Kama Slaa, Migiro, Salim, Lowassa, Shein hawafai kuwa Rais; nani atatufaa 2015?

mharakati usimpige bit Motown maana anayo haki kujua nani anaweza kuwa kiongozi wake na impact ya uongozi wake kwa maisha yake.Kama anaona hao wanamtandao hawana ni sifa za kuwa Maboss wake 2015 ni hake yake kusema na kuhakikisha kweli hawawezi kuwa viongozi wa Taifa ili.We cant let things go to dogs as it happened in 2005 and 2010.


marais wote kuanzia sasa watatoka kwenye mitandano yao..hata huko upinzani kutakua na kamtandao nyuma ya kila mgombea na watasuluhisha matatizo kwa muda wakati wa uchaguzi na kuendelea tena na mitandao yao wakishinda au zaidi na wazi wazi wakishindwa. Lowassa na Rostam wametuingiza kwenye siasa hizi na Mkapa alizibariki basi tena hatuna jinsi
 
Wana jf nisaidieni hili la Dk. Slaa na Lowasa hivi nani anaweza kuwa raisi 2015 ikitokea wamepewa nafasi za kugombea kwa vyama vyao kwenye uraisi kwa sababu nilikuwa Arusha juzi nikawa niko kwenye hotel moja mjini arusha nikakuta mjadala mkubwa sana juu ya hawa watu wawili kugombea uraisi,

kuna mmoja huyo aliyekuwa ana msifia sana lowasa kuwa ni muadilifu na hana kashfa yeyote na ndipo mmoja wapo akatokea akazungumzia swala na richmond huyu aliyekuwa ana mtetea lowasa akamtaka atoe ushahidi juu ya hilo na wengine wakawa wanasema ccm itashinda uraisi kwa sababu lowasa ana kubalika lakini wabunge wengi watatoka chadema.

Na wengine wakampigania sana dk slaa kuwa atakuwa raisi wa nchi hii kwa sababu ni mwaadilifu sana na mchapa kazi na kwa hatua nchi ilipofikia awana mbadala wa kuliongoza taifa hili ila ni dk slaa tu

Kwa uapande wangu hili jambo nimeona nililete hapa jukwaani nipate michango ya wana jf kwa mitizamo yao tofauti tofauti,
 
Wewe unafananisha treni na bajaji, hivi unaweza kumfananisha Lowasa na mzee wa document za siri? Hii ni sawa na kumtukana Lowasa. Labda ungesema Zitto au Mbowe ndio tunge kuelewa.
 
labda atashinda Urais wa Baraza la maaskof ( TEC) maana ndo ana PHD ya mambo ya dini, Urais wa Nchi hiii NOOoooooooooooo, ikibidi tutagawana fito mkajenge nchi yenu hukooooo kaskazini, kutawaliwa na Padri katika nchi ya kisekula ni Big NOoooooooooo!

umesema kweli kabisaaaaaa.
 
Mnaokataa tusijadiri masuala ya urais 2015 mna hoja gani za msingi? Tukiwajua mapema, tutawapima na kuona. Muda ukifika ni kutekeleza tu. Sera za CCM ni zile zile kwa hiyo hakutakuwa na jipya. Dr. Salim alichafuliwa na mtandao wa JK ulioongozwa na Lowassa, lakini kwa maoni yangu ni mmoja wa wanasiasa bora katika nchi yetu. Dk Shein pia ni mwadirifu na mzalendo pia ni mchapa kazi. Hizo ndizo sifa Kuu tunazozihitaji kwa mahali ambapo kama taifa tumefika. Dr. Wilblod Slaa kwa upande wa upinzani anafaa pia kuongoza Taifa letu. Ni mtu jasiri, mfuatiliaji, makini na mzalendo. Tusiwapime watu kwa kauli zao za kukurupuka katika mambo yanayohitaji umakini katika kufanya maamuzi kwa vile tu watu hao ni marafiki, ndugu au kwa vile tumeahidiwa u DC wakifikia malengo yao. Wapo wanaounda mitandao kwa kutumia mamilioni ya pesa. Wanataka ikulu wakafanye biashara gani ili warejeshe fedha zao? Tuweni makini sana na watu hao. Tukiendelea kufanya makosa kwa makusudi au kwa bahati mbaya, ipo siku wajukuu zetu watachapa viboