Kamati Kuu ya CHADEMA Kukutana Kesho Kupitisha Wagombea BAVICHA

Regia Mtema

R I P
Nov 21, 2009
2,970
864
Wakuu Salaam.

Kamati Kuu ya dharura ya CHADEMA kukaa kesho kwa mujibu wa Katiba kwaajili ya kupitisha Wagombea nafasi mbalimbali katika Baraza la Vijana CHADEMA(BAVICHA).

Siku ya kesho ndio mtapata nafasi ya kujua idadi kamili ya Wagombea pamoja na majina yao.Uchaguzi unatarajiwa kufanyika Siku ya Jumamosi tarehe 28 Mei 2011 kama ilivyotangazwa hapo awali.

Kaeni Mkao wa Kula.

Kutoka Makao Makuu ya Chama

Regia E Mtema
Waziri Kivuli-Kazi na Ajira
 
Wakuu Salaam.

Kamati Kuu ya dharura ya CHADEMA kukaa kesho kwa mujibu wa Katiba kwaajili ya kupitisha Wagombea nafasi mbalimbali katika Baraza la Vijana CHADEMA(BAVICHA).

Siku ya kesho ndio mtapata nafasi ya kujua idadi kamili ya Wagombea pamoja na majina yao.Uchaguzi unatarajiwa kufanyika Siku ya Jumamosi tarehe 28 Mei 2011 kama ilivyotangazwa hapo awali.

Kaeni Mkao wa Kula.

Kutoka Makao Makuu ya Chama

Regia E Mtema
Waziri Kivuli-Kazi na Ajira

Habari nzuri hii
Ila tuteulieni vijana wtakaofanya kazi
 
Thanx,Mh.Regia.Tunachoomba yale ya 2009 ya akina kafulila na Heche kura kuzidi idadi ya wapiga kura yasijitokeze tena.Mungu ibariki Cdm,mungu ibariki Tanzania.
 
kamati kuu kitengo cha intelgensia naamini kipo, kijitahidi kuwachunguza hawa wagombea kwa makini wasije kutuletea mamluki knye uongozi
 
Mtuletee wagombea ambao watakuwa majasili,wasio ogopa na kutishishiwa nyau,tunataka viongozi ambao si walarushwa watakao sema no kwa dhuruma na wizi unaotokea sasa

angalizo kusiwe na upendeleo wowote ule ktk process ya kuteuwa wagombea hao,
pamoja daima
niwatakie kazi njema hiyo kesho
 
All the best Chadema na mipango hii . Haki itendeke Regia waambie akina Slaa na wengineo huko . Wapeni haki waumane kwa haki akishindwa mtu aone kashindwa hakuna makundi hapa .
 
Sasa karibu tunaingia msimu mkuu wa siasa Tanzania.....a lot of evils zitakuwa revealed,just wait!
 
Sasa karibu tunaingia msimu mkuu wa siasa Tanzania.....a lot of evils zitakuwa revealed,just wait!

Hivi Tanzania kuna wakati ambao si wa siasa. hata hapa JF unaoa bajeti itayokuja tutaichambua kisiasa as usual.


BTN

Regia asante kwa taarifa endeleeni kusukuma hili gurudumu la mabadiliko
 
Hivi Tanzania kuna wakati ambao si wa siasa. hata hapa JF unaoa bajeti itayokuja tutaichambua kisiasa as usual.


BTN

Regia asante kwa taarifa endeleeni kusukuma hili gurudumu la mabadiliko
Utanielewa baada ya wiki
 
nawatakia uchaguzi mwema! hekima na busara zitangulie katika kuwapata viongozi watakaowakilisha vyema vijana katika medani ya siasa baada ya uvccm kukosa muelekeo.
 
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU ORODHA YA WAGOMBEA NA UTARATIBU WA UCHAGUZI WA BARAZA LA VIJANA WA CHADEMA (BAVICHA) NGAZI YA TAIFA


Taarifa inatolewa kwa umma kuhusu orodha ya wagombea waliorudisha fomu na utaratibu wa uchaguzi wa Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA) ngazi ya taifa kama ifuatavyo:

ORODHA YA WALIORUDISHA FOMU ZA KUGOMBEA:

Nafasi ya Mwenyekiti (Wagombea 10)
Aidan Sadik P.,
Benard A. Mao,
Benard Saanane,
Deogratias Kisandu,
Edwin Soko,
Greyson Nyakarungu,
Habib Mchange,
John Heche,
Masood S. Suleiman
Mtela Mwampamba.

Nafasi ya Makamu Mwenyekiti (Bara) (Wagombea 5) :
Emanuel Somoin,
Gwakisa B. Mwakasendo,
Joseph Patric,
Juliana Shonza
Julieth V. Rushuli.

Nafasi ya Makamu Mwenyekiti (Zanzibar) (Wagombea 3)-
Sharim S. Khamis,
Zainab B. Bakari
Ally Akalipo Ally.

Nafasi za Ujumbe: Wawakilishi wa BAVICHA kwenye Mkutano Mkuu wa chama-nafasi 20 (Wagombea 39) na wawakilishi wa BAVICHA kwenye Baraza Kuu la chama-nafasi 5 (Wagombea 32).

Wagombea waliorudisha fomu kwa nafasi za Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu, Mratibu wa Uhamasishaji, Mweka Hazina watatangazwa katika ratiba ya baadaye.

MIKUTANO YA UCHAGUZI:

Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Wawakilishi wa BAVICHA kwenye baraza kuu na mkutano mkuu watachaguliwa na Mkutano Mkuu wa BAVICHA utakaofanyika tarehe 28 Mei 2011 kama ilivyotangazwa awali. Wagombea husika wanakumbushwa kufika kwenye mkutano mkuu kwa gharama zao.

Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu, Mratibu wa Uhamasishaji na Mwekahazina watapendekezwa na Kamati ya Utendaji ya BAVICHA kwa mujibu wa ratiba itayopangwa baadaye na uteuzi wao utathibitishwa na Kamati Kuu ya chama hivyo wataalikwa katika vikao vya baadaye.

UCHUJAJI NA USIMAMIZI WA UCHAGUZI:Kwa mujibu wa katiba ya chama uchaguzi husika kwa kuwa ni wa kitaifa mkutano wake utasimamiwa na wazee wastaafu wa chama wakati katibu mkuu ndiye msimamizi wa uchaguzi katika taratibu zote kuanzia hatua ya awali.Aidha ngazi ya uchujaji itakuwa ni Kamati Kuu ya chama ambayo itafanya uteuzi wa wagombea katika kikao chake cha tarehe 26 Mei 2011 kwa kuwa ndiyo yenye wajibu wa kuyasimamia mabaraza kwa mujibu wa katiba na kanuni.

TARATIBU ZA KAMPENI: Kampeni za uchaguzi zitafanywa kwa kuzingatia kanuni za chama, maadili ya uongozi/viongozi (rejea kanuni za chama vifungu vya 10.1, 10.2 na 10.3) pamoja na muongozo juu ya uendeshaji wa uchaguzi ndani ya chama uliopitishwa na Baraza Kuu la Chama tarehe 13 Disemba 2007 unafafanua mambo yanayopaswa kufanywa na yasiyopaswa kufanywa wakati wa kampeni na uchaguzi ndani ya chamakwa lengo la kujenga mshikamano na umoja ndani ya chama na kufanya uchaguzi uwe huru na wa haki.

Wagombea wote wanahimizwa kuzingatia taratibu za kampeni za uchaguzi ambazo nakala yake inapatikana pia kwenye mtandao wa chama www.chadema.or.tz kutokana na umuhimu wa uongozi wa vijana kwa mustakabali wa chama na taifa kwa ujumla.

Kauli mbiu ya BAVICHA-Vijana; Nguvu ya Mabadiliko


John Mnyika (Mb)
Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Vijana
0784222222
 
i blamed you before,nafurahi kutujuza habari kama hizi,!
Now kitengo cha habari kina fanya kazi some how,here we go chadema!!
 
Mtoeni hapo huyo Dikteta Saanane,akafie Nyamongo kama anaamini katika radicalism kama dini,akaifie dini yake hiyo ya radicalism.Kama chadema tuko serious basi Mchange angeua sumu ya ubaguzi
 
Back
Top Bottom