Kama umeguswa saidia watoto hawa

TIQO

JF-Expert Member
Jan 8, 2011
13,787
2,078
Na Mwandishi wetu
KATIKA gazeti la Uwazi, toleo la wiki iliyopita tulitoa habari za mtoto Mustafa Ally, 12, (pichani), mkazi wa Mtoni Mtongani, Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam anayewauguza wadogo zake mapacha wenye umri wa miezi nane.
Mtoto Mustafa ambaye ni mwanafunzi wa darasa la sita katika Shule ya Msingi Twiga, Temeke amelazimika kuwauguza wadogo zake hao, Swaumu na Ramadhani kwa kuwa baba yao alishafariki na mama yao yupo mahututi.
Watoto hao mapacha wanaumwa na wamelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu. Mama yao aliyekuwa akiwauguza aliugua ghafla na kupewa matibabu na kwa sasa yupo hoi nyumbani kwake, hivyo Mustafa kuchukua mzigo huo wa kuwauguza.
Matatizo yanayoikabili familia hiyo ni pamoja na ukosefu wa chakula, nguo za kawaida na za shule, fedha za matumizi, maziwa ya unga ya watoto na kodi ya nyumba.
Gazeti hili kwa niaba ya familia hiyo linatoa shukrani kwa watu mbalimbali waliompatia msaada wa maziwa, sabuni, sukari, nguo na fedha, vyote vikiwa na thamani ya shilingi 300,000.
Bado msaada unakaribishwa kwa watoto hawa. Aliyeguswa na kilio cha mtoto Mustafa afanye mawasiliano na Afisa Ustawi wa Jamii Muhimbili, Erika Ishengoma kwa simu 0714 220 038 au mwandishi wetu kwa namba 0713 454 656 au afike Muhimbili wodi ya watoto, Makuti B atakutana nao ana kwa ana.



Mtoto Mustafa ambaye ni mwanafunzi wa darasa la sita katika Shule ya Msingi Twiga, Temeke amelazimika kuwauguza wadogo zake hao, Swaumu na Ramadhani kwa kuwa baba yao alishafariki na mama yao yupo mahututi.

Source: Global Publishers
 

Attachments

  • mtotonawadogozakemuhimbili.jpg
    mtotonawadogozakemuhimbili.jpg
    37.3 KB · Views: 21
Jamani akina baba, mama, dada, kaka tuwekeni kando lawama na sihasa tuwasaidie hawa watoto ili waokoe maisha yao na wao waishi kama sisi wengine tunavyo ishi.
 
Mungu atawasaida, mimi niko mbali tu lakini ningepita kuwasaidia.
 
Too bad!
Really paining!

Mkuu fanya kama yule member aliye fiwa na mkewe. Kutoa ni moyo chochote ulicho nacho
Fikiria dogo huyo wa darasa la sita ndo anauguza hao watoto mapacha mama ake yupo mahututi nae.
 
Mungu atawasaida, mimi niko mbali tu lakini ningepita kuwasaidia.

Penye nia, Njia haikosekani mkuu!! Hata mimi niko mbali tena sana tu kutoka kwetu!! Lakini No doubt wengi wetu tunaoishi mbali na nyumbani huwa tunafanya mengi tu bila sisi wenyewe kuwepo. kwani kuna watu huwa wantuwakilisha. Piga moyo konde kakaa!
 
Back
Top Bottom