Jumapili, Septemba 12, 2010.
Na Maggid Mjengwa,
HUU ni mjadala niliouanzisha kule kwenye jukwaa la Jamii (www.jamiiforums.com). Nauendeleza hapa ili uwafikie wengi zaidi.
Ni tathimini yangu. Ni mtazamo wangu huru. Katika kuishi kwangu kuna chaguzi nilizozishuhudia kwa macho na nilizosoma vitabuni. Hivyo, ninachoandika kinatokana na uzoefu wangu wa kufuatilia kwa karibu mienendo ya chaguzi zetu.
Naam. Zikiwa zimebaki siku 45( Leo Jumatano, Septemba 15, 2010) naiona hali ifuatayo kama uchaguzi ungefanyika hii leo;
Mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi, Jakaya Mrisho Kikwete angeibuka mshindi . Dk Wilbroad Slaa ( CHADEMA) angechukua nafasi ya pili na huku Profesa Ibrahim Lipumba ( CUF) akishika nafasi ya tatu. Wagombea wa vyama vilivyobaki wangekuwa wasindikizaji kwa kupata chini ya asilimia 5 ya kura zote kwa pamoja.
Hali hiyo ingeakisi pia matokeo ya uchaguzi wa wabunge na madiwani ( Bara). Tafsiri yake; Jakaya Mrisho Kikwete angeunda Serikali huku yeye na chama chake wakikabiliwa na changamoto kubwa kutokana na upinzani utakaokuwa umeongezeka nguvu ndani na nje ya bunge kutokana na ujio wa Dk Slaa kama mgombea Urais katika uchaguzi wa mwaka huu.
Ni dhahiri kuwa Chama Cha Mapinduzi baada ya Oktoba 31, kinatakiwa kijipange upya kuikabili hali mpya katika uwanja wa kisiasa. Viashiria vya jamii inayotaka mabadiliko vimeshaonekana. CCM itakuwa na mawili ya kuchagua; kuchukua jukumu la kuyaongoza mabadiliko hayo au kusubiri kuzamishwa na mkondo wa maji ya mabadiliko hayo.
CCM ianze sasa kufikiria namna itakavyounda Serikali miaka ijayo kwa kushirikiana na vyama vingine. Ifikirie pia uwezekano wa kuwapo Serikali ya Mseto hata Tanzania bara. Ndio, kutoa fursa kwa chama au vyama pinzani vitakavyokuwa na idadi kubwa ya wabunge kushiriki kuunda serikali ya Umoja wa Kitaifa.
Na hakika miaka mitano mpaka kumi ijayo, tutakuwa na Tanzania tofauti na ya sasa. Na mtaziona ishara. Kauli za ' Kidumu Chama Cha Mapinduzi! Na CCM Daima! Zitaonekana na wapiga kura kuwa ni za waliopitwa na wakati. Hiki ni kizazi kipya na dunia imebadilika.
Kwa hali ilivyo kwa sasa, CCM wanajivunia:
Kuwa ni chama kikongwe, kikubwa na kilichotawala kwa muda mrefu. Kuna hata wanaokipigia kura chama hicho ' Kwa mazoea tu'. Na katika nchi zetu hizi; kukiondoa chama kilicho madarakani, Chama kilichopigania uhuru au kinachotokana na chama kilichopigania uhuru ni kazi ngumu sana. Kwa anayetaka kufanikiwa katika hilo, anahitaji kwenda ilipo mizizi ya chama hicho. Ni vijijini. Na huko vijijini kwa leo hii chama wanachokijua ni CCM. Naam. Ndio ' Zimwi' wanalolijua.
Mwanakijiji atatembea kwa miguu kilomita kumi kwenda kuhudhuria mkutano wa CCM. Atakwambia amepewa taarifa ya mkutano na Balozi wake wa Nyumba Kumi. Hivyo basi, CCM wanajivunia mtandao wao wa kichama kuanzia ngazi ya Balozi wa Nyumba Kumi, shina, tawi na kuendelea. Na hata mtandao wa Kiserikali.
