Kamati kuu CCM yamtosa Hussein Bashe, adaiwa si raia wa Tanzania

Mkuu ninasaka sana habari za uchaguzi Mkoa wa Tabora, kwa bahati mbaya hazipatikani au kama zinapatikana basi uandishi wake uko nusu nusu. Ina maana mkoa wangu hauna wawakilishi/waandishi wa magazeti?
Kuna mengi yanayotokea. Kwamba hakuna waandishi hilo siliamini, siamini pia kuwa kuna tatizo la mawasiliano... kwa wengi hiki ni kipindi cha kuhangaika sana... nadhani, kuna nguvu inadhibiti waandishi huko Tabora
 
Huyu mwandishi wa Mwananchi anapaswa kuendelea kuwabana wale waliotrangaza kuwa Bashe si raia watpe ufafanuzi. Na kama ningekuwa Bashe ninge....
 
Kuna mengi yanayotokea. Kwamba hakuna waandishi hilo siliamini, siamini pia kuwa kuna tatizo la mawasiliano... kwa wengi hiki ni kipindi cha kuhangaika sana... nadhani, kuna nguvu inadhibiti waandishi huko Tabora

Hapo kwenye bold ninaweza kukuunga mkono. Unajua nimekuwa nikifuatilia habari za uchaguzi kwenye huo mkoa, lakini ukizipata ziko nusu au hazipatikani kabisa.

Mfano, nadhani last week nilisoma mahali mwandishi alikuwa anaongelea mgogoro wa CCM wilaya ya Uyui. Mwishoni akasema CCM inakabiliwa na upinzani katika majimbo ya Nzega, Tabora Mjini, Sikonge na Igalula kama sikosei. Nikawa more interested kujua ni wagombea gani waliosimamishwa kwenye hayo majimbo kutoka vyama vya upinzani. Sikupata jibu.

Juzi, HabariLeo, wakaandika kwamba CHADEMA wajipanga kuchukua majimbo 6 kati ya 9 ya Mkoani Tabora. Mwandishi wa habari hakutaja hayo majimbo wala wagombea wake. On other hand, in the same newspaper mwandishi mwingine akiwa anaongelea wagombea wa CCM alitaja majina na majimbo wanayogombea, sasa nikawa najiuliza, kwanini waandishi wanatoa info nusu?

May be kuna mtu anashughulikia ku-censor news kwa ajili ya damage control.
 
Hivi Bashe hawezi kumfungulia mashtaka Mzee Makamba/CCM kwa kumchafulia jina? sheria zinasemaje juu ya hili?
 
Waache waendelee kuchezea vichwa vya watu. Hata hivyo inabidi wajue kuwa ipo siku watanyolewa wao kwani mwosha huoshwa!!

Kwa mtaji huo Masha anathibitisha kuwa JK na nyau wake wote ni vilaza kiasi kwamba hawawezi kusoma na kuelewa nyaraka muhimu kama hizo? Halafu kabla ya kufanya huo upuuzi wao kwa nini hawakumuuliza Masha?

Na hivi Masha anajua uzito wa kauli zake hizo anazotoa wakati boss wake ndiye alikuwa kinara wa kumvua bashe uraia?
 
that cant happen ever in history,when the ccm party knows their faults kept as series and not considering the lost in action.
 
Back
Top Bottom