Kama yametokea Italy, na Greece, sisi tutanusurika?

The Hunter

JF-Expert Member
Dec 25, 2010
1,049
305
Wadau nimejikuta nafikiria hatma ya nchi yetu pendwa Tanzania, haswa kutokana na yanayojiri ulimwenguni leo, sijiiti mtabiri lakini nikiwa mmoja ninae amini katika uhalisia, naamini nchi yetu itakwama muda si mrefu kiuchumi, na tutarajie anguko kubwa sana hii ni kutokana na kuzidi kuporomoka kwa uchumi wa dunia, ambao umeshazikumba nchi za ulaya, leo kama Italy, na Greece zimefilisika vipi nchi yetu hii ambayo haijawahi kuwa tajiri! Taasisi za uchumi zinatabiri uwepo wa great depresion katika majira mafupi yajayo.

Shule hazitaendesheka, vyuo halikadhalika, mahospitali yetu yatakosa uwezo wa kuhudumia wagonjwa na hii nikutokana na kuyumba kwa uchumi.
Marekani na China zimeshatangaza misimamo yao ya kutokuisadia nchi yoyote ya ulaya itakayofilisika je wataweza kutusaidia sisi wa huku bara la tatu.
Kweli Serikali hii ya masharobaro isipoamua kutulia na kutafuta solution za kunusuru uchumi, janga litakalotokea itachukua milongo kurekebisha hali hii.
 
Kuna nchi za Ulaya tutazipa misaada sasa hivi maana watafilisika kuliko sisi tulivyo maskini....just wait and see
 
Mimi ninaifurahia hali hiyo kwa sababu hizi zifuatazo
1.Safari za kila kukicha za matanuzi ambazo husingizia kuwa wanaenda kuhemea vibaba/vibakuli zitaisha kwa kuwa sasa hakuna atakayetupa tena faranga na hawataweza kwenda tena majuu kufanya nini ?huwezi kwenda kuomba jamvi msibani
2.Wale waliokuwa wanatutishia kuwa hawatatupa msaada mpaka tuukubali USHOGA sasa itakuwa imekula kwao kwani hiyo misaada hawaezi kutoa tena kwetu kwani nao hali ni dhufli hali itabidi wakae na USHOGA wao.
3.Inatufundisha kuwa tutumie rasmali zetu wenyewe bila kutegemea wafadhili,kwetu sisi viongozi wetu wansingekuwa na wagumu kama ngozi ya kiboko wangebadilika kutokea hiyo hali ilivyoikumba Marekani huko nyuma,kwa rasmali tulizonazo sikuona sababu ya wakubwa kuhemea vibaba,na hivyo vibaba vinawanufaisha wao tu na si wananchi
 
Back
Top Bottom