Na hakika, mara zote ni vema na ni busara kusema yaliyo kweli na tunayoyaamini, hata kama ukweli mwingine unahuzunisha, ni vema ukasemwa. Kuufumbia macho ni sawa na kuogelea kwenye mapovu wakati maji yapo.
Udhaifu wa CCM:
Pamoja na kuwa ni chama kikongwe na chenye uzoefu, wakati mwingine inashangaza kuona katika maeneo kadhaa kinavyoshindwa kusoma alama za nyakati. Kura za maoni ni mfano wa udhaifu wa CCM kushindwa kubaini kuwa kwa utaratibu mpya ulijiojiwekea katika kupata wagombea walisahau umuhimu wa kuyapitia na kuyachuja majina ya wanachama wake waliotangaza nia ya kugombea na kuchukua fomu kabla ya kuyapeleka kwa wanachama wake kupigiwa kura za maoni.
Badala yake, CCM iliacha wanachama waamue halafu bado chama nacho kikaingilia kati kuamua tena. Kuna adhabu ya chama kutoka kwa wanachama wake inakuja kutoka katika baadhi ya majimbo. Kwa utaratibu uliotumika sasa, wanachama wa CCM huko tuendako wanaweza kujikuta wakiwapigia kura za maoni wagombea wenye fedha chafu zinazotokana na shughuli haramu. Na kinachojitokeza zaidi sasa ni kubadilika kwa mwenendo wa wapiga kura. Kidogo kidogo wapiga kura wameanza kuangalia zaidi watu na si chama. Ni kwenye ngazi ya udiwani na ubunge. Hizi ni dalili mpya za kubadilika kwa mwenendo wa wapiga kura. Kwamba mtu kwanza, ilani ya chama baadae.
CHADEMA: Ujio wa Dk Slaa:
Sio tu umewashangaza CCM na mgombea wake urais, bali pia unaonekana kuwashangaza CHADEMA wenyewe wanaoonekana kutokujiandaa na namna Dk Slaa alivyopokewa na wananchi. Na kama ilivyotabiriwa na Mwalimu, CHADEMA inaonekana kuwa ndio chama cha upinzani chenye nguvu na chenye nafasi ya kuipoka CCM mamlaka ya kuongoza dola endapo CCM kama chama haitafanya juhudi za makusudi za kufanya mabadiliko ya kimsingi yatakayoonekana na wapiga kura.
Udhaifu wa CHADEMA
Unajidhihirisha kwenye eneo la oganaizesheni na kifedha. Bado CHADEMA haina uwakilishi mpana katika ngazi za mashina na matawi. Dk Slaa anaweza kutua na helikopta Pawaga, Iringa. Lakini, mara ile akiruka, huku nyuma hakuna watendaji wa CHADEMA wa kufanya kazi ya CHADEMA. Kuna taarifa pia za wagombea wake ubunge na udiwani wa CHADEMA kukosa nguvu za kifedha kuendesha kampeni . Taarifa hizo zilizoripotiwa kwenye vyombo vya habari haziwezi kupuuzwa tu. Hapa inahusu udhaifu katika maandalizi. Kuna wagombea wa CHADEMA watakaoanguka katika chaguzi kwa tatizo hilo.
Zitto Kabwe:
Huyu ni kada nyota ndani ya CHADEMA. Hata hivyo, ‘sarakasi' zake za kisiasa huenda zinachangia kukidhohofisha chama chake kuliko kukipa nguvu. Majuzi hapa aliripotiwa na magazeti kutamka hadharani kuwa anajiandaa kugombea urais 2015. Zitto Kabwe anaacha maswali; Kulikoni ndani ya CHADEMA? Je, Dk Slaa ni mgombea wa ‘msimu' tu? Au ndio sababu Zitto Kabwe hakuhudhuria Mkutano wa ufunguzi wa kampeni za CHADEMA pale viwanja vya Jangwani?
Inachojivunia CHADEMA:
Bado ni chama kinachoonyesha kuwa na mvuto kama kitajipanga vema. Kesi iliyofunguliwa Mahakamani dhidi ya Dk Slaa kuhusiana na masuala binafsi ya mahusiano inaonyesha kumtangaza na kujenga zaidi Dk Slaa kwa wapiga kura wanaotia shaka wakati uliotumiwa kuibuliwa kwa suala hilo. Kuna watakaompigia Dk Slaa ' Kura za Kumhurumia'.
Umakini wa CHADEMA:
CHADEMA imekuwa ikijinadi kama chama makini machoni mwa wapiga kura. Hata hivyo, taarifa zilizoripotiwa kuwa Naibu Katibu Mkuu , CHADEMA, Zanzibar Hamad Yussuf huenda akaondolewa kwenye timu ya kampeni ya Dk Slaa kwa kuwa amekuwa kero inaonyesha namna timu ya kampeni ya CHADEMA ilivyoshindwa kubaini mapema, Hamad Yussuf alikuwa kero kwa wapiga kura. Maana, kwa utamaduni wa Watanzania, namna Naibu yule Katibu Mkuu alivyokuwa akimfananisha Dk Slaa na Bwana harusi na kauli nyingine pale viwanja vya Jangwani ilikuwa ni ' matusi' hata kama kuna waliotaka kupewa tafsiri sahihi ya neno hilo. Ni heri kwa CHADEMA wameamka na kubaini kero hiyo ndani ya nyumba yao.
Kauli na Ishara:
Kama hakuna aliyelifikiria hili ndani ya CHADEMA, basi, hata kama CCM wanaimba ' Wapinzani tuwalete , tuwakatekate' , hilo ni kosa ambalo halipaswi kujibiwa na kufanya kosa lingine, Ni pale viongozi wa CHADEMA wanapotamka maneno ya Kiingereza; " People's…. Power! Huku wakiamrisha wafuasi wao kusokota ngumi . Kitendo hicho kinatoa ishara mbaya kwa mpiga kura wa kawaida. Bado kuna Watanzania wengi waliopokea maelekezo ya tangu enzi za Mwalimu kuwa; "Tujiadhari na wanaotaka kutusababishia vita na mapigano katika nchi." Kukunja ngumi ni ishara ya kujiandaa kupigana. Kuna kura zinazokimbia kutoka CHADEMA kwa ngumi hizo.
CUF: Chama cha Wananchi
Katika hali ya kushangaza, CUF ( Bara) safari hii kinaonekana zaidi kuwa ' jokeli' katika karata za kisiasa. Profesa Ibrahim Lipumba bado anaonekana kuwa na nguvu katika kanda ya Pwani na mikoa ya kusini. Lakini, nguvu hizo haziwezi kulinganishwa na za katika uchaguzi mkuu uliopita. Profesa Lipumba aliyeanza kuwania Urais tangu 1995 sasa anaonekana zaidi kuwa ni mtu anayepita ' kuwaaga' Watanzania kuliko kuomba kura zao.
Na kuna wakati, CUF wanaonekana kama ' Chama Rafiki' na CCM kuliko chama cha upinzani. Na laiti ' urafiki' huo wa kisiasa ungekuwa kati ya Profesa Lipumba na Dk Slaa, basi, mgombea Urais wa CCM angekuwa na kibarua kigumu zaidi, lakini si kwa sasa, siku 45 kabla ya Oktoba 31. Ninapoandika fikra hizi huru. Urafiki huo wa CCM na CUF unaweza pia kumgharimu mgombea wa CCM, Rais Kikwete na kujikuta akigawana kura na Profesa Lipumba na si kura za upinzani kugawanywa. Hilo linaweza kutokea na kuwashitua CCM.
CHANZO: Raia Mwema
========================================================

NAANDIKA haya kutokana na uzoefu wangu wa kufuatilia kwa karibu mienendo ya chaguzi zetu. Kwa chaguzi nilizozishuhudia kwa macho na nilizosoma vitabuni. Naam. Zikiwa zimebaki siku 48 ( Leo Jumapili, Septemba 12, 2010) naiona hali ifuatayo kama uchaguzi ungefanyika leo hii;
Mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi, Jakaya Mrisho Kikwete angeibuka mshindi . Dr Wilbroad Slaa ( CHADEMA) angechukua nafasi ya pili na huku Profesa Ibrahim Lipumba ( CUF) akishika nafasi ya tatu. Wagombea wa vyama vilivyobaki wangekuwa wasindikizaji kwa kupata chini ya asilimia 5 ya kura zote kwa pamoja.
Hali hiyo ingeakisi pia matokeo ya uchaguzi wa wabunge na madiwani ( Bara). Tafsiri yake; Jakaya Mrisho Kikwete angeunda Serikali huku yeye na chama chake wakikabiliwa na changamoto kubwa kutokana na upinzani utakaokuwa umeongezeka nguvu ndani na nje ya bunge kutokana na ujio wa Dr Slaa kama mgombea Urais katika uchaguzi wa mwaka huu.
CCM wanajivunia:
Kuwa ni chama kikongwe, kikubwa na kilichotawala kwa muda mrefu. Kuna hata wanaokipigia kura chama hicho ' Kwa mazoea tu'. Na katika nchi zetu hizi; kukiondoa chama kilicho madarakani, Chama kilichopigania uhuru au kinachotokana na chama kilichopigania uhuru ni kazi ngumu sana. Kwa anayetaka kufanikiwa katika hilo, anahitaji kwenda ilipo mizizi ya chama hicho. Ni vijijini. Na huko vijijini kwa leo hii chama wanachokijua ni CCM. Naam. Ndio ' Zimwi' wanalolijua. Mwanakijiji atatembea kwa miguu kilomita kumi kwenda kuhudhuria mkutano wa CCM. Atakwambia amepewa taarifa ya mkutano na Mjumbe wake wa nyumba kumi. Hivyo basi, CCM wanajivunia mtandao wao wa kichama kuanzia ngazi ya Balozi wa Nyumba Kumi, shina, tawi na kuendelea. Na tayari CCM ina wabunge kumi waliopita bila kupingwa na madiwani zaidi ya 100 kwa mujibu wa gazeti la NIPASHE la leo Jumapili.
Udhaifu wa CCM:
Pamoja na kuwa ni chama kikongwe na chenye uzoefu, wakati mwingine inashangaza kuona katika maeneo kadhaa kinavyoshindwa kusoma alama za nyakati. Kura za maoni ni mfano wa udhaifu wa CCM kushindwa kubaini kuwa kwa utaratibu mpya ulijiojiwekea katika kupata wagombea walisahau umuhimu wa kuchuja majina ya wagombea kwanza ili kubaini wale ambao wangewaletea shida. Badala yake, waliacha wanachama waamue halafu bado chama nacho kikaingilia kati kuamua tena. Kuna adhabu ya chama kutoka kwa wanachama wake inakuja kutoka katika baadhi ya majimbo. Na kinachojitokeza zaidi sasa ni kubadilika kwa mwenendo wa wapiga kura. Kidogo kidogo wameanza kuangalia zaidi watu na si chama kwenye ngazi ya udiwani na ubunge. Hizi ni dalili mpya.
CHADEMA:
Ujio wa Dr Slaa:
Sio tu umewashangaza CCM na mgombea wake urais, bali pia unaonekana kuwashangaza CHADEMA wenyewe wanaoonekana kutokujiandaa na namna Dr Slaa alivyopokewa na wananchi.
Udhaifu wa CHADEMA
Unajidhihiri kwenye eneo la oganaizesheni na kifedha. Bado CHADEMA haina uwakilishi mpana katika ngazi za mashina na matawi. Dr Slaa anaweza kutua na helikopta Pawaga Iringa, lakini mara ile akiruka, huku nyuma hakuna watendaji wa CHADEMA wa kufanya kazi ya CHADEMA. Kuna taarifa pia za wagombea wake ubunge na udiwani kukosa nguvu za kifedha kuendesha kampeni . Taarifa hizo zilizoripotiwa kwenye vyombo vya habari haziwezi kupuuzwa tu. Hapa inahusu udhaifu katika maandalizi. Kuna wagombea wa CHADEMA watakaoanguka katika chaguzi kwa tatizo hilo.
Zitto Kabwe,
Ni kada nyota ndani ya CHADEMA lakini ‘sarakasi' zake za kisiasa huenda zinachangia kukidhohofisha chama chake kuliko kukipa nguvu. Majuzi hapa aliripotiwa na magazeti kutamka hadharani kuwa anajiandaa kugombea urais 2015. Zitto Kabwe anaacha maswali; Kulikoni ndani ya CHADEMA? Je, Dr Slaa ni mgombea wa ‘msimu' tu? Au ndio sababu Zitto Kabwe hakuhudhuria Mkutano wa ufunguzi wa kampeni za CHADEMA? Kuna watakaouliza.
Inachojivunia CHADEMA:
Bado ni chama kinachoonyesha kuwa na mvuto kama kitajipanga vema. Kesi iliyofunguliwa Mahakamani dhidi ya Dr Slaa kuhusiana na masuala binafsi ya mahusiano inaonyesha kumtangaza zaidi Dr Slaa kwa wapiga kura wanaotia shaka wakati uliotumiwa kuibuliwa kwa suala hilo. Kuna watakaompigia Dr Slaa ' Kura za Kumhurumia'.
Umakini Wa CHADEMA:
CHADEMA imekuwa ikijinadi kama chama makini machoni mwa wapiga kura. Hata hivyo, taarifa zilizochapwa leo ( MWANANCHI) kuwa Naibu Katibu Mkuu , CHADEMA, Zanzibar huenda akaondolewa kwenye timu ya kampeni ya Dr Slaa kwa kuwa amekuwa kero inaonyesha namna timu ya kampeni ya CHADEMA ilivyoshindwa kubaini mapema kuwa Naibu huyo alikuwa kero kwa wapiga kura. Maana, kwa utamaduni wa Watanzania namna Naibu yule Katibu Mkuu alivyokuwa akimfananisha Dr Slaa na Bwana harusi na kauli nyingine pale viwanja vya Jangwani ilikuwa ni ' matusi' hata kama kuna waliotaka kupewa tafsiri sahihi ya neno hilo. Ni heri kwa CHADEMA wameamka na kubaini kero hiyo ndani ya nyumba yao.
Kauli na Ishara:
Kama hakuna aliyelifikiria hili ndani ya CHADEMA, basi, hata kama CCM wanaimba ' Wapinzani tuwalete , tuwakatekate' , hilo ni kosa ambalo halipaswi kujibiwa na kufanya kosa lingiine, Ni pale viongozi wa CHADEMA wanapotamka maneno ya kiingereza; " People's…. Power! Huku wakiamrisha wafuasi wao kusokota ngumi . Kitendo hicho kinatoa ishara mbaya kwa mpiga kura wa kawaida. Bado kuna Watanzania wengi waliopokea maelekezo ya tangu enzi za Mwalimu kuwa; " Tujiadhari na wanaotaka kutusababishia vita na mapigano katika nchi." Kukunja ngumi ni ishara ya kujiandaa kupigana. Kuna kura zinazokimbia kutoka CHADEMA kwa ngumi hizo.
CUF: CHAMA CHA WANANCHI
Katika hali ya kushangaza, CUF ( Bara) safari hii kinaonekana zaidi kuwa ' jokeli' katika karata za kisiasa. Profesa Ibrahim Lipumba bado anaonekana kuwa na nguvu katika kanda ya pwani na mikoa ya kusini. Lakini nguvu hizo haziwezi kulinganishwa na za katika uchaguzi mkuu uliopita. Kuna wakati, CUF wanaonekana kuwa zaidi ' Chama Rafiki' na CCM kuliko chama cha upinzani. Na laiti ' urafiki' huo wa kisiasa ungekuwa kati ya Profesa Lipumba na Dr Slaa, basi, mgombea Urais wa CCM angekuwa na kibarua kigumu zaidi, lakini si kwa sasa, siku 48 kabla ya Oktoba 31. Ninapoandika fikra hizi huru.
Maggid
Iringa