Kamanda Kamuhanda: Siwezi kujiuzulu

naombeni namba yake tafadhali....


RPC IRINGA
con_tel.png

+255 715009921
 
Hapa sio suala la kujiuzulu, na wala sisi hatuombi RPC Kamuhanda ajiuzulu. Akishajiuzulu so what? Ndio kanawa mikono au? TUNACHOTAKA NI RPC KAMUHANDA APANDISHWE KIZIMBANI KWA MAUAJI YA MWANGOSI (RIP).
 
JUMAMOSI, SEPTEMBA 22, 2012 08:48 NA ELIZABETH MJATTA

KAMANDA wa Polisi, Mkoa wa Iringa, Michael Kamuhanda, ameibuka na kusema hawezi kujiuzulu kutokana na kifo cha aliyekuwa Mwandishi wa Habari wa Kituo cha Channel ten, Daud Mwangosi, aliyeuawa hivi karibuni mkoani Iringa.

Kamanda Kamuhanda alitoa msimamo huo jana alipokuwa akihojiwa na Kituo cha Radio cha Radio One wakati wa kipindi cha Kumepambazuka.

“Ninachofahamu mimi ni kwamba, kesi ya msingi iko mahakamani na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ameshaunda kamati ambayo inachunguza mwenendo mzima wa tukio hili na baadaye itatoa taarifa.

“Kwa hiyo, siwezi kujiuzulu kwa sababu tukio hilo la kifo lilitokea wakati wa kutimiza wajibu wa kutii sheria bila shuruti,” alisema Kamanda Kamuhanda.

Alipoulizwa kuhusiana na kuwajibika kutokana na mauaji hayo alisema, hawezi kuwajibika kwa sababu hana makosa.

“Niwajibike kwa kosa lipi?, kuna kosa mtu anaweza akawajibika, lakini kama huna kosa huwezi kuwajibika, haiwezekani watu waliofanya makosa wenyewe kwa kuandamana bila uhalali wasiwajibike halafu mimi niwajibike, haiwezekani.

“Sisi tunapokuwa kazini, tunalinda raia na mali zao na ndiyo tulilofanya na mara zote tunasisitiza utii wa sheria bila kushurutishwa.

“Kwa hiyo, hicho ndicho kilichokuwa kinafanyika, kilichofanyika ndiyo utii wa sheria bila shuruti, wangetii sheria bila shuruti yote yasingetokea,” alisema.

Septemba 2 mwaka huu, Mwangosi aliuawa kwa kupigwa na kitu kinachodhaniwa kuwa ni bomu alipokuwa kazini katika Kijiji cha Nyololo, Wilaya ya Mufindi, mkoani Iringa.

Baada ya kulipuliwa na kitu hicho, mwili wake ulisambaratika vipande vipande ingawa pia askari mmoja aliyekuwa jirani naye, pia alijeruhiwa mguu.

Baada ya tukio hilo, waandishi wa habari, wanaharakati na watu mbalimbali, walilaani tukio hilo na kutoa matamko yao wakitaka Kamanda Kamuhanda ajiuzulu, kutokana na mauaji hayo.

Septemba 12 mwaka huu, askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia mwenye namba G2573, Pasificus Simon, alipandikizwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mfawidhi Wilaya ya Iringa, kwa kosa mauaji ya marehemu Mwangosi.

Mtuhumiwa huyo alipofikishwa mahakamani hapo, hakutakiwa kujibu lolote kutokana na kosa linalomkabili haliwezi kusikilizwa katika mahakama hiyo. Hadi sasa mshitakiwa yuko mahabusu.


Kosa halihalishi kosa. Suluhisho la kosa la kuto kutii sheria kwa hiari si kuua. Na kama hicho kitendo cha kuua ni halali kwa nini huyu askari wa cheo cha chini kafikishwa mahakamani?
 
Majibu yake yamenistua sana.

Hakika sheria si mali kitu kwa the keeper.

askari with an empty big head... ooh pumpkin between his shoulders, eti anasema kama wagetii sheria bila shuruti hayo yote yasingetokea. sasa kesi mahakamani, na kamati sijui tume ni za nini, huyu kamanda bure kabisa. mjinga sana huyu mzee. wakati utamuhukumu.
 
Back
Top Bottom