Kama upo ARUSHA hii inakuhusu

Nadhani sasa hivi vibaka wa Arusha wataneemeka sana kipindi hiki.Sipati picha hapo Unga ltd na giza totoro jinsi panavyochimbika! Ngoja niwasiliane na Mganga mkuu wa Mt.Meru waongeze idadi ya nyuzi za kushonea majeraha maana vibaka wa Arusha bila kumwaga damu bado hawajakuibia.

Wakija kwangu usiku hawana bahati labda wanivizie njiani.
 
Sakina ndo targeted area,..na hasa kuanzia maeneo ya tecnical kuja huku juu,...nafikiri wanafanya makusudi ingawa sijui lengo ni nini hasa,hili tatizo halijaanza juzi ni muda kitambo kwa sisi tunaoishi huku maeneo ya technical.

Mkuu kila sehem kwa sasa sio sakina tuu maeneo mengi ni kuwa unakatika saa kumi na mbili au kumi na moja jioni unarudi kesho yake saa mbili au tatu asubuhi. hapo sijui ndo wanawaambia vibaka wakaibe
 
Nimetoka kuongea na Customer care Tanesco (kwa simu namba 0732 979280) kuhusu mgao mpya wa umeme cha kusikitisha jamaa anaongea huku akicheka kuwa sehemu kubwa ya Arusha haitakuwa na umeme kabisa mchana kwa majuma kadhaa..(sishangai kwani sakina kuanznia j'pili hatuna umeme) nilipomuuuliza mpaka lini akasema Mungu ndo anajua....sasa najiuliza hilo jibu maana yake ni nini wakati rais ni juzi ameingiza kampuni ya Kimarekani kuzalisha umeme....au ile kampuni ni kanyaboya wahusika wanaendelea na ishu nyingine? Jamani tutaishije tunaochomelea....wafugaji wa kuku...wauza samaki wabichi.....internet cafe......saloon sawmill mashine za kusaga.....hii mbona ni kama kukomoana?

Afadhali wewe uliambiwa Mungu anajua, mimi nilijibiwa karaha mpaka nikashangaa "customer care" unaqjibu rafu namna hiyo sijui tunaipeleka wapi nchi yetu wakati tunajiandaa kuingia kwenye shirikisho, wenzetu (Kenya, Uganda na Rwanda) ukifika au kupiga simu customer care utapokelewa/kujibiwa vizuri mpaka hata kama ulikuwa na hasira kwa ubovu/kukosekana huduma unapoa mwenyewe.

cha kushangaza zaidi wafanyakazi wa Tanesco badala ya kuliona hili ni janga si tu kwa watumiaji umeme bali pia ajira yao wao wanaona sawa tu. Hivi tutafika kweli, mimi nafikiri suluhisho ni 2015 kuitoa hii serikali madarakani na kuweka wenye uchungu na nchi yetu.
 
aisee ni kweli umeme arusha kuna ishu gani?
nimeongea na jamaa zangu uko wanasema umeme ni fulu kukatika
na hakuna tangazo wala nini!!ivi wanataka watu wawe majambazi?
je ni nini?mana usipotoa maelezo kila mtu atafikilia la kwake kichwani

wafanyakazi wa tanesco hasira zenu si kwa wanainchi,pelekeni kwa bosi wenu ngeleja na rais wenu
toeni amelezo kama ni libwawa limekauka au vipi!!
 
Nadhani sasa hivi vibaka wa Arusha wataneemeka sana kipindi hiki.Sipati picha hapo Unga ltd na giza totoro jinsi panavyochimbika! Ngoja niwasiliane na Mganga mkuu wa Mt.Meru waongeze idadi ya nyuzi za kushonea majeraha maana vibaka wa Arusha bila kumwaga damu bado hawajakuibia.

vibaka wa Arusha wakishakuibia ukisikia wanasema "mpe risiti."... ujue ni panga la kichwa.... yaani na hili giza..... hivi Moshi kwa mzee Ndesa....mabo ndo hivi hivi...coz hii sasa ni siasa full....
 
Mgao umekaa kisaniii kweli.... Majumbani - usiku kucha giza.... makazini - mchana hakuna umeme(kama huna generator kazi inalala) Mimi toka juzi sijui kama Tanesco wapo, maana nikitoka kazini kwenda nyumbani hakuna umeme, giza fullu , kombora nikiwahi kazini hakuna umeme !!! fullu matatizo!!!
 
Swala la umeme balaa kabisa............unaamka asubuhi umekatika unarudi usiku umelala.......tunaweza kuwa kwenye soko la pamoja kwa nchi iliyogizani namna hii
 
vibaka wa Arusha wakishakuibia ukisikia wanasema "mpe risiti."... ujue ni panga la kichwa.... yaani na hili giza..... hivi Moshi kwa mzee Ndesa....mabo ndo hivi hivi...coz hii sasa ni siasa full....

Mkuu hii ya kupewa risiti sijawahi isikia na kama ndivyo ilivyo basi hawa mijizi imezidisha ubunifu wa kishetwani sana. Usipotaka kupokea risiti inakuwaje sasa?
 
Na hapo vijana ajira zimeathirika, so tutegemee ujambazi kuongezeka...mbona hii nchi hatua mmoja mbele, hatua mbili nyuma...
 
wanasema kisa ni Arusha kuchagua Chadema.Tunakomolewa.

Waondoe kabisa nguzo na nyaya ila CC-Magamba kuongoza tena jimbo la Arusha itabaki Historia kama leo tunavyowaeleza watoto wetu habari za wakoloni.
 
Ndugu zanguni Leo nimeongea na marafiki zangu Wa Tanesco hapa Arusha hawajui tatizo la kukatika Umeme ni nini wanasema wanajaribu kuwauliza madingi zao hawasemi chochote hivo hili ni janga la wanaarusha hiyo Siri wanaijua madingi Wa Tanesco Arusha Giza kuu lisilojulikana mwisho ni lini na tatizo ni nini.
 
Mkuu hii ya kupewa risiti sijawahi isikia na kama ndivyo ilivyo basi hawa mijizi imezidisha ubunifu wa kishetwani sana. Usipotaka kupokea risiti inakuwaje sasa?

Ukatae kupokea risiti wakati wakishasema mpe risiti ni panga linashuka
kaka unataka kifo au hujipendi
 
Kuna miradi ya wakubwa imeingizwa A-town, kama petroli na ma jenereta, kwa hiyo wakisha rudisha hela zao (mukisha nunua vyakutosha), mtarudishiwa umeme....lol...
 
sasa nendeni mwanza ndo mtashaa,mgao everyday 12 hours na 2 days usiku gizani
na hakuna sijui viwanda sijui maofisi ya serikali makubwa!!ila mgao kama kawa

kweli ngeleja alishajifia na bosi wake!!tanesco wamejaa dharau ajabu
nafikiri ndicho wanasiasa wanachokifurahia kufarakanisha watu!!
 
Mgao umekaa kisaniii kweli.... Majumbani - usiku kucha giza.... makazini - mchana hakuna umeme(kama huna generator kazi inalala) Mimi toka juzi sijui kama Tanesco wapo, maana nikitoka kazini kwenda nyumbani hakuna umeme, giza fullu , kombora nikiwahi kazini hakuna umeme !!! fullu matatizo!!!

mkuu asante, umenifanya nicheke angalau nimeongeza siku zangu.... sasa mkuu hiyo generator mafuta yanashikika??? si utabaki kufanyia kazi wauza mafuta?
 
Back
Top Bottom