Kama unadaiwa na loans board angalia jina lako hapa

analysti

JF-Expert Member
Aug 24, 2009
729
612
Ndugu JF members, naona serikali imeamua kukaba kila kona. Na sasa, imeanza kufuatilia wanufaika wa mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu ambao bado hawajaanza kulipa madeni yao mpaka hivi leo. So kama unataka kujua status yako, fuatilia linki hii, kisha fungua ktk chuo ulichosoma, basi utaweza kufahamu status yako. GONGA HAPA Loan Defaulters/Wadaiwa
 
Jina langu nimeliona na wala sitalipa deni hilo kwani si deni kwangu bali ilikuwa ni haki yangu ya msingi kama walivyopata haki hiyo wale waliosoma tangu UDSM ianze. Pesa hiyo ilikuwa ni ya mlipa kodi, nami leo nalipa kodi, hivyo wanaosoma sasa hivi watumie kodi yangu na isiitwe mkopo kwao.

Taongea zaidi na kutoa strong evidence tukikutana mahakamani.
 
Hao jamaa kuna makosa wameyafanya, mimi mwenyewe nina zaidi ya miaka miwili toka nianze kulipa lakini cha ajabu nimeona jina langu na liko kwenye orodha ya watu ambao hawajaanza kulipa na kuna wengine wengi tu nawajua nao wameshaanza kulipa lakini cha ajabu majina yao yapo.
 
Ajira ziko wapi ili walipe mikopo yao?
Watalipa hao hao waliofanikiwa kupata hizo ajira,
watoto wetu bado wanaranda na njia tu.
 
Back
Top Bottom