Mlalahoi
JF-Expert Member
- Aug 31, 2006
- 2,182
- 883
Let's call a spade a spade.Mjengwa hana tofauti na Michuzi.Hawa ni wakereketwa wa Kikwete.Mjengwa aliwahi kuandika makala moja ya ajabu sana huko Raia Mwema akitetea safari za Kikwete.Na juzijuzi tu eti kamsifia Kikwete kwa "moto alioanzisha ndani ya CCM kudhibiti uchakachuaji"
Aliandika (namnukuu)
Kuhusu safari za Kikwete,Mjengwa aliandika (namnukuu tena)
Mjengwa anadai hapa (namnukuu)
In same manner,unatetea utalii wa Kikwete huko nje ya nchi na kutoa mifano dhaifu ya kampeni za malaria na kuanzishwa kwa safari za ndege za Turkey,lakini kwa makusudi unakwepa kubainisha kuwa kazi hizo zingeweza kabisa kufanywa na mabalozi wetu,kama sio waziri wa mambo ya nje.Kwani trade centres zetu zinafanya kazi gani?
Haihitaji hata short course ya uandishi wa habari kutambua msimamo wako pale Raia Mwema.Kamwe hujawahi kumlaumu Kikwete hata iweje.Na japo utajitetea kuwa huo ni mtazamo wako na kutukumbusha uhuru wa kutoa mawazo yako binafsi,wasomaji wako pia tungependa kukukumbusha kuwa mawazo mufilisi yana-deserve kukabiliwa haraka iwezekanavyo kwa vile yakiachwa yanaweza kujenga kupata status ya kuwa facts.
Hebu tuonyeshe hapa where we dare to speak openly ni lini uliwahi kuandika chochote kinachomkosoa Kikwete?
Utafiti wako wa kijiweni kuhusu matokeo ya uchaguzi wa mwaka huu hauna tofauti na vitisho vya majini ya Sheikh Yahya.Or is it majini yanayomlinda Kikwete yamevamia JF?
Aliandika (namnukuu)
"Kama wengine, nimekuwa nikifuatilia kinachoendelea katika nchini sasa. Ninachoandika hapa ni fikra zangu huru katika kujaribu kuchambua kile ninachokiona. Naam. Mambo hayaendi kama yanavyotakiwa yaende kutokana na mazoea. Rais na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi, Jakaya Kikwete amewasha moto ndani ya chama chake.
Kwa ninayeangalia kutoka nje nakiona kivuli katika moto aliouwasha Kikwete. Ndiyo, hata moto una kivuli chake. Yawezekana kabisa, kuwa huu ukawa ni mwanzo wa mwisho wa tufani iliyowakumba Watanzania wengi kwa muda mrefu. Kila baya jema, walitwambia wahenga.
Watanzania tuna kitu tunahisi tumekipoteza. Huenda watakaonielewa zaidi ni Watanzania wa kizazi changu; kizazi cha Azimio. Tumezaliwa na kukulia katika kipindi kinachotufanya tujisikie tuna kitu tumekipoteza katika wakati wetu huu. Si kingine, bali ni kile ambacho Wafaransa wangeweza kukiita "L'esprit Mwalimu" – Ari ya Mwalimu.
Nataka niamini, kuwa anachokifanya Rais Kikwete, hususan, ndani ya CCM, ni kurudisha misingi ya Chama Cha Mapinduzi na hivyo basi, "Ari ya Mwalimu".
Inahusu kujenga misingi ya usawa na haki katika jamii"
Kuhusu safari za Kikwete,Mjengwa aliandika (namnukuu tena)
"Na wengi waliojaribu kuonyesha upande ulio chanya juu ya safari hizo wamekuwa wakiandamwa. Kuna wakati ni lazima tuelezane ukweli. Hata kama Rais aliye madarakani ana kasoro zake ambazo tumekuwa tukiziainisha, lakini bado ana mambo ambayo amefanikiwa sana katika uongozi wake.
Mojawapo ni namna alivyofanikiwa, kupitia ziara zake za kikazi za nje ya nchi, kujenga ushawishi kwa asasi za kiserikali na zisizo za kiserikali za nchi alizotembelea. Amefanikiwa kuzifanya nchi na asasi hizo kuisikiliza Tanzania kama mshirika wake wa kimaendeleo.
Kuna mifano mingi hai ya mafanikio ya ziara za Rais Kikwete nje ya nchi; mradi wa kutokomeza Malaria nchini ambapo Rais mwenyewe, sio tu amesaidia kuwajengea imani wanaotusaidia, bali yuko mstari wa mbele katika kuongoza mapambano hayo.
Juzi hapa Shirika la Ndege la Uturuki limeanzisha safari za ndege kuja Tanzania. Ni kufuatia ziara ya Rais Kikwete aliyoifanya Uturuki miezi kadhaa iliyopita. Rais amesaidia kuwajengea imani kwetu Waturuki, kuwafanya wafahamu zaidi umuhimu wa kuwa na ushirikiano nasi.
Lakini hilo la ndege ya Uturuki kutua Dar es Salaam halina maana ya Waturuki na watu wa mataifa mengine kuja kufanya utalii na biashara nchini mwetu tu. Limetatua pia kero ya muda mrefu ya mahujaji wa Kitanzania kusafiri kwenda kuhiji Mecca.
Ni fursa pia kwa Watanzania kuutumia usafiri huo wa gharama nafuu katika kufanya biashara na Uturuki, na nchi nyingine za Mashariki ya Kati, Ulaya na Marekani.
Hapo juu ni mifano miwili tu kati ya mingi ya mafanikio yatokanayo na ziara za Rais Jakaya Kikwete nje ya nchi. Ukiwa ni mtu wa hulka ya kubeza tu, mwishowe nawe utabezwa! Hilo la mwisho ni la hasara zaidi kwa anayebezwa na jamii kwa ujumla."
Mjengwa anadai hapa (namnukuu)
.Hivi hizo makala mbili tu hapo si uthibitisho tosha kuwa wewe ni mnazi sugu wa Kikwete?Unapozungumzia "moto aliowasha ndani ya CCM" na kumlinganisha na Baba wa Taifa (huko aliko anatetemeka kwa tusi hilo) halafu kwa makusudi unakwepa kuzungumzia upande wa pili wa shilingi-yaani huwezi kuzungumzia failures za CCM pasipo kumhusisha Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho-inaleta tafsiri gani kama sio unazi.....Na kama utaweka hapa ukumbini makala ya nyuma yenye kufanana na hiyo niliyoandika, basi, nitaacha kabisa kuandika na nitajitoa uwanachama wa JF....