibariki CHADEMA

Mungu ibariki Tanzania
 
Wandugu,

Kuna majina nimeona hapo ni ya matapeli naomba nyie kama chama mfanyie uchunguzi msije kuingia aibu siku za mbeleni

Yangu hayo tu

Ahsanteni
 
The Following User Says Thank You to Zitto For This Useful Post:

King of Kings (Today)

kwa mara ya kwanza nimekogongea Thanks, kipindi kile ulikuwa unaleta mtafaruku cdm now umekomaa upepo umevuma upande wa pili

STAY FOCUSED KARIBU KUNDINI
 
Vijana nawakatakia kila jambo jema sana . Mnyika asante kwa taarifa hizi na Mungu Ibariki Chadema
 
Wandugu,

Kuna majina nimeona hapo ni ya matapeli naomba nyie kama chama mfanyie uchunguzi msije kuingia aibu siku za mbeleni

Yangu hayo tu

Ahsanteni
wataje ili wajulikane kabisaa! au unataka cdm kiwe kama magamba kumwingiza kimeo NApe
 
Natambua kwamba mnaenda kufanya Uchaguzi katika ili kuwapata Viongozi wa Taasisi nyeti kabisa katika Uhai wa Chama, siyo Taasisi ya Fedha bali ni Taasisi ya Vijana, Wenzenu CCM wanaiita UVCCM na ninyi mnaiita BAVICHA.

Kwenu CHADEMA Taifa

Natambua Nguvu ya Vijana katika Harakati za Kisiasa hasa Siasa za Kisasa na kwa kutambua kwangu huku leo nimeona ni Vyema nikatumia Jumapili yangu hii kuwaasa CHADEMA na BAVICHA kwa Ujumla.

Vijana ni kama Oil Kwenye Engine ya Gari, Chama Chochote kisichokuwa na Uungwaji mkono wa Vijana hicho chama ni Marehemu Mtarajiwa. Bahati Nzuri sana CHADEMA mna Bahati ya kukubalika na Vijana ingawa mpaka sasa ni Nguvu chache sana imetumika katika kuhakikisha hawa Vijana haitatokea hata siku moja wakageuka.

Ni Vizuri mkajifunza kwa CCM, CCM ilidharau Vijana na hata Umoja wao Ulikuwa ni kama Kijiwe cha watoto wa vigogo Kujifunzia Siasa ili waje kushika Tamu za Uongozi. Chonde chonde CHADEMA mkipita katika hiyo Njia Vijana watawahukumu. Naamini Mnaviongozi wazuri sana na Hamtaweza kuingia katika Mtego huo..

Mmefika hapo Mlipo sababu kubwa ni Vijana wengi kuvutiwa na Umakini wa viongozi vijana wa CHADEMA kama Zitto Kabwe, Halima Mdee, John Mnnyika na wengine wengi ambao nikiwaorodhesha nitakesha.

Tunaomba muwaache vijana washindane kwa Hoja ili Chama kipate Safu nzuri Uongozi wataoendeleza yale ambayo yameshafanywa.

Kwenu BAVICHA

Kwanza kabisa Nachukua nafasi hii kuwapongeza kwa Uamuzi wenu wa Kizalendo wa Kuamua Kujiunga na kugombea nafasi za Uongozi katika Chama ambacho si Tawala, ambacho hakuna uwezako wa ninyi kuula kama Kuteuliwa Ukuu wa Wilaya n.k

Ni Uamuzi Mgumu ikizingatiwa kwamba Mkiwa kama Vijana Mna ndoto za kuwa na Maisha Mazuri ili muwasaidie Wazazi wenu na Ndugu zetu. Wengi wenu kama si wote si Watoto wa Vigogo bali Mmeamua ku Risk Maisha yenu ili muweze Kuwatetea Watanzania kwa Ujumla. Wengi tulitamani tuwe kama Ninyi Lakini Ni Waoga, si Majasiri na Wabinafsi sana. lakini Napenda kuchukua Nafasi hii kwa Niaba ya Waoga wenzangu kuwapongeza kwa Ujasiri kwani Natambua Ujasiri wenu utakuja Kukumbukwa na Vizazi.

Natambua kwamba Nyote Mnaogombea nafasi hizi Mna sifa kwa Sababu Nimebahatika kuwasikiliza na Hakika Nikasema kama Kungekuwa na Uwezekano hakuna Haja ya Kufanya Uchaguzi na wote ningewatangaza kama Viongozi wa BAVICHA. Hakika CHADEMA ina kazi kubwa ya kuchuja maana vijana wote wanafaa

Natambua na Naamini kwamba Nanyi Mnatambua Kwamba Nafasi Mnazogombania Ziko Nne ( 4) Na ninyi mko zaidi ya Kumi ( 10). Hii ina maana kwamba Zaidi ye 50% ya wagombea lazima wakose Hizo Nafasi.

Kwa wale Wachache watakaopata Hizo Nafasi ni Bora wakashirikiana na wale waliokosa na wale wataokosa washirikiane na Wengine katika Harakati za Kukifanya CHADEMA chama kinachostahili kuchukua dola 2015.

Natambua katika Uchaguzi wowote kuna Makundi ( Hilo haliwezi kupingika). Ni vyema nasi mkatambua kwamba Makundi ni Silaha tu ya kushind uongozi lakini baada ya Uchaguzi ni lazima muwe kitu Kmoja katika kuendeleza harakati

Vijana ni Nguvu ya Chama, CHADEMA chukeni tahadhari

NAWATAKIA UCHAGUZI MWeMA
 
Nimekuwa nikisoma threads mbalimbali hapa JF zinazojaribu kuonyesha kuwa viongozi wa CHADEMA wana wagombea katika uchaguzi wa vijana. Sitaki kuwasemea wenzangu. Isipokuwa mimi sina mgombea na nimekataa katakata kuwa na mgombea yeyote kwa faida ya chama. Mgogoro uliotokea wakati wa David Kafulila baada ya kuwa amemshinda ndugu John Heche na hatimaye Kafulila kuondoka katika chama ulikuwa ni mgogoro mkubwa ambao ulikiyumbisha chama. Niliapa kwa mungu wangu kutojihusisha tena na kwa namna yeyote ile na makundi ya chama ili chama kiwe salama na tujiandae vema na uchaguzi ujao.
Ninaomba nisihusishwe kabisa na uchaguzi wa BAVICHA. Wagombea wote waliokuja kuniomba msaada nimewaambia kuwa sitaki kwani sitaki makundi. Kama kuna wengine na hasa wabunge wanasaidia baadhi ya wagombea miye siwezi kuwasemea.

Kuhakikisha sijihusishi na uchaguzi huu, niliamua kutohudhuria kikao chochote cha chama kitakachojadili majina na sijahudhudhuria na hata Kamati Kuu ya suala hilo sijahudhuria. Pia niliamua kutohudhuria uchaguzi wenyewe ingawa mimi ni mpiga kura. Sitahudhuria.

Nitafanya kazi na kiongozi yeyote ambaye vijana watamchagua kwa matakwa yao na nainaomba watu wanaogozwa na mazoea tu kuwa Zitto na Mbowe wana makambi waondokane na mawazo hayo kwani mimi sina kambi wala kundi and i have submitted myself to the existing leadership.

Wenye ugonjwa wa Zittophobiasis watafute dawa tu as i wont give you the lines to attack. All my efforts are directed towards party building.

Mgombea yeyote ambaye atajisema eti ni wa Zitto nawaomba vijana wamkatae na wachague mtu wa CHADEMA na sio mtu wa kundi lolote.

Nawatakia wagombea wote ushindi mwema na ninawatakia vijana wote wa CHADEMA uchaguzi makini utakaoonyesha sura chanya ya chama chetu.

Zitto Kabwe
Naibu Katibu Mkuu Taifa
Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni
Waziri Kivuli Fedha na Uchumi
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma.

Umejitanabaisha ni jinsi gani unastahili cheo, nafasi na heshima uliyojijengea. Naamini ulichosema unamaanisha!
 
Taarifa zilizopo; 1. Juliana Shonza 2. .......
 
Chadema mzee Mtei ametutoa mbali mamluki kwetu mwiko_Ole wao watakao ingia kwenye uongozi wa BAVICHA kwa kashfa na kama watakuwa Mamluki sisi kitengo muhimu cha CDM hatutavumilia kwani sisi tunaona Chama pekee ambacho kinatupatia uhuru na haki,amani na mwanga wa maisha ya baadaye ya watoto wetu ni CHADEMA.Nipo tayari kujitoa muhanga kwa ajili ya Uhai wa chama changu.NAOMBA WAGOMBEA WOTE WA UONGOZI NDANI YA BAVICHA KAMA KUNA YEYOTE ALIYETUMWA BASI AJIENGUE Mwenyewe kabla ajaingia kikaangoni.MUNGU IBARIKI TANZANIA,MUNGU WABARIKI VIJANA WA TANZANIA Na MUNGU IBARIKI CHADEMA Amen.
 
Back
Top Bottom