hivi mbwa akikung´ata utamshitaki mbwa au mwenye mbwa? Hivi kosa ni la mbwa au mwenye mbwa kumuachia angáte wapita njia? Ukiona mbwa anangáta halafu mwenye mbwa hata hamzuii wala hashtuki jua mbwa kafunguliwa na huyo mwenye mbwa ili angáte! Kumaliza tatizo pressure lazima iwekwe kwa mwenye mbwa kwanza then mbwa ndio tutamaliza tatizo!unaweza kusoma kitu fulani hapa kama hayati nyerere alivyosema; "ukishaonja nyama ya mtu vigumu kuacha." mwisho wa nukuru. Nilipokuwa nasikia kauli hiyo sikujua nyerere alikuwa anamaanisha nini kwa vile nilikuwa bado mdogo sana.
Kamuhada ameua songea watu wanne mwaka huu, na kisha kuhamishiwa iringa ameanza kuvuta kiti chake cha u-rpc kwa kuua mwandishi wa habari mauaji ya kinyama yeye akishuhudia amebaki gari kando yake.
Leo anakuja kwa kujiamini na bila wasiwasi kwamba hawezi kujiuzuru alikuwa anatekeleza kazi yake.
Ukiona dalili za kuzeeka vibaya na kushia kustaafu kutokuwa na maisha ya raha na starehe huku ukiwazia tamu ulizozimwaga, basi ujue mambo kama hayo si ya umri wa sasa tunaouona, ila ni jambo alilolizoea na ndio maana anajiamini na hana wasiwasi kwa mauaji yake.
Kiongozi mwenye dhamiri ya kujali maisha ya binadamu angeona aibu na kusikitikia tukio lile linalolaaniwa na watanzania na dunia nzima na hata kuisababishia serikali kupata matatizo kwa wahisani kama umoja wa nchi za ulaya uliyvotolea kauli jana.
hivi mbwa akikung´ata utamshitaki mbwa au mwenye mbwa? Hivi kosa ni la mbwa au mwenye mbwa kumuachia angáte wapita njia? Ukiona mbwa anangáta halafu mwenye mbwa hata hamzuii wala hashtuki jua mbwa kafunguliwa na huyo mwenye mbwa ili angáte! Kumaliza tatizo pressure lazima iwekwe kwa mwenye mbwa kwanza then mbwa ndio tutamaliza tatizo!
Kwa hiyo, siwezi kujiuzulu kwa sababu tukio hilo la kifo lilitokea wakati wa kutimiza wajibu wa kutii sheria bila shuruti, alisema Kamanda Kamuhanda.
Alipoulizwa kuhusiana na kuwajibika kutokana na mauaji hayo alisema, hawezi kuwajibika kwa sababu hana makosa.
Niwajibike kwa kosa lipi?, kuna kosa mtu anaweza akawajibika, lakini kama huna kosa huwezi kuwajibika, haiwezekani watu waliofanya makosa wenyewe kwa kuandamana bila uhalali wasiwajibike halafu mimi niwajibike, haiwezekani.
Kwa hiyo, hicho ndicho kilichokuwa kinafanyika, kilichofanyika ndiyo utii wa sheria bila shuruti, wangetii sheria bila shuruti yote yasingetokea, alisema.
kwa nini waandishi wa habari huwa mnawaauliza hawa mnaowauliza maswali mwongozo? kwa nini usimuulize ni makosa gani ambayo yanapaswa mtu akawajibika kama alivyosema kuna makosa ya kuwajibika?
yaani mpaka hapo haoni kosa na hawezi kujiuzulu hata kama polisi wake wakiua maelfu machoni pake.
Hiyo ni jeuri ya kulindwa na ccm hasa waziri nchimbi.Hii inaonyesha wazi kuwa huu ni mpango ambao ulikuwa umepangwa.Huyu kamanda nasita na kuchela kusema ni mbumbu wa sheria.hata kama ni utii paipo shuruti, ni wapi katika hilo sheria inaruhusu kutoa uhai wa mtu kwa majibizano?na kama hata alikuwa hakutii sheria hivyo ilipasa polisi kumuua?na je yeye kama mwangosi ndo aliyetoa amri ya kuandamana bila kibali au alikuwa nachukua habari kwnye tukio hilo?je raia kufa mikononi mwa polisi bila ulizi wa maisha yake si kosa la kiutendaji katika taaluma ya kipolisi?huyu kamanda mbona anawatukana watanzania! na nani anamtumikia?kama aliapa kiapo cha kutumikia katiba , je haoni katiba iko wazi kutetea na kulinda maisha ya mwanadamu?hawa ndo makamanda amao kiapo chao hawakijui na pia hawajui wanamtumikia nani.kama ni watanzania wanasema umkosea vyema akasikiliza lakini kama natumikia watawala waliomtuma, ndo maana mjeuri na kiburi.