Kamati Kuu CHADEMA yawavua Uanachama Madiwani 2 Jiji la Mwanza

Owawa Stephen J
CHADEMA yawavua uanachama madiwani wawili wa mkoa wa Mwanza na kuvunja Uongozi wa Chama Mkoa uku madawani wote wakipewa onyo kali,Maamuzi haya yameniumiza sana kwani moja wa aliyevuliwa uanachama ni Adam Ibrahim Chagulani diwani wa Igoma, Mwanaharakati mahiri tangu tukiwa UDSM.

Nini mustakabali wa Vijana ndani ya Vyama vya Siasa?
 
Huyo Meya si imeonekana alishindwa kazi? Yaani CHADEMA nao mtu akiwa mwiba kwa viongozi walioshindwa kazi anafutwa uanachama!!!
 
Tukiwapa urais sitashangaa kuona mnamvua rais wa nchi uanachama tunaanza kuhangaika kurudi kwenye makatiba na tafsiri za kisheria.
 
Ndio maana nawaambia vijana kila siku ukombozi mnaouzungumza mdomoni hautoshi, ingieni field muone kazi ilivyo ngumu. Sasa huyu Chagulani pamoja na jitihada zake za kuijengea CHADEMA imani kwa wanamwanza ambao wameshakuwa disappoited na CHADEMA anaishia kufutwa uanachama!!!
 
Last week alikuwa EATV alionekana yuko very composed na alisema hatagombea umeya kwa sababu lengo lake ni kukijenga chama. Mara anafutwa uanachama...duh, kweli kuishi kwingi kuona mengi!
 
Ki ukweli huyo diwani wa igoma alilewa sifa na anatabia kama za Zitto. Siku zote aliwaza atakuwa meya alipopigwa chini alianza kuwashawishi watu wamchukie mbunge Wenje. Baada ya kuongoza BAVICHA kichwa kilimpanda akadhani anaweza kupata cheo chochote kama wamemtimua safi sana.
 
Kama walifanya hujuma kwa CDM ni vema walivyofukuzwa maana hao ni wahaini kabisa maana haiwezekani wahujumu chama kwa kushirikiana na CCM
 
sielewielewi hapa,kama ilisemekana meya alivuliwa umeya kwa kuvurunda,iweje madiwani wawajibishwe.??
 
Owawa Stephen J
CHADEMA yawavua uanachama madiwani wawili wa mkoa wa Mwanza na kuvunja Uongozi wa Chama Mkoa uku madawani wote wakipewa onyo kali,Maamuzi haya yameniumiza sana kwani moja wa aliyevuliwa uanachama ni Adam Ibrahim Chagulani diwani wa Igoma, Mwanaharakati mahiri tangu tukiwa UDSM.

Nini mustakabali wa Vijana ndani ya Vyama vya Siasa?

Huyo Chagulani anapenda madaraka sana alipochaguliwa tu alianza kampeni za umeya ila hakufanikiwa. Alipokuwa m/kiti bavicha ilemela akadhani anaweza kumtoa Wenje relini. Unafiki wake uliendelea mpaka akaanza kampeni za kumuengua Meya kwa tuhuma feki za kanisa la Wasabato. Huyo jamaa yako kiukweli anapenda cheap popularity kama Zitto na Kafulila. Mzee wa Magnum club (H. Matata) ni kama Shibuda.
 
njia yoyote ya kuelekea kwenye ukombozi huwa ni ngumu. kuna miba mingi sana hadi uufikie huo ukombozi. kwa hivyo basi hao madiwani ni miiba inayotuchelewesha tusiifikie njia hiyo. tumeshaing'oa tusonge mbele hadi tufike 2015. kama kuna mingine njiani inataka kutublock, bora ijiondoe mapema b4 haijafikiwa na dhoruba ya cdm. VIVA CDM.
 
Owawa Stephen J
CHADEMA yawavua uanachama madiwani wawili wa mkoa wa Mwanza na kuvunja Uongozi wa Chama Mkoa uku madawani wote wakipewa onyo kali,Maamuzi haya yameniumiza sana kwani moja wa aliyevuliwa uanachama ni Adam Ibrahim Chagulani diwani wa Igoma, Mwanaharakati mahiri tangu tukiwa UDSM.

Nini mustakabali wa Vijana ndani ya Vyama vya Siasa?
Owawa,pole sana kwa kuguswa na jambo hili,na nadhani wote tumeguswa.sikumfahamu chagulani ila nilikutana naye wakati wa uchaguzi wa bavicha huu uliompa heche uenyekiti.mimi ni mwanafalsafa,nilisikiliza tu hoja zake,yeye,mtu anaitwa Ben,na mwakagila.baada ya kuchambua upeo wao haraka japo sikujua historia yao niliwashauri na ninakujibu swali lako la mustakabali wa vijana kwenye vyama vya siasa.jibu lako na ndicho niliwaambia wakati ule ni Vijana waache ujinga na kudhani siasa za daruso ziko applicable hata kwenye platform ya taifa.chadema kujitanabahisha kuwa chama cha vijana haimaanishi kwa mtizamo wangu kuwa sasa vijana hata wahuni,wasiojali wanaweza kupenya.kwa hiyo vijana wa chadema na hata ccm na wote kama swali lilivouliza tuwe watulivu na kuwa na nidhamu.
 
Ni ADAMU CHAGULANI IGOMA NA HENRY MATATA KITANGIRI
Pia Imevunja uongozi wote wa chadema mkoa wa mwanza.sababu kuhujumu chama na kumvua umeya meya wa chadema kinyume na utaratibu wakishirikiana na maccm na serikali
Kwa hiyo mwizi akiwa CHADEMA poa tu!
Mbona mnakosa upeo na kurudia makosa yale yale ya CCM.
 
Back
Top Bottom