Kama umezaliwa miaka ya 1970 na 1980...

Mkuu fikiria furaha unayoipata pale unapotengeneza manati yako, then unaingia mawindoni na unamtungua ndege unamkamata, au unatega mtego unakamata ndege wako.Ilikuwa raha sana, vijana wa sasa hata manati hawazijui!!!

Jamani jamani ntalia mie!!!!!!!!!
 
Those times, those wonderful times will never echo again. If you were not around, there are no words to describe those times,.., those wonderful times.

Sitaacha kukumbuka pilika pilika zetu majalalani kutafuta betri zilizotupwa, tukazipondaponda, kuzianika na kuziviringinga kwenye karatasi ngumu ilimradi jioni magari yetu tuliyojitengenezea kwa mabati, mbao na kandambili yawashe taa kama Simba Luwala na The Blog Mayai.

Ni nyakati zile tulicheza kombolela na kidari tukifukuzana mitaani bila viatu. Lakini we were very happy. Shuleni tulikula mihogo na sun vita na si soda kwa chips kama leo. The last generation to listen stories from grandpas and grandmas.

Naona wengine wana criticize those happy memories, as we could not be quite seeing those white birds crossing our horizons without helping us to make our fingernails white...so many to say about those days....the days that will never come back again.

Kwenye nyekundu umenikumbusha mbali sana mkuu "nyange nyange nipe kucha nyeupe" ...lol
 
Wakuu mmenikumbusha mbali. Enzi hizo ndala zilizokwisha tumika ni mali mno, makopo ya mafuta (cowboy, kcc) zilikuwa dili kwa kutengeneza mabasi, kila kijani mtaani alikuwa na manati yake. Shuleni ukifika darasa la tatu unapewa bustani ya mbogamboga na maua uitunze mpaka utakapofika darasa la saba. Kulikuwa hakuna simu, mpenzi akikuandikia barau kanyunyiza poda na stika kibao basi ukiipata usiku hulali utaamka mara kadhaa utawasha kibatari na kuisoma. Maisha yalikuwa kiasili zaidi
 
Nakumbuka tulivyotumia Tubes za bicycle tyres kutengeneza magozi, tulivizia na kudandia gari la mataka kutoka Kiwanda cha BORA na reject tubes tulikusanya na kutengeneza Mipira.
 
Back
Top Bottom