Kama ungekuwa wewe ungechukua uamuzi gani?

joel amani

Senior Member
Nov 22, 2011
100
8
mimi ni mtumishi wa umma na mke wangu nimeishi naye miaka 7 na tumezaa mapacha na wengine 2,mama watoto anatabia ya kutoka nje ya ndoa ni kama amelogwa,nikitaka kumuacha nashindwa mana anajituma sana katika kujishugulisha na kazi za nje mpaka ndani na anajua vizuri kutunza familia,kama mapenz nampatia vizuri sana na pesa ya matumizi nampatia,sasa nifanye nini? nimezungumza naye sana anachokitafuta nje lkn wapi,mke mzuri ni yule mwaminifu na anayejituma na kazi,ushauri wenu wana Great thinkers
 
Sasa hapo itakuwa anakupenda wewe au maisha anayoyapata kutoka kwako? Mpeleke katika Uongozi wa Kidini au Itisheni wazazi, ni jambo baya sana tena sana kutoka nje ya ndoa.
 
free advice, "RUN FOR YOUR LIFE KABLA HAUJA FUNGWA NEPI " - You may take it or leave it
 
Una uhakika mkuu kana unampa dose ya kutosha? Kama ni hivyo atakuwa ana pepo la ngono, pili utakuwa umepewa limbwata. Ikiwa hakuna uaminifu kwenye ndoa ni fullstop, hata kama kuna tabia nyingine nzuri bwana its invalidate everything. Wewe ulimwoa ili awe mwenza katika kujenga family, kama anajituma nje hiyo ni nyongeza lakini kama unakipato cha kawaida si vile umuhimu wake wa kufanya kazi.

Hata kama anajali watoto kwa sasa ni wadogo lakini wakipata fahamu hawataweka taswira nzuri zaidi anaweza kuharibu pia watoto kuwa tabia hii ni kawaida.

Ushauri wangu kaeni muyazunguze in bold na washiriki wazee na watu wa dini, ni bora kila mtu achukue zake, utaishia kufa bure watoto wakose baba na mama mapema.
 
duh, mke anapiga mechi za mchangani hadi unajua????

Hakuna kitu mwanamke hapendi mmewe ajue kama ana mabwana nje.

Hadi kukuonesha, aisee una kiranga, tena sio kidogo.
 
mimi ni mtumishi wa umma na mke wangu nimeishi naye miaka 7 na tumezaa mapacha na wengine 2,mama watoto anatabia ya kutoka nje ya ndoa ni kama amelogwa,nikitaka kumuacha nashindwa mana anajituma sana katika kujishugulisha na kazi za nje mpaka ndani na anajua vizuri kutunza familia,kama mapenz nampatia vizuri sana na pesa ya matumizi nampatia,sasa nifanye nini? nimezungumza naye sana anachokitafuta nje lkn wapi,mke mzuri ni yule mwaminifu na anayejituma na kazi,ushauri wenu wana Great thinkers

Kama uliyoyaandika hapo juu yote ni kweli, basi mkeo ni mhuni maana uhuni ni tabia tu kama zilivyo tabia zingine za uvutaji sigara, ugomvi, wizi nk. Cha hatari zaidi ni kuwa tabia ya uhuni yaweza kuwaletea magonjwa mkatoweka na kuwaacha watoto wenu yatima.

Ni muhimu sana kushirikisha ndugu, hasa wazazi, na viongozi wa dini ili waweze kumsaidia mkeo aachane na tabia hiyo then jaribu kumpa muda huku ukimchunguza kama tabia yake imebadilika, kama bado aisee hakuna namna ni bora kufanya maamuzi magumu kuliko kupoteza maisha kizembe na kuwaacha wanenu yatima ...

Pole mkuu!
 
Hakuna anayehusika zaidi ya wewe na yeye. mdadisi ujue ni kwa nini anatoka nje ya ndoa.
Kwanza ulijuaje kama anatoka nje ya ndoa?
Ulipolibaini hilo ulichukua hatua gani?
Yeye mwenyewe alionesha hali gani baada ya kugundua kuwa amejulikana kwa matendo yake machafu?

Ukijibu maswali hayo, ushauri uko nje nje.....
 
Una uhakika mkuu kana unampa dose ya kutosha? Kama ni hivyo atakuwa ana pepo la ngono, pili utakuwa umepewa limbwata. Ikiwa hakuna uaminifu kwenye ndoa ni fullstop, hata kama kuna tabia nyingine nzuri bwana its invalidate everything. Wewe ulimwoa ili awe mwenza katika kujenga family, kama anajituma nje hiyo ni nyongeza lakini kama unakipato cha kawaida si vile umuhimu wake wa kufanya kazi.

Hata kama anajali watoto kwa sasa ni wadogo lakini wakipata fahamu hawataweka taswira nzuri zaidi anaweza kuharibu pia watoto kuwa tabia hii ni kawaida.

Ushauri wangu kaeni muyazunguze in bold na washiriki wazee na watu wa dini, ni bora kila mtu achukue zake, utaishia kufa bure watoto wakose baba na mama mapema.
hivi kama hupati dozi la kutosha lazima uende nje?
 
Hongera kwa huo uvumilivu uliopitiliza..Naomba nikuulize swali moja tuu?? Je, upo tayari pia kuvumilia kuletewa magonjwa ya zinaa ukiwemo UKIMWI?? Dunia yako, chaguo lako...!
 
kwa hiyo unaogopa kumuacha kwa sababu kipato kitapungua? Basi ridhia akuketee ngoma,
 
Na kuonea huruma sana, yan una angalia jinsi unavyo hatarisha maisha yako!

Umejitetea kuwa una timiza majukumu yako, ni bora hiwe hivyo!

Lakini una hisi kwa nini anatoka nje ya ndoa?

Pole sana.
 
Du pole sana mkubwa ,huyo bi mkubwa utulivu ni sifuri kabisa.
Mi nakushauri urejee kwenye maandiko kwani nijuavyo mimi hakuna dini inayoruhusu zinaa.
jikaze kiume fanya maamuzi magumu before it's too late !!!
 
Tata kyala gwe! Jehanam inatisha! Soon you re' to sing in hell. Fukuza, fukuza, fukuza. Aende huko huko anakoona kunamfaa. Ukivumilia ukae kimya usije hata siku moja kutuomba ushauri, " Eti wana jf nina ngoma nataka ushauri" TUTAKUFUKUZIA MBALI UNASIKIA? Haya nenda kafukuze ulete majibu haraka
 
Back
Top Bottom