Kamanda Kova asilaumiwe!

mwangalizi

JF-Expert Member
Apr 24, 2012
842
512
Ndugu wanaJF, humu ndani kumejaa lawama na laana kwa kamanda wetu kipenzi, Kova. Najua uchungu uliopo mioyoni mwa watz wengi. Lakini tujiulize au tuvae viatu vya kamanda wetu;
- Je mwenyewe alipenda alicho kitangaza?
- Hakujua mwitikio wa watz utakuwaje?
- Je yeye ni mjinga?

Hakika majibu yetu sote ni HAPANA!

Kwa nini sasa?

ANA WAKATI MGUMU MAISHANI MWAKE KAMA KAMANDA!!! Tumtie moyo tu. Au mnadhani sikio linaweza kupita kichwa?
 
- Je mwenyewe alipenda alicho kitangaza? No idea
- Hakujua mwitikio wa watz utakuwaje? Must have an idea kuwa watu si wajinga
- Je yeye ni mjinga? Yes, kama unajua kabisa issue hata wewe huiamini kwanini usiseme kuwa kuna mtu tume mkamata tunaendelea na uchunguzi, kwanini akimbilie kutangaza?
 
Ndugu wanaJF, humu ndani kumejaa lawama na laana kwa kamanda wetu kipenzi, Kova. Najua uchungu uliopo mioyoni mwa watz wengi. Lakini tujiulize au tuvae viatu vya kamanda wetu;
- Je mwenyewe alipenda alicho kitangaza?
- Hakujua mwitikio wa watz utakuwaje?
- Je yeye ni mjinga?

Hakika majibu yetu sote ni HAPANA!

Kwa nini sasa?

ANA WAKATI MGUMU MAISHANI MWAKE KAMA KAMANDA!!! Tumtie moyo tu. Au mnadhani sikio linaweza kupita kichwa?

Kweli kabisa Mkuu, wana JF wengi would radher shoot the messenger kuliko kusikia message yenyewe.

Wengine wanachangia utafikiri Kova ndiye kamleta huyo Joshua Gitau a.k.a. Gun Gangster.
 
Hakuna lolote hapo mkuu, kova alijua na anajua anachokifanya... Msifikiri watanzania wote ni wajinga.
 
Kova angejiuzulu kama ni mwadilifu kuliko kutumiwa na Dhaifuz' government kukwepa lawama za umma tukio ambalo hajafanikiwa..
 
Hakuna lolote hapo mkuu, kova alijua na anajua anachokifanya... Msifikiri watanzania wote ni wajinga.
Sasa nyie mnaolielewa tukio zima lilikuwaje mbona hamjafungua ripoti popote pale hata kwa kutumia lile kundi la haki za binadamu?
 
KOVA yote aliyajua na angekuwa muungwana na muadilifu kwa Mungu na Watanzania angejiuzuru kabla ya kutangaza upuuzi huo, kwa mtazamo wangu lawama na laana zote zinamuendea yeye kwanza aliyefikisha ujumbe huo hakuna mwingine.
 
Unadhani alaumiwe nani? Maana mie hata ningekuwa nimevaa viatu vyake kamwe siwezi kutangaza huo ujinga unless kama mtu ushawahi kufanya kazi katika kampuni ya security ya kutoa mmbwa vinginevyo ni wendawazimu... Kwa mtu kujitoa ufaham na kutangaza kitu ambacho mtu yoyote hata akienda kuwaambia wale wamirembe watakataaa..
 
Kova angejiuzulu kama ni mwadilifu kuliko kutumiwa na Dhaifuz' government kukwepa lawama za umma tukio ambalo hajafanikiwa..

Tatizo ugali kaka! Fani yake hii akijiuzulu labda akaajiriwe Security Companies, ambako mshahara ni kimo cha mbuzi, na yeye ameshazoea kimo cha twiga; huoni kuwa ni wakati mgumu?
 
Jason bourne tangu adanganye jukwaa kakimbia kabisa maana thread kama hii angesema yeye ndio alimuandikia ile Statement Kova na kumlazimisha aisome.
Jamani nauliza tu lile kontena la visu walivyoingizaCUF ambalo tulitangaziwa na Mahita liko wapi?
 
Last edited by a moderator:
Sasa nyie mnaolielewa tukio zima lilikuwaje mbona hamjafungua ripoti popote pale hata kwa kutumia lile kundi la haki za binadamu?
Tunahitaji ukweli na sio ubabaishaji kama huu unaoendelea. Serikali inatakiwa kuunda tume huru ili itupe ukweli na sio kutupa ripoti kupitia vyombo vyake dhalimu. Hatuna imani na ripoti za aina hii tena kwa sababu imani yetu ni kwamba serikali ndio inahusika na tukio hili la utekaji wa Dr. Ulimboka, na hii ripoti ya kamanda kova ni kiini macho kinachotumika ili kupotosha ukweli.
 
Tatizo la kova ni kupenda sana sifa na coverage,akiambiwa atangaze lolote atafanya so long as kuna camera...pambaf zake...
 
hivi kova si ndiye aliyeunda tume ya polisi ya uchunguzi,je kwenye tv ndo kwenye tume,ampeleke huyo mkenya kwenye tume ya msangi ili aunganishwe na uchunguzi wa awali au anataka kutuambia ile tume yake ilikuwa haina ilichokuwa imeanza kufanya.
na kama ilishaanza kazi kwa nini mkimbilie mahakamani haoni hiyo itamzuia kuendelea na upelelezi kwa sababu atakuwa anaingilia uhuru wa mahakama.

vichekesho vitupu.
 
tuache lawama Kova hana budi, kwani hata Hakimu naye vivyo hivyo kwani jamaa keshaenda Segerea hajabinywa wala kuhojiwa atakaporudi hiyo Agosti 5 utaambiwa ushahidi haujakamilishwa, Mwendesha mashtaka nae mtaanza kumlaumu. Basi mwenye ushahidi kamili aende kuutoa mahakamani
 
Ndugu wanaJF, humu ndani kumejaa lawama na laana kwa kamanda wetu kipenzi, Kova. Najua uchungu uliopo mioyoni mwa watz wengi. Lakini tujiulize au tuvae viatu vya kamanda wetu;
- Je mwenyewe alipenda alicho kitangaza?
- Hakujua mwitikio wa watz utakuwaje?
- Je yeye ni mjinga?

Hakika majibu yetu sote ni HAPANA!

Kwa nini sasa?

ANA WAKATI MGUMU MAISHANI MWAKE KAMA KAMANDA!!! Tumtie moyo tu. Au mnadhani sikio linaweza kupita kichwa?

Kamanda Kova anastahili lawama zote kwa kuwa amekubali kuwa kibaraka wa viongozi wachache. Kuna mengi tu ambayo tuna uhakika kuwa anatumiwa na yeye ameridhika kwa kuwa na yeye ni mchumia tumbo tu. Kama angekuwa hapendi anachokifanya angeandika barua ya kujiuzuru uone kama anayetaka kumtumia hatorudi nyuma. Kova ni kiongozi goigoi ndia maana ameridhika kuwa kibaraka/kuwadi wa wengine. Kova hana usafi unaotaka tuuamini kuwa anao. Moron!!
 
Ni vyema kutomjadili huyu aliyetumwa na magamba.Huyu hana jipya zaidi ya kutetea ugali wake.Atakuja juta cdm tutakapochukua uongozi wa nchi hii kwa sababu wote waliohusika katika kuifanya nchi kuwa maskini na kudharaulika watawajibishwa ipasavyo
 
Ndugu wanaJF, humu ndani kumejaa lawama na laana kwa kamanda wetu kipenzi, Kova. Najua uchungu uliopo mioyoni mwa watz wengi. Lakini tujiulize au tuvae viatu vya kamanda wetu;
- Je mwenyewe alipenda alicho kitangaza?
- Hakujua mwitikio wa watz utakuwaje?
- Je yeye ni mjinga?

Hakika majibu yetu sote ni HAPANA!

Kwa nini sasa?

ANA WAKATI MGUMU MAISHANI MWAKE KAMA KAMANDA!!! Tumtie moyo tu. Au mnadhani sikio linaweza kupita kichwa?

Ni kweli kwa upande wako, uyasemayo kuwa kamanda kova asilaumiwe. Bosi wake mwenyewe alishawahi kusema kuwa ' za kuambiwa changanya na zako' Afande kova alitakiwa kufikiri kabla ya kutenda ni kama vile kutoa maamuzi kabla ya kumrushia risasi mhalifu. Atalaumiwa kwa kutotumia akili zake kwa ufasaha na umakini,

Huwa najiuliza, Mtu kama Kova, hivi ana dini kweli?

Anafanya hivi kwa maslahi ya nani? Taifa, jeshi, raisi au familia yake?
NAPATA UTATA KUWA KAMA HUYU KAMANDA KOVA ANAFIKIRI SAWA SAWA.
KOVA NA SERIKALI ANAYOITETEA WAJUE KUWA WATANZANIA WA LEO SI WA JANA. JANJA WANAYOTUMIA HAINA NA HAIWEZI KULETA MASHIKO VICHWANI MWA WATANZANIA.
KWA UJUMLA ALITAKIWA KUFIKIRI KABLA YA KUUTANGAZIA UMMA JUU YA UPUUZI WAO.
NAWASILISHA.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom