Kamanda nzowa kaudangaya umma, ukweli huu hapa

palalisote

JF-Expert Member
Aug 4, 2010
8,335
1,455
Kwanza huyo mtuhumiwa na wenzie hawakukamatwa na cocain kama anvyo sema , wao walikamatwa na heroin. Pili thamani ya heroin waliyokamatwa nayo ni billioni 2.8 ambayo ni sawa na kilo 18 (Kilomoja ni wastani wa million 156 source:http://www.idmu.co.uk/heroin-price-trends.htm ). Tatu wote si watanzania na hakuna ushahidi wowote kuwa dennis ni mchungaji. Kamanda Nzowa anatakiwa atupe ushaidi kututhibitishia ni mchungaji otherwise wameshindwa kumtaja huyo mchungaji na kubaki kutapatapa.


KATIKA PICHA HAPA CHINI: RAIA wanne wa kigeni, Dennis Okechukwu na Paul Obi wote wa Nigeria, Stani Hycenth wa Afrika Kusini na Shoaib Muhammad Ayaz kutoka Pakistan wakitoka kusomewa mashitaka ya kula njama na kuingiza nchini dawa za kulevya aina ya heroin zenye thamani ya sh. bilioni 2.8, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mjini Dar es Salaam, leo. (Picha kwa hisani ya Chachandudaily.blogspot.com).​


 
Kadanganya vipi basi...Onyesha amekosea wapi, ili tuujue ukweli, maana ulichofanya ni ku-post picha tu..
 
Umemwona askofu kwenye hizo picha?

askofu ndio huyo ukechuku ama mwingine? maana kuna thread inamtaja okechuku kama ni mmoja wa viongozi wa dini,lakini si mtanzania hapo ndipo napojiuliza mahusiano yaliyopo kati ya huyo okachuku na maaskofu wa tz
 
Huyu mchumia tumbo alikuwa anajigamba. Ngoja maskofu watakavyomshukia maana masaa 48 yameisha na hakuna aliyetajwa,hawatakurupuka kama ikulu na huyu mchumia tumbo anayejaribu kumtetea bosi wake kwa kutumia evidence za uongo.
 
Kamanda nzowa alisema Okechukuni mchungaji wa tanzania, kumbe ni raia wa Nigeria!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Hapo bado tunakazi kubwa wa ndugu.
 
hata hivyo Denis sio mchungaji wala askofu! halafu mbona IKULU ilijibu tofauti na NZOWA?
 
MODS kwa hisani yako naomba hii thread ipelekwe kwenye jukwaa la siasa. hii habari inabidi ingaliwe kwa jicho la kisiasa maana Nzowa amejitokeza maada ya zoezi la 'ziba mdomo' toka kwa Kikwete huko Mbinga. Tafadhali sana.
 
Ha ha ha ha ha ha....nasema hivi huyu J.Kiwete kwa hawa Maaskofu hajateleza tu bali tayari kaanguka na yuko chini anagalagala kwenye matope...ataiona PhD yake ilivookuwa ya kuchonga,ya hisani na si kushika kalamu kama ya Mzee wa watu,dakta wa ukweli,PhD holder,S.Peter
 
Hujui Kusoma? maelezo juu ya picha wewe hujayasoma?

Nzowa mwenyewe ana tuhuma za kubambikia watu madawa ya kulevya tutamwaminije na hajasafisha tuhuma za Mengi? Halafu kwanini taarifa atoe leo baada ya boss wake Jk kubanwa mbavu?
Uongo mtupu na upuuzi. Hawa tunawa-mark nchi ikichukuliwa tu lazima watafute taifa la kwenba kuishi siyo Tz.
 
Nzowa mwenyewe ana tuhuma za kubambikia watu madawa ya kulevya tutamwaminije na hajasafisha tuhuma za Mengi? Halafu kwanini taarifa atoe leo baada ya boss wake Jk kubanwa mbavu?
Uongo mtupu na upuuzi. Hawa tunawa-mark nchi ikichukuliwa tu lazima watafute taifa la kwenba kuishi siyo Tz.

Uko sahihi mkuu, alitakiwa sasa awe ansota rumande kwa ujahili wake!
 
Kichwa cha habari kingetakiwa kiwe
"Kikwete amedanganywa tena"kwani
ukisoma hakuna mahali hii habari
inasema hawa ni wachungaji au
maaskofu wa Tanzania
 
Kichwa cha habari kingetakiwa kiwe
"Kikwete amedanganywa tena"kwani
ukisoma hakuna mahali hii habari
inasema hawa ni wachungaji au
maaskofu wa Tanzania
Muheshimiwa rais ajasema wachungaji na wala maaskofu amesema vita imekuwa ngumu cos hata watumishi wa mungu wamejiingiza ktk biashara hiyo,huyo nzowa yy amelopoka tu.
 
Du. Kazi kweli kweli. Sidhani Kama rais alisema maskofiu alisema viongozi. Wa dini. Labda mashekh au masinga singa au mabudha wapangani
 
Du. Kazi kweli kweli. Sidhani Kama rais alisema maskofiu alisema viongozi. Wa dini. Labda mashekh au masinga singa au mabudha wapangani
Lakini si shehe alijitokeza kwenye luninga debating on the same: nadhani wao hawana dini hivyo rai ya JK haiwahusu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom