Kamati Kuu ya CCM - Mtego unasao?

Nadhani mwisho wa EL kisiasa unaelekea ukingoni na pia ameonyesha wazi kwamba hajui kusoma alama za nyakati. Kama angekuwa smart angejiuliza mara 100000000 kwanini wananchi walishangilia sana waliposikia kwamba jamaa kaamua kuachia ngazi? Furaha haikuwa kwa wapinzani tu bali pia hata kwa wana CCM wenzake, mawaziri na wabunge. Huo ni ushahidi tosha kwamba wananchi na baadhi ya watu serikalini walishamchoka, walikuwa wakisubiri kwa hamu ni lini ataachia ngazi.

Kidudumtu ni yeye mwenyewe, maana alishasahau ile kasheshe ya akina Laizer (Mbunge wa Longido) na Elisa Mollel (Mbunge wa Arumeru) jinsi alivyowaingiza kwenye mkenge wa PCCB kiasi cha kuhatarisha hata uanachama wao wa CCM na pia kupoteza opportunity ya kugombea uongozi kwenye chama. Leo hii yeye kupewa dose kamili analalamika kwamba kaonewa! Mkuki kwa nguruwe ....!

Mbona hayo maelezo hakuyatoa Bungeni ili kuweka sawa record kwenye hansard? Maelezo ya kwenye mikutano hiyo ya hadhara hayana nguvu wala kumbukumbu ya kudumu. Kumbukumbu nzuri ingekuwa Bungeni ili watu tumuone anavyochemka. Sasa kwenda kuongea huko Mto wa Mbu ambako watu hawana hata uwezo wa ku-digest hotuba yake ni kujitafutia umaarufu mbele ya wachovu!

Hivi Balile ni Mwandishi wa Habari ama ni Mhariri wa Gazeti la Mtanzania?
 
“Tusimamie Ilani ya uchaguzi kwa mshikamano. Tukiyumba katika hili na tusipofanya hivyo, mwaka 2010 tutakuwa na maswali mengi sana na wapinzani wetu tutawapa fursa,”

Mie nina uhakika Kamati kuu haimuachi Lowassa,na hii itadhihirika wazi hivi karibuni,WMaacheni amalizie muda wake tu.CCM haiwezi kuanguka sababu ya Lowassa,akaendeleza Biashara zake,Kwanin lazima kila mtu afanye siasa?imetosha
 
Kuna kidudumtu ndani ya ccm zaidi ya Mtandao ambao yeye Lowassa ndiye architect? Mkuu amepigwa na matendo yake na pia unafiki wa kisiasa za bongo, za kumpa Salim uwaziri mkuu wa nchi, lakini akigombea urais wa nchi yetu anakuwa mwarabu na amemuua Karume,

Ndugu Lowassa, muosha hatimaye naye huoshwa pia, Sumaye na Salim, walipopigwa bao Dodoma kama wewe, walienda kwa Tinga Tinga, kuomba ushauri na wewe si ndiye aliyekuleta mjini kwa nini usiende kupata ushauri waliopewa wenzio, tena siku hizi hata Ben naye huomba ushauri huko, nenda tu mkuu na wewe ushauriwe badala ya kuwasumbua wananchi na hotuba ambazo ni hewa tupu!
 
Balile kahama Tanzania Daima kaenda kwa watu wa mtandao.Alinunuliwa mapema akiwa Hull University naona sasa kafika .Rostam na Rweyemamu walimfuata na sasa anatumiwa kuichafua Chadema na Mbowe karibuni kisa alikuwa mwandishi wa Tanzania Daima .

Lowas kwenda Chadema ? Mnaleta utani sana . Yaani Chadema wakae chini wampokee Lowasa ? Ama kweli nyie mlichoka hata kufikia maoni na mawazo haya .Yaani Chadema ya Zitti na Mnyika ?
 
Lowasa ni Mzigo Mkubwa hauziki hivyo hawezi kujiunga na chadema, TLP au hata chausta.

Nafikiri ataanzisha chama kipya. Chama hicho wafuasi wake watakuwa Karamagi, Rostam Azizi, Baadhi ya mawaziri wa JK, na wengine wengi waliochota pesa BOT nk.

Hiki chama hata kule Longido na Mto wa Mbu kitapigwa vita ambavyo siyo vya kawaida.

Wanachama wake nafikiri wanakuwa wanaogopa hata kupita machoni mwa watanzania. Watakuwa wanajiona kama wako watupu.

Huko kutaitwa kuangukia pua. KWa kifupi Mh. Lowasa katika siasa za tanzania kaangukia pua.
 
Kuna kidudumtu ndani ya ccm zaidi ya Mtandao ambao yeye Lowassa ndiye architect? Mkuu amepigwa na matendo yake na pia unafiki wa kisiasa za bongo, za kumpa Salim uwaziri mkuu wa nchi, lakini akigombea urais wa nchi yetu anakuwa mwarabu na amemuua Karume,

Ndugu Lowassa, muosha hatimaye naye huoshwa pia, Sumaye na Salim, walipopigwa bao Dodoma kama wewe, walienda kwa Tinga Tinga, kuomba ushauri na wewe si ndiye aliyekuleta mjini kwa nini usiende kupata ushauri waliopewa wenzio, tena siku hizi hata Ben naye huomba ushauri huko, nenda tu mkuu na wewe ushauriwe badala ya kuwasumbua wananchi na hotuba ambazo ni hewa tupu!

FMES mapenzi yako kwa TIngatinga ni ya kifani?Ndio Tingatinga ndiyo alimg'oa Lowassa,unadhani Lowassa anaweza kuwafuata wazee.Wamefanikisha walichokuwa wankitaka na Mama John Kilango Malecela atakula Ukuu wa Mkoa Hivi Karibuni.
 
CCM yagawanyika
`
:: Makundi yatishia uhai wake

na mwandishi wetu

YAPO mawazo miongoni mwa jamii kwamba yaliyotokea katika mkutano wa 10 wa bunge uliomalizika Dodoma hivi karibuni, ndiyo unaweza kuwa mwanzo wa kumomonyoka kwa Chama Cha Mapinduzi.

Mawazo hayo, yanatokana na ukweli kwamba yaliyotokea Dodoma, yanavinufaisha vyama vya upinzani ambavyo kwa muda wa miaka 16 vimekuwa vikitafuta mwanya bila mafanikio na kwamba nafasi hiyo imepatikana kwa CCM kuamua kujidhoofisha chenyewe.

Kilichotokea hapa ni kundi moja la hao lakini kila moja likifanya kazi kwa wakati wake na kundi jingine ni la wale waliodhani mambo yako safi lakini wakajikuta wakishtuliwa.

Katika hili, suala siyo Richmond na CCM ijiandae kwani baada ya suala la Richmond, yataibuka mambo mengi yatakayofanana na Richmond. Na kila moja litakuwa na mtikisiko wa aina yake. Kama tatizo lingekuwa Richmond, sasa tungekuwa tunaambiwa mmiliki wake na hata mmiliki wa Dowans tungekuwa tunamjua baada ya ripoti ya Kamati ya bunge.

Wachambuzi wa mambo ya siasa wanasema kuwa ndani ya Chama Cha Mapinduzi, siasa zake zimechafuka kweli kweli hali iliyolifanya bunge kuwa bunge la upinzani. Wapo wapinzani wa aina mbili; wale wa kawaida wa vyama, na wale wa ndani ya CCM ambao wanataka kujisafisha kwa wapiga kura wao.

Wachambuzi wa mambo wanasema kwa sasa tutarajie wabunge hawa kujiandaa kukusanya heshima yao ya majimboni kwa kujionyesha uwezo wao wa kuichachafya serikali yao. Na haya yakitokea mawaziri, makatibu wakuu na watendaji wengine wa serikali wataanza kufanya kazi zao kwa makini na kwa misingi ya sheria. Baadhi ya hizi sheria, ndiyo wabunge hawa wamekuwa wakizilalamikia kwamba zimepitwa na wakati. Kabla ya mapinduzi ya kikao cha bunge kilichopita, wabunge wangeweza kuivumilia serikali kama ingekunja sheria ili kuwezesha jambo fulani litekelezwe. Kwa sasa, itakuwa vigumu kwa sababu wabunge watakuwa macho kuangalia kitu chochote kinachokwenda kinyume na sheria. Watashambulia bila simile. Na hii itakuwa faraja kubwa kwa wabunge wa upinzani.

Kwa ujumla, bunge tangu lililopita hadi yajayo, ni mabunge ya upinzani. Wabunge wa CCM wanaona ufahari kujitambulisha na wabunge wa upinzani wakati katika kipindi kilichopita haikuwa hivyo. Wabunge wa CCM watataka kujionyesha kwamba wao ni wazalendo kwa kuwakumbatia na kuyakumbatia mawazo ya wapinzani. Ni kipindi cha neema kwa wapinzani iwapo watajipanga vizuri na wanaweza kuitumia kete hiyo katika majimbo.

Wachambuzi wa mambo ya siasa wanasema njia waliyoitafuta kwa muda wa miaka 16 sasa imewezeshwa na wana CCM wenyewe huku wapinzani wakichekelea.

Mwanasiasa mmoja wa upinzani, ametabiri kwamba katika hali kama hii, CCM haiwezi kutekeleza ahadi zake hata kwa asilimia 50 jambo litakalowafanya wapinzani kuibuka kidedea katika majimbo yao.

Kwa hali ilivyo sasa, wapinzani wachache waliomo bungeni, wamekwishajijengea mizizi kutokana na mambo yaliyopita. Hawana wasiwasi wa kupoteza majimbo yao.

Kwa upande wa CCM mambo ni tofauti kabisa. Hakuna nguvu ya pamoja tena kutokana na makundi yaliyomo. Wapo wachambuzi wa mambo wanaosema kwamba ushindi wa Kiteto unaonyesha njia nyeupe ya CCM kushinda katika uchaguzi ujao.

Hata hivyo, wachambuzi wengine wanasema Kiteto haiwezi kuwa kipimo kizuri kwa sababu ya mambo kadhaa. Kwanza nafasi hiyo ilikuwa ikijazwa ya mtu aliyefariki wa CCM. Hakuwapo ili kuhukumiwa na wananchi. Lakini ya pili, viongozi karibu wote walielekeza nguvu zao huko. Katika uchaguzi mkuu, kila mtu anakuwa katika jimbo lake akisulubiwa na wapiga kura wake.

Tatu kipindi cha miaka mitano kitakuwa kimepita, na ahadi za CCM ndiyo zitakuwa zikipimwa kama zimetekelezwa au la. Katika hali hiyo, wachambuzi wa mambo wanasema, CCM itakuwa na deni kwa wananchi ambalo itatakiwa kujibu.

Wachambuzi wa mambo wanasema uchaguzi mkuu ujao, utakuwa tofauti sana na uchaguzi wa miaka yote iliyopita kwa sababu ya watu kufunguka macho na uhuru wa watu kujieleza ambao umekuwa mpana katika kipindi cha awamu ya nne.

Hapo zamani, wachambuzi wanasema, wananchi walikuwa wakielezwa tu na wao kusikiliza, kupiga makofi au kuguna.

Lakini sasa, itakuwa ni zamu ya viongozi kueleza yale waliyoahidi na jinsi walivyoyatekeleza.

Hata hivyo, kiongozi mmoja wa upinzani, alipuuza mawazo kwamba upinzani nchini unaweza kuimarika kutokana na mgawanyiko ndani ya CCM.

“Kinachotokea ni kwamba CCM wanagombana wenyewe. Na ugomvi wao hautokani na tofauti ya ideology. Ni mambo yao tu ya mahusiano yao ndani ya chama. Ila kweli ninachokiona ni kwamba watapata taabu sana kutekeleza Ilani yao ya uchaguzi. Nakupa miaka mitatu, tuulizane,”alisema.

Kiongozi huyo ambaye alikuwa Kiteto katika uchaguzi wa Jimbo hilo, alisema ni vigumu sana upinzani kufaidika na magomvi ya CCM kwa sababu vyama vya upinzani ni vichanga katika nyanja nyingi.

“Sioni ni kwa jinsi gani upinzani utakavyofanikiwa. Sioni fall out (anguko) ya CCM kwa sababu hawajatofautiana kiitikadi na kama wangetofautiana kiitikadi, basi ingekuwa rahisi kwao kudondoka na sisi kufaidi,” alisema.

Akitolea mfano wa Kiteto, kiongozi huyo alisema CCM walishinda Kiteto kwa ubora wa mikakati na nguvu watu. “Sisi hatukuwa na human resources, hatukuwa na fedha wala mikakati. Tunafanya siasa katika old fashion (kizamani).

Kama tungeweza ku modernize opposition, tungeweza kufaidika na udhaifu huu wa CCM. Kwa kutumia uzoefu wao, CCM ikatumia kugawanyika kwa wana Kiteto kati ya wakulima na wafugaji na ikashinda,”alisema na kuongeza:

“Sisi tulijikita kwenye maeneo ya wakulima. CCM ikajikita katika maeneo ya wafugaji. Ikahakikisha kuwa iko na wafugaji. CCM ilikoshinda ilishinda kweli kweli. Kwa mfano kati Kata ya Ndedo CCM ilipata kura 992 na sisi tukapata kura 22. Kule Makami CCM walipata kura 940 na sisi tukapata 11.

Haya ni maeneo ya Wamasai hasa. Watu waliojitokeza kupiga kura walikuwa zaidi ya asilimai 70. Kwa upande wetu, wapiga kura katika maeneo waliyotuunga mkono walikuwa wachache sana. Kwa mfano eneo moja, wapiga kura waliojiandikisha walikuwa 11,000, waliojitokeza walikuwa 5,000. CHADEMA tukapata asilimia 56 tu. Kwenye wafugaji CCM iliwekeza na kushinda zaidi ya asilimia 80. Kwetu tulishinda lakini margin ndogo. CCM, ilijua waliojiandikisha. Sisi hatukujua,” alisema na kuongeza kuwa heri ya vyama vya upinzani, ni kama makundi haya ya CCM yataamua kugawanyika na kuzaa chama kingine.

The only way ni sprit ya ccm kama matatizo ya sasa yatageuka kuwa ideological yawagawe katika makundi mawili. Au kungekuwa na high profile individual wakaingia kule.

RAI
 
Mwenzenu keshapima yote. Sasa hivi mwenyewe anasema hana cha kupoteza. Ila zimeanza kumrudia baada ya siku chache zilizopita kumkandia mzee hadharani. Tunawaachia Lowassa tunaendelea na mgeni mpya. I like the new guy.

Asante.
 
Mwenzenu keshapima yote. Sasa hivi mwenyewe anasema hana cha kupoteza. Ila zimeanza kumrudia baada ya siku chache zilizopita kumkandia mzee hadharani. Tunawaachia Lowassa tunaendelea na mgeni mpya. I like the new guy.

Asante.


Nimeptea kabisa na comments zako .Hebu niweke sawa
 
Hakuondoka hivi hivi bali alidai kilichofanyika ni "Njama" tena njama kama ile iliyosimuliwa kwenye "maajabu ya mlima Kolelo".Ilikuwa ni njama ambayo kutisha kwake kulikuwa kama hadithi za "Mizimu ya Watu wa Kale". Ni Njama hii iliyomuudhi Lowassa na kuamua kuanza kuandaa "Kikosi cha Kisasi".

Mwanakijiji,

Kwani yeye amekuwa Ndelawasi?:confused:
 
Kwa mujibu wa Katiba ya CCM Kamati Kuu ya CCM ina jukumu la "Kutoa uongozi wa siasa nchini"


Kwa kuangalia historia ya Kamati Kuu ni wazi kuwa chombo hicho bado kina nguvu ya kuweza kuingilia jambo lolote na wana uwezo wa kumchukulia hatua mwanachama wao yeyote yule ambaye siyo tu anatishia maslahi ya chama hicho bali pia anatishia hali ya mwelekeo wa kisiasa nchini.

Vibwengo "Kidudumtu"

Historia ya CCM inaonesha kuwa hawakusita kuwachukulia hatua watu kama Aboud Jumbe, Seif Sharrif Hamad na wenzake, Horace Kolimba na viongozi kadha wa kadha pale inapobidi
.


Lakini swali ambalo ni la kujibiwa kabla ya kufika huko ni je JK anaweza kuleta mizengwe ya kiCCM na kutumia fimbo yake ya Uenyekiti wa CCM kuvunja daima urafiki wake na Lowassa? Kwa upande wa Lowassa swali analohitaji kujibu kabla ya kugongana na KK ni je anakubalika kiasi gani kwa wananchi wa kawaida kiasi cha kuweza kumrudisha Bungeni kwa tiketi ya chama kingine chochote kile?


Nakubaliana na wengi huko juu,huu sio mtego kwa EL, bali kwa JK mwenyewe!

MM, JK and group? wanahitaji kushinda 2010-ili aendeleeeze sera zake (Ilani ya CCM?)- Nafikiri anaelewa maana ya kuwa 'Raisi wa muhula mmoja Tanzania'

'Vibwengo' hii nimeitoa kwa "Kidudumtu" rejea hapo juu...CCM inahitaji kurejesha imani kwa wananchama wake kwanza, na kwa nguvu hizi-nafikiri hii inaonekana- EL pamoja na 'Uswaiba' inawezekana akapigwa na Vibwengo vya CCM.:cool:

Je Lowassa anakubalika?

Tunaweza kusema kwa uhakiki kama huu ndi utarajio wa 'CCM B'?
Nani atanasa?

Tuangalie hizo moves sasa!
 
Chadema, kwa maoni yangu haistahili kabisa kumchukua Lowassa. Wamchukue kwa lipi hasa atakaloweza kuwasaidia Chadema? Makombo ya CCM yakubaliwe na Chadema?, NO WAY! watakuwa wamefanya kosa kubwa sana. Anaweza akaacha historia nzuri kama atakuwa mkweli na kusema ufisadi wote anaoufahamu kuhusu kashfa mbali mbali za ndani ya serikali

asilimia 70 ya viongozi wa upnzani ni makombo ya CCM au walikuwa wanachama wa CCM, Mpinzani mzuri wa kuibomoa CCM atatoka ndani ya CCM, ni nani na ni lini subiri mtaniambia na si siku nyingi toka sasa.


Wabillah Tawfiq
 
Kitendo cha Naiko kuleta swala la ukabila kwenye Richmond ni kosa kubwa sana.

Mi nashindwa kuelewa mtu kama Naiko anadai kwamba ameonewa kwa sababu ya ukabila. Jamani Lowassa ni mmeru si mmasai kama anavyodai na Naiko anajuwa wazi hilo
 
Butiama kuitikisa CCM

na Mwandishi Wetu

HALI ya kisiasa ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) si shwari na taarifa za hivi karibuni zinaonyesha kuwa makundi ya kisiasa ndani ya chama hicho yameshaanza kujipanga kwa ajili ya kushitakiana ndani ya vikao vikubwa viwili vitakavyoitishwa baadaye mwezi huu.

Taarifa za uhakika ambazo Tanzania Daima imezipata kutoka ndani ya chama hicho zinaeleza kwamba, wajumbe wanaounda makundi hayo ambayo yamechipua kutokana na Kashfa ya Richmond wameshaanza kufanya mashauriano ya namna ya kukabiliana wakati wa vikao vya Kamati Kuu na baadaye Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho.

Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, kinatarajiwa kufanyika baadaye mwezi huu Butiama, ambako ndiko nyumbani na mahali alikozikwa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere.

Vyanzo vya habari vya kuaminika kutoka ndani ya makundi hayo mawili, moja likiwa ni lile lililofanikisha kuanguka kwa aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, na jingine linalojaribu kumsafisha yeye na wenzake wengine kadhaa tayari yanaonyesha mwelekeo wa kujipanga, tayari kukabiliana na mwenendo huo wa mambo.

Mmoja wa makada maarufu wa chama hicho anayetoka katika kundi linaloshangilia kuanguka kwa Lowassa, Nazir Karamagi na kusakamwa kwa mfanyabiashara Rostam Aziz, aliieleza Tanzania Daima mwishoni mwa wiki iliyopita kuwa tayari walikuwa wameshajipanga kwa ajili ya kukamilisha kazi hiyo.

Mwana CCM huyo ambaye ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho, alisema tayari wameshaanza kufuatilia kile walichokiita nyendo za Lowassa na wana CCM wenzake wengine wanaomuunga mkono ili kuweza kupata msingi imara wa kujenga hoja zao dhidi ya kundi hilo.

Kada huyo machachari wa CCM alisema miongoni mwa hadidu za rejea ambazo watazitumia kummaliza Lowassa, Rostam, Karamagi na wanasiasa wenzao wa kundi hilo ni kauli walizozitoa nje ya Bunge dhidi ya ripoti ya Kamati Teule ya Bunge iliyoongozwa na Mbunge wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe.

Kwa mujibu wa kada huyo, watu kadhaa wenye msimamo kama wake tayari wameshaanza kukusanya vielelezo na kujenga hoja ambazo wanaamini wakizitumia zitasaidia kuzima jitihada zozote zinazoonekana kuanza za Lowassa na wana CCM wenzake kujisafisha.

Kundi hilo la wana CCM, kwa kutumia kivuli cha Rais Kikwete, limepanga kwenda kummaliza Lowassa ndani ya NEC kwa kile kinachodaiwa kuwa ni kutoa kauli zinazokinzana na wabunge wenzake wa CCM, wakati walipokuwa wakimkaanga Lowassa ndani ya Bunge hadi kujiuzulu wadhifa wake.

“Lowassa amefanya mambo ya ajabu, amekichafua chama, anataka kujikosha kwa jambo la wazi kabisa ili wabunge wa CCM waonekana kuwa wamemwonea. Safari hii tunaenda kupambana naye ndani ya chama Butiama,” kilisema chanzo chetu cha habari.

Mbali ya Lowassa, kundi hilo linataka pia chama hicho kitoe karipio kali dhidi ya Rostam na Karamagi kutokana na kile wanachokieleza kuwa ni kukitia doa chama na serikali, kwa sababu tu ya kuweka kwao mbele masilahi ya kibiashara kuliko ya umma.

Katika kufanikisha hilo, kundi hilo limepanga kuitumia hotuba ya mwishoni mwa mwezi Januari ya Rais Kikwete ambaye pamoja na mambo mengine, alieleza kuhusu dhamira yake ya kutenganisha shughuli za kisiasa na zile za kibiashara, hasa katika ubunge na uwaziri.

Habari zaidi kutoka ndani ya kundi hilo la kwanza zinaeleza kwamba, iwapo mkakati wao huo utakwama ndani ya chama, basi hatua itakayofuata itakuwa ni kuupeleka bungeni ambako wataitumia Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kuwachukulia hatua Lowassa na wenzake kadhaa wanaodaiwa kutoa kauli ambazo zinaonyesha dharau kwa Bunge.

Wakati kundi hilo la kwanza likijipanga kwa ajili ya kupigilia msumari wa mwisho katika kile wanachokiona kuwa ni ‘jeneza la kisiasa’ la kina Lowassa, Rostam na Karamagi, upande wa pili nao unaonekana kujipanga kwa ajili ya kulikabili kundi hilo la kwanza.

Habari ambazo Tanzania Daima imezipata kutoka katika kundi hilo la pili zinaonyesha kuwa, nalo limeanza kukusanya vielelezo kadhaa ambavyo wanataka kuvitumia kwa lengo la kukishawishi chama chao kuwa Kashfa ya Richmond ilikuwa na lengo la kuwadhalilisha, kuwaumiza na kuwamaliza kisiasa.

“We will definitely hit back (Ni wazi kwamba tutajibu mapigo). Hatuwezi tukakaa kimya wakati tukijua waziwazi kwamba watu hawa wameazimia kutuumiza kwa malengo ya kisiasa.

“Hii si haki hata kidogo, mtu unazushiwa uongo wa wazi halafu watu wanakuwa washangiliaji. Ni jambo baya kwamba taasisi za kisheria zimefanya ‘mob justice’ (zinachukua sheria mikononi).

“Hili hatuwezi kukubali liendelee. You wait and see,” alisema mmoja wa wanasiasa hao waliotajwa katika sakata la Richmond ambalo lilisababisha Lowassa ajiuzulu uwaziri mkuu huku Karamagi na Dk. Ibrahim Msabaha wakijiuzulu nyadhifa zao za uwaziri.

Kauli ya mwanasiasa huyo kwa kiwango fulani inatoa mwelekeo kama ule uliotolewa na Karamagi ambaye wakati alipofanya mahojiano na gazeti hili zaidi ya wiki mbili zilizopita alieleza bayana dhamira yake ya kutumia vikao halali vya chama kuwashitaki wale wote aliosema walikuwa wameamua kumshutumu kwa kumuonea.

Wakati hali ikionekana kuwa hivyo, vyanzo vilivyo karibu na Lowassa, vinaeleza kuwa mwanasiasa huyo ameendelea kulalamika kuhusu kile kilichotokea akisema hakuhusika kwa namna yoyote katika kuileta au kuipigania Richmond ili ishinde zabuni ya kuzalisha umeme wa dharura.

Nje ya majukwa ya siasa, inaelezwa kwamba, kwa mara ya mwisho, Lowassa alibainisha msimamo wake huo wakati maaskofu wa makanisa kadhaa nchini walipokwenda kumtembelea na kumfariji nyumbani kwake Monduli alikokwenda kuwaeleza wapiga kura wake kile kilichosababisha kujiuzulu kwake.

Siku chache tu baada ya Lowassa kuhojiwa na TvT na baadaye kuzungumza katika mikutano ya hadhara kuhusu sakata hilo la Richmond, Spika wa Bunge alikaririwa na vyombo kadhaa vya habari akionya kuhusu kuwapo kwa uwezekano wa Bunge kuchukua hatua iwapo itathibitika kuwa kulikuwa na kudharauriwa kwa taasisi hiyo muhimu.

Baadhi ya wadadisi wa mambo waliozungumza na Tanzania Daima wanasema, hitimisho la suala hilo ndani ya CCM, litakuwa kipimo muhimu cha utendaji wa kazi na uwezo wa kuhimili vishindo vya kisiasa wa Rais Kikwete ambaye ni Mwenyekiti wa Taifa wa CCM.

Source: Tanzania Daima
 
Naamini Nyerere hata kama alikufa mzimu wake uko hai. Sasa wanaenda Butiama kumsimanga maana aliyokuwa anayakataa wao wameyatanguliza mbele.
Ole wenu CCM, kama mtamsimanga baba wa Taifa, hakika hamtarudi kama mlivyoenda.
Kuweni makini na mtakayojadili na kuamua, kamwe mafisadi wasionewe huruma. Kamati kuu iundwe upya maana Rostam Aziz amalalamikiwa, Chenge amelalamikiwa, Lowassa hana mamlaka tena. Hao kama wataendelea kubaki kamati kuu, nini mwelekeo wa CCM katika kupambana na ufisadi?
 
Nahisi kuna watu hata hapa JF bado wanafikiri CCM bado ni ileile ya Nyerere, tena yenyewe majanja yameamua kupeleka mkutano hukohuko kwa Nyerere ili kuwapumbaza wananchi zaidi. Kufikiria kwamba kamati kuu hii ya Kikwete inaweza kuwashughulikia mafisadi katika CCM ni sawa na kutaka mbuzi ale nyama. Sanasana watakachojadili huko ni namna ya kuweka mikakati ya kuficha ufisadi ili watakapoyafisadi mahela yetu tusijue. Wataweka mikakati kuwashughulika watumishi wote wa serikali ambao wamekuwa wakilikisha taarifa za ufisadi.
 
Huu mtego naona wala haunasi.. ni kama mtego wa bui bui ambao unashindwa kunasa hata nzi!
 
Kamati Kuu ilishaishiwa meno yake sasa ni butu kama mdomo wa kibogoyo.......
 
Back
Top Bottom