Mkulima wa Kuku
JF-Expert Member
- Jan 13, 2011
- 1,270
- 533
Nimepata bahati ya kutembelea nchi kadhaa hapa ulimwenguni. Wenzetu wana shida zao kama sisi tulivyo na za kwetu. Kinachotofautisha wenzetu ambao tunasema wanashida na sisi ni kuwa hata kama wanalia kuna shida kuna mambo ya msingi hakuna anayeweza kuyachezea. Kwa mfano miundombinu katika ujumla wake. Ukifika kwenye mji kama Harare nimepata muda wa kuuzunguka kwa miaka mingi karibu wote. Sijaona Squatter area hata moja. Wabongo wenzangu wanaoifahamu Harare watakubaliana nami. Mpango mji ukiwekwa hakuna yeyote atakayeuvuruga kwa namna yoyote. Ukijenga kibanda ukasema unataka uongeze kwenye nyumba yako kesho asubuhi kinavunjwa kwa sababu ya mipango mji. nafasi za wazi zote ziko vilevile tangu mkoloni.
Mheshimiwa Mkulu wetu anakimbiliaga sana kwenda kusuluhisha migogoro ya wenzake kule nje, lakini ya kwake imemshinda...gogoro la umeya Arusha ameliachia na linazidi kukua huku kila siku mara Kenya, mara Somalia mara kule.
Ushauri wangu wa bure kwa JK ni kuwa kama nchi imemshinda awaachie wengine kuliko uharibifu huu tunaouona sasa hapa Bongo.
Nawasilisha.