Kamati Kuu CHADEMA yawavua Uanachama Madiwani 2 Jiji la Mwanza

Kamati kuu imechemka, ilipaswa iwape ONYO then mengine ndio yafuatwe! ADAMU CHAGULANI NI KIONGOZI MWENYE UDHUBUTU, VERY INFLUENCIAL! CDM JIPANGENI!
 
kama kabla ya kufukuzwa waliitwa na kamati kuu, wakajieleza na kupewa natural justice THEN Mimi sioni tatizo kufukuzwa kwao! Heri kuwa na madiwani 3 waaminifu kwa chama kuliko wengi ambao ni Mapandikizi ya ccm!
 
Owawa Stephen J
CHADEMA yawavua uanachama madiwani wawili wa mkoa wa Mwanza na kuvunja Uongozi wa Chama Mkoa uku madawani wote wakipewa onyo kali,Maamuzi haya yameniumiza sana kwani moja wa aliyevuliwa uanachama ni Adam Ibrahim Chagulani diwani wa Igoma, Mwanaharakati mahiri tangu tukiwa UDSM.

Nini mustakabali wa Vijana ndani ya Vyama vya Siasa?

Sasa ulitegemea nini, na huyo Adam Ibrahim.
 
Tukiwapa urais sitashangaa kuona mnamvua rais wa nchi uanachama tunaanza kuhangaika kurudi kwenye makatiba na tafsiri za kisheria.
Siyo kweli,demokrasia yo yote ina gharama yake. Chama (iwe CCM,CUF,CDM) kuna taratibu na kanuni zinazosimamia viongozi. Miiko ya uongozi ni muhimu kutekelezwa,
 
Hakuna kiongozi africa aliyeilewa maana halisi ya demokrasia, hata kama aliielewa basi hawezi kuiruhusu imuumize yeye. Zitto Kabwe alianza kusaka sign 70 za wabunge ili wamuondoe waziri mkuu akaungwa mkono na wabunge wengi hata wa CCM, sikuona wala kusikia wakiguna ila tulishangilia sana, kwani ilikua njia pekee na sahihi ya kikanuni ya kuiwajibisha serikali, leo hii meya wa mwanza aliyefail kazi tangu achaguliwe hata kwenye mkutano pale furahisha mimi nikiwepo nilishuhudia wananchi wakimzomea mbele ya mzee Slaa na Mbowe,

Leo anakingiwa kifua na kufukuzisha wanachama uanachama ikiwa ni juhudi za wenje kwa hofu ya ubunge 2015, Wenje kahamia Dsm anaongoza jimbo kwa simu hajui lolote la Mwanza isipokuwa kwa simu tu na endapo tatizo likitokea yeye huja mwanza na kufanya mkutano nyuma ya pazia la kuitupia lawama CCM zote na kwa kuwa watu wameichoka CCM basi huamini kila asemalo ..

Ushauri kwa Wenje, kwa kuwa amefanikiwa juhudi zote za kumuondoa uanachama chagulani na matata, juhudi alizokuwa akizifanya kupitia viongozi wa juu wa chama kwa kuwadanganya, juhudi nilizowahi kuonana nae mara kadhaa pale G&G hotel mwanza na malaika hotel akiwa na jopo la wanachama alowatengeneza kuhakikisha anamuondoa chagulani, amefanikiwa ila ajue kuwa anatakiwa ajiandae kuishi Mwanza kama kweli anataka kuendelea kuw amgombea wa ubunge Mwanza...Mwanza ninavyoijua kumekucha sasas
 
Udikteta wa kuwanyamazisha watu. Na hii ni kwasababu udiwani hauongezi ruzuku.
Mbona Shibuda hawawezi kumfuta?

ni sawa kufukuzwa lazima atakuwa anamatatizo ,dr huwa atakagi upuuzi .kumbuka chadema wanaenda kuchukua nchi .wapuuzi kama wa gamba hawana nafasi cdm,
 
Arusha walivuliwa watano na huko tena wawili chadema kpo makini hatulei mafisad waende kwa mafisad wenzao ccm
 
Owawa Stephen J
CHADEMA yawavua uanachama madiwani wawili wa mkoa wa Mwanza na kuvunja Uongozi wa Chama Mkoa uku madawani wote wakipewa onyo kali,Maamuzi haya yameniumiza sana kwani moja wa aliyevuliwa uanachama ni Adam Ibrahim Chagulani diwani wa Igoma, Mwanaharakati mahiri tangu tukiwa UDSM.

Nini mustakabali wa Vijana ndani ya Vyama vya Siasa?

Umahiri wake na ujana wake hautuzuii kufanya maamuzi magumu.
Pia hata kama mngesoma naye havard, kilichozingatiwa hapa ni katiba ya chadema.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Safi sana,kuna watu ndani ya CDM hujiona kama miungu watu kisa walijenga chama.Hakuna mtu maarufu zaidi ya chama hata Dr Slaa au Mbowe akifanya upuuzi afukuzwe mchana kweupe.Tunawafundisha CCM ili watakapokuwa upinzani wawe imara
 
Hivi hao kamati ku hawakuona adhabu nyingine kwa makosa kama haya zaidi ya kufukuzana? Haya wakiendelea kufukuzana hivi watabakia wangapi!
 
haki kama imetendekea sawa ila kama haijatendeka waangalie upya kuna nini hapo na wajue kuna akina Dialo na Marsha wanafanya kazi wakikutana na vijana njaa kuwarubuni ni rahisi sana ili 2015 warudi ulingoni
 
Hivi hao kamati ku hawakuona adhabu nyingine kwa makosa kama haya zaidi ya kufukuzana? Haya wakiendelea kufukuzana hivi watabakia wangapi!

Adhabu "hazitungwi" utakavyo wewe. Kila kitu kipo documented kwenye Katiba na miongozo mingine ya chama. Wala hakuna cha kuwapa muda "wale krismasi na mwaka mpya"; wala hakuna cha gamba, wala nini? Kila kitu kiko clear and open.
 
Back
Top Bottom