Kamati kuu CHADEMA kufunika Arusha Alhamisi

Freeman Mbowe,Willibroad Slaa, Zitto Kabwe Peter Msigwa, Regia Mtema, Heche Suguta, Chiku Abwao Ezekia Wenje, Tundu Lissu, Kasululu Malima, Lazaro Masai, Jaffar Maiko, Godbless Lema na madiwani wengine wa Jiji la Arusha

Hili ni kongamano, warsha, semina au ni mgao wa ruzuku? Ndio maana wengi walihamaki baada ya Mallah kumaliza huu mgogoro maana unafaidisha wengi sana.
 
Hili ni kongamano, warsha, semina au ni mgao wa ruzuku? Ndio maana wengi walihamaki baada ya Mallah kumaliza huu mgogoro maana unafaidisha wengi sana.
Ndio maana hamtaki kuwavua magamba ili mgogoro uendelee Nape azidi kula ruzuku ya kuzunguka mikoani kuhubiri kitu kisichokuwepo.
 
nawatakia kila laheri makamanda wote. Mapambano yanendelea. Kwanza nina hasira sana, mgao mkali sana
 

Kichwa kimoja kinapambana na zaidi ya vichwa mia tano. Hivi siku mkimfukuza Shibuda si mtabeba na Billcanas casino muende nayo kwa wasukuma maana kwa madiwani imebidi muende na chama chote.
 
Mmmh sijui wanakuja Arusha kutuambia jinsi walivyo wafukuza madiwani! Kweli magwanda ni hatari wanaua,wanafukuza halafu wanahutubia tena watu walewale eneo lile lile,mji ule ule! Hakika UMeya Wa Arusha Umewatesa sana Magwanda(mgambo)!
 
Mungu awape nguvu,uwezo na hekima iliyotukuka wote waiongozao CHADEMA!Busara awajazie na ulinzi awape!All the best!i'l be there if possible
 
acheni uongo mbona shibuda hamkumfukuza, madiwani wa chadema bado ni madiwani halali wanaenda mahakamani kupinga kuvuliwa udiwani.
 
Ni mkakati ambao unasthili pongezi kwa watu wenye fikira chanya
ktk mageuzi ya kisiasa ya dhati na harakati mpya za siasa za kweli ktk
Tanzania mpya.

Naipongeza CC kwa uamuzi huo wa kuamua kuto mrejesho kwa
wana Arusha,chama makini lazima kifanye hivyo yaani kuwafuata
wananchi na kuwaeleza maamuzi yaliyofikiwa,bila hofu kuwa wakereketwa
watasusia mkutano kwa hili CDM nawapongeza,

CCM ktk harakati zao geresha za kujivua gamba RA aliachia ngazi kwa sababu
ya siasa uchwara ndani ya ccm akiwatupia lawama lukuki nape na chiligati
mpaka leo si mukama,jk wala nape amekanyaga Igunga kuonesha kusikitishwa
na kauli ya RA kwa wanaigunga.Good start CHADEMA......tunawaelewa na wengine
wataelewa kama si leo nikesho.Ikumbukwe pia ktk kilio cha kupinga kubakwa kwa
Demokrasia ktk uchaguzi wa Meya timu nzima ilikuwepo,rudini makamanda muwapa WTZ mrejesho.
 
Chadema kimeandaa mkutano mkubwa wa hadhara mjini Arusha Alhamisi wiki hii utakao ongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Freeman Mbowe Kwa kushirikiana na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Willibroad Slaa, Naibu Katibu Mkuu, Zitto Kabwe na wajumbe wa CC.


Wajumbe wa CC watakaokwenda kuhutubia mkutano huo ni Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa; Mbunge wa Viti Maalum, Regia Mtema; Mwenyekiti wa baraza la Vijana Taifa wa chama hicho, Heche Suguta; Mbunge wa Viti Maalum, Chiku Abwao na Mbunge wa Nyamagana Ezekia Wenje.

Wengine ni Mbunge wa Singida Mashariki na Mnadhimu wa kambi ya upinzani bungeni, Tundu Lissu; Meya wa Manispaa ya Musoma, Kasululu Malima; Mwenyekiti wa Halmashauri ya Karatu, Lazaro Masai, na Mwenyekiti Manispaa ya Moshi, Jaffar Maiko. Pia atakuwapo Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema na madiwani wengine wa Jiji la Arusha.

Madiwani waliofukuzwa

attachment.php


Kutoka kushoto: Estomih Mallah wa Kata ya Kimandolu, John Bayo wa Kata ya Elerai, Ruben Ngowi wa Kata ya Themi, Rehema Mohamed wa Viti Maalum na Charles Mpanda wa Kata ya kaloleni.

Source: Nipashe

lets wait and see!!
 
Kama KAMATI KUU YA CHADEMA ...

Ingejiuma uma mdomo na kufikicha vidole ..kwa aibu kama ya kibinti ...

Ingitia aibu isio na kifani ... Imefanya kilichopaswa kufanyika ... na kilichotegemewa na wananchi wote wa Arusha na Taifa la Tanznaia

Ingeshindwa kuwavua gamba madiwani watano ..kamati ingekuwa haina tofauti na kamati kuu ya CCM

Chadema ..bila kujali matokeo ..imebidi ionyeshe kile walichoshindwa CCM kwa kuoneana haya ..na kumumunya maneno na kila mmoja akisubiri nani atakuwa wa kwanza kusonga mbele...Huo ni woga ulilifikisha Taifa la Tanznaia hapa lilipo.

Kama CCM ingeefanya walichofanya Chadema sasa ...wangekifanya mapema ... Baada tu ya kashafa za EPA..Meremeta na uchafu mwingine zillipojitokeza...Leo Taifa lingukwa na heshima na nidhamu ya hali ya juu ..usingesikia Vituo vya mafuta vya goma, Askari wa migodi waua
....wanafunzi wa vyo wagoma.., wasukuma mikokoteni wajichukulia sheria mikononi ..na migawanyiko yote ya aibu inayoikuba Taifa...

KISA KUCHEKEANA NA KUBEMBELEZANA KWENYE MAMABO YA MSINGI ....

Kusita sita mbela ya Rostam, Lowasa na Chenge ...ADUI aliwezakusoma CCM na Sereakali yake kuwa ni dhaifu , haina ushujaa na udhubutu wowote ...leo kila mtu ni Rais wa nchi kwa namana yake... kila mtu hategemei uogozi wowote kujiogoza...kila kijikundi kinajiogoza na kujichukulia sheri mikononi nk...SHAME!!!

Kwa nini..

Kulindana... kuogopana ..kutetemekeana ..Na kutoweka mstaari ulionyooka wa maamuzi mazito..kwa masilahi ya sasa na sikuzijazo ya Taifa.

Kamati kuu ya Chadema ..Mna heshima na mnawajibikia Chama na nidhamu ya Taifa..mmefanya kile kilichoshindikana CCM HAKUNAKUKUNA KICHWA WALA KUTETEREKA ..MKO SAHIHI SANA ... MNA SAPOTI YOTE ..KUANZIA KWA MUNGU HADI TAIFA LOTE!!

WANANCHI WOTE WA ARUSHA WAMELIONA HILO NA HAKUNA KULALA KWENYE KUVUA GAMBA 5 (CHANAGA...HAZIJAKOMAA)... NA KUWEKA CHAMA KWENYE MSTAARI!!

HI;O NDILO CHIMBUKO LA DEMOKRASIA YA KWELI YA MAENDELEO...

NANI ANABISHA ..AJITOKEZE TUMUONE...NA AIBU ZAKE!!!
 
acheni uongo mbona shibuda hamkumfukuza, madiwani wa chadema bado ni madiwani halali wanaenda mahakamani kupinga kuvuliwa udiwani.
Utasemaje bado madiwani wakati hata mahakamani hawajafika au huo udiwani unawapa kwa mamlaka uliyojipa nyuma ya laptop.
 
Nimesikitika sana kuona kuwa hata viti maalum alikuwa anatunishia CC kifua!

Hongera kwa mara nyingine CC-CDM kwa maamuzi magumu ya kufuta historia chafu iliyotaka kuletwa na viongozi wenyewe tamaa binafsi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom