Kamanda mwema OCD huyu hatufai tuondolee Lindi

bamku

JF-Expert Member
Aug 15, 2012
538
427
Kuna kijana mmoja mfanyabiashara hapa Lindi mjini anaitwa OLIVER.

Ameachana na mkewe na mkewe amefungua kesi ya madai ambapo inabidi amlipe mkewe sh.10,000,000/= kwa vile mali walichuma pamoja. Siku ya sikukuu ya iDD EL FITR huyu kijana alienda nyumbani kwa mtalaka mwenzie na gari lake kumuomba waende kwenye sherehe pamoja mwanamke huyu alikubali.

Kilichotokea ni kwamba akiwa ndani ya gari Oliver alimpiga sana kwa nia ya kutaka kumuua, aliopoona amepoteza fahamu alimtupa polini maeneo ya mmongo barabara ya DSM.

kwa bahati mzuri yule dada alizinduka alfajiri baada ya kupigwa na upepo wa asubuhi akajivuta barabarani na dereva mmoja wa bodaboda akamuona na kumpeleka nyumbani. ndugu yake wakamchukua kupeleka polisi. Baada ya kutoa maelezo polisi OCD akamwambia ndugu wa yule dada akamkamate huyo kijana amlete polisi.

Ndugu wa dada alikasilika sana akaenda kuwasiliana na RPC. RPC alimuuliza OCD kuhusu kuwepo kwa tukio hilo na akatoa amri amkamate huyo kijana. Kwa sasa kijana kakimbia ameenda DSM.
 
Kuna kijana mmoja mfanyabiashara hapa Lindi mjini anaitwa OLIVER. Ameachana na mkewe na mkewe amefungua kesi ya madai ambapo inabidi amlipe mkewe sh.10,000,000/= kwa vile mali walichuma pamoja. Siku ya sikukuu ya iDD EL FITR huyu kijana alienda nyumbani kwa mtalaka mwenzie na gari lake kumuomba waende kwenye sherehe pamoja mwanamke huyu alikubali.Kilichotokea ni kwamba akiwa ndani ya gari Oliver alimpiga sana kwa nia ya kutaka kumuua, aliopoona amepoteza fahamu alimtupa polini maeneo ya mmongo barabara ya DSM. kwa bahati mzuri yule dada alizinduka alfajiri baada ya kupigwa na upepo wa asubuhi akajivuta barabarani na dereva mmoja wa bodaboda akamuona na kumpeleka nyumbani. ndugu yake wakamchukua kupeleka polisi. Baada ya kutoa maelezo polisi OCD akamwambia ndugu wa yule dada akamkamate huyo kijana amlete polisi . Ndugu wa dada alikasilika sana akaenda kuwasiliana na RPC. RPC alimuuliza OCD kuhusu kuwepo kwa tukio hilo na akatoa amri amkamate huyo kijana. Kwa sasa kijana kakimbia ameenda DSM.

Kisa hiki nilikifatilia jana kwenye kituo kimoja cha redio lakini mwema mwenye hatakiwi sasa sijui nani aanze kutoka....
 
Kisa hiki nilikifatilia jana kwenye kituo kimoja cha redio lakini mwema mwenye hatakiwi sasa sijui nani aanze kutoka....

ndo hapo sasa, full sarakasi, mchafu sana amsafishe mchafu mwenzie ambaye anajifunza kuchafuka sana ili na yeye aje awe mchafu kupindukia, ha ha haaa!!!!!


Tuendeleeni kuwaelimisha watanzania, waelimike ili waling'oe madarakani hili li-serikali la ccm MAONGO/MAFISADI/MAJAMBAZI/WAUAJI.
 
aanze mwema. Kuna uovu mwingi uko chini yake. Atakayekuja atasafisha wote!

mwema anatimiza miaka 60 mwakani, mkuu wa kaya kamuomba aongeze mkataba kakataa, matusi anayotukanwa kwa ubovu wa watendaji wake, ameyachoka, anataka kupumzika sasa. bt mwema kafanya mengi mazuri zaidi ya mara 100 ya mahita.
 
Duu hawa wakuu na viongozi ndani ya Serikali wanapaswa kukumbuka..

"Ni vizuri kujitahidi kutenda wema japo kidogo tu ili kutokumpa wakati mgumu mshereheshaji au MC, kutafuta maneno mazuri ya kumpamba marehemu siku anapofikwa na mauti."

Hivi, ni kwanini baadhi ya viongozi huwa hawajifunzi kutenda wema japo Kiduchu?
 
Back
Top Bottom