Du Bois ideas
JF-Expert Member
- Feb 1, 2011
- 427
- 82
Safu imekaa ki demkrasia kweli
CHADEMA Hawagawi vyeo, Uliwashauri vizuri wakamgawia yule mama..........aaaagggrrrrr.....nimeikumbuka sura yake tu nikapata kichefuchefuCdm ingependeza sana kama mngempa mwanadada ili muonekane kuwa mnajali
Wakuu Salaam.
Kamati Kuu ya dharura ya CHADEMA kukaa kesho kwa mujibu wa Katiba kwaajili ya kupitisha Wagombea nafasi mbalimbali katika Baraza la Vijana CHADEMA(BAVICHA).
Siku ya kesho ndio mtapata nafasi ya kujua idadi kamili ya Wagombea pamoja na majina yao.Uchaguzi unatarajiwa kufanyika Siku ya Jumamosi tarehe 28 Mei 2011 kama ilivyotangazwa hapo awali.
Kaeni Mkao wa Kula.
Kutoka Makao Makuu ya Chama
Regia E Mtema
Waziri Kivuli-Kazi na Ajira
Ndani y achadema hakuna kugawana vyeo, ni kugawana majukumuCdm ingependeza sana kama mngempa mwanadada ili muonekane kuwa mnajali
Wakuu Salaam.
Kamati Kuu ya dharura ya CHADEMA kukaa kesho kwa mujibu wa Katiba kwaajili ya kupitisha Wagombea nafasi mbalimbali katika Baraza la Vijana CHADEMA(BAVICHA).
Siku ya kesho ndio mtapata nafasi ya kujua idadi kamili ya Wagombea pamoja na majina yao.Uchaguzi unatarajiwa kufanyika Siku ya Jumamosi tarehe 28 Mei 2011 kama ilivyotangazwa hapo awali.
Kaeni Mkao wa Kula.
Kutoka Makao Makuu ya Chama
Regia E Mtema
Waziri Kivuli-Kazi na Ajira
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU ORODHA YA WAGOMBEA NA UTARATIBU WA UCHAGUZI WA BARAZA LA VIJANA WA CHADEMA (BAVICHA) NGAZI YA TAIFA
Taarifa inatolewa kwa umma kuhusu orodha ya wagombea waliorudisha fomu na utaratibu wa uchaguzi wa Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA) ngazi ya taifa kama ifuatavyo:
ORODHA YA WALIORUDISHA FOMU ZA KUGOMBEA:
Nafasi ya Mwenyekiti (Wagombea 10)
Aidan Sadik P.,
Benard A. Mao,
Benard Saanane,
Deogratias Kisandu,
Edwin Soko,
Greyson Nyakarungu,
Habib Mchange,
John Heche,
Masood S. Suleiman
Mtela Mwampamba.
Nafasi ya Makamu Mwenyekiti (Bara) (Wagombea 5) :
Emanuel Somoin,
Gwakisa B. Mwakasendo,
Joseph Patric,
Juliana Shonza
Julieth V. Rushuli.
Nafasi ya Makamu Mwenyekiti (Zanzibar) (Wagombea 3)-
Sharim S. Khamis,
Zainab B. Bakari
Ally Akalipo Ally.
Nafasi za Ujumbe: Wawakilishi wa BAVICHA kwenye Mkutano Mkuu wa chama-nafasi 20 (Wagombea 39) na wawakilishi wa BAVICHA kwenye Baraza Kuu la chama-nafasi 5 (Wagombea 32).
Wagombea waliorudisha fomu kwa nafasi za Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu, Mratibu wa Uhamasishaji, Mweka Hazina watatangazwa katika ratiba ya baadaye.
MIKUTANO YA UCHAGUZI:
Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Wawakilishi wa BAVICHA kwenye baraza kuu na mkutano mkuu watachaguliwa na Mkutano Mkuu wa BAVICHA utakaofanyika tarehe 28 Mei 2011 kama ilivyotangazwa awali. Wagombea husika wanakumbushwa kufika kwenye mkutano mkuu kwa gharama zao.
Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu, Mratibu wa Uhamasishaji na Mwekahazina watapendekezwa na Kamati ya Utendaji ya BAVICHA kwa mujibu wa ratiba itayopangwa baadaye na uteuzi wao utathibitishwa na Kamati Kuu ya chama hivyo wataalikwa katika vikao vya baadaye.
UCHUJAJI NA USIMAMIZI WA UCHAGUZI:Kwa mujibu wa katiba ya chama uchaguzi husika kwa kuwa ni wa kitaifa mkutano wake utasimamiwa na wazee wastaafu wa chama wakati katibu mkuu ndiye msimamizi wa uchaguzi katika taratibu zote kuanzia hatua ya awali.Aidha ngazi ya uchujaji itakuwa ni Kamati Kuu ya chama ambayo itafanya uteuzi wa wagombea katika kikao chake cha tarehe 26 Mei 2011 kwa kuwa ndiyo yenye wajibu wa kuyasimamia mabaraza kwa mujibu wa katiba na kanuni.
TARATIBU ZA KAMPENI: Kampeni za uchaguzi zitafanywa kwa kuzingatia kanuni za chama, maadili ya uongozi/viongozi (rejea kanuni za chama vifungu vya 10.1, 10.2 na 10.3) pamoja na muongozo juu ya uendeshaji wa uchaguzi ndani ya chama uliopitishwa na Baraza Kuu la Chama tarehe 13 Disemba 2007 unafafanua mambo yanayopaswa kufanywa na yasiyopaswa kufanywa wakati wa kampeni na uchaguzi ndani ya chamakwa lengo la kujenga mshikamano na umoja ndani ya chama na kufanya uchaguzi uwe huru na wa haki.
Wagombea wote wanahimizwa kuzingatia taratibu za kampeni za uchaguzi ambazo nakala yake inapatikana pia kwenye mtandao wa chama www.chadema.or.tz kutokana na umuhimu wa uongozi wa vijana kwa mustakabali wa chama na taifa kwa ujumla.
Kauli mbiu ya BAVICHA-Vijana; Nguvu ya Mabadiliko
John Mnyika (Mb)
Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Vijana
0784222222
UCHAGUZI WA BAVICHA KIZUNGUMKUTI.
-UCHAGUZI WA BAVICHA NI KIZUNGUMKUTI....nasema ni kizungumkuti kwa sababu unawagawa vijana wa chadema katika mapande manne mpaka sasa na hii inatokana na VIONGOZI WA JUU kupigana vikumbo katika nafasi ya MWENYEKITI WA TAIFA KATIKA UCHAGUZI UNAOKUJA waliorudisha fomu wengi wao wanabebwa na MAFISADI WA CHAMA.
1. BERNAD SAANANE
2.JOHN HECHE
3.EDWIN SOKO
watajwa hapo juu ni wateule wa mwenyekiti wa chama FREEMAN HAIKAEL MBOWE ndiye anapanga taratibu za kuhakikisha miongoni mwa vijana hao mmoja anakuwa mwenyekiti wa BAVICHA ili iwe rahisi kwake kupambana na MAHASIMU wake mbele ya safari, ngoma nzito hiyo kazi ipo watachakachuana mpaka wataota mbigili, sijui itakuaje maana HECHE aliwapiga vita sana akina HALIMA MDEE, LUCY OWENYA, SUZAN LIYMO, ANNA KOMU ili kuwepo na uchaguzi wa huru na wahaki viti maalum ubunge 2010 inasemekana alizunguka nchi nzima kuwa maliza na alfanikiwa maana timbwili timbwili kila mtanzania alilisikia na kuliona mwaka jana, sasa je atasalimika na ho ni wajumbe wa kamati kuu ya chadema? tusubiri.........yetu sie mijicho..............na misikio....................
1.HABIB MCHANGE.
2.GREYSON NYAKARUNGU.
3.MASOOD S. SULEIMAN.
-WATAJWA hapo juu hawa ni madogo wa KABWE ZUBIRI ZITTO yeye alipigania miongoni mwa vijana hawa mmoja awe ndie mwenyekiti wa BAVICHA sijui watasuguana namna gani, suala la ukanda linaweza wasaidia itategemea watakavyojieleza katika mkutano wa uchaguzi wao hiyo 28 may 2011 siku ya jumamosi, najua wabunge wengi wapya wachadema wanamsaidia HECHE KUCHUKUA HIYO NAFASI maana alisaidia pia kutetea japo kisirisiri ila kwa fitina kubwa iliyomtingisha FREEMAN HAIKAEL MBOWE mpaka sasa hajui hatma yake ya baadae maana KABWE ZUBERI ZITTO KESHA SEMA 2015 atagombea urais ndani ya CHADEMA.
-HALIMA MDEE/LUCY OWENYA/JONH MNYIKA/ wameunda timu yao ya kuhakikisha GREYSON NYAKARUNGU jina halipiti ndani ya kamati kuu kwani alihongwa na FISADI NIMROD MKONO asigombee musoma vijijini na zengwe linaendelea kwa kasi kubwa maana kikao kilichokaliwa cha siri siku mbili zilizopita kimepanga siku ya kikao cha kesho kuamsha moto wa ukweli juu ya kijana huyo.
-BERNAD SAANANE ni kijana lakini inaonekana hakubaliki na vijana wengi wa CDM maana anaonekana ni mgeni na MBOWE ana siri kubwa na kijana huyo watamalizana wenyewe hawa CDM, CV YAKE IMEJAA UZUSHI mwingi ambao akipatikana kijana aliyesoma India anaweza kuweka wazi baadhi ya mambo aliyoyaeleza.
-chadema hamna jipya mshatokota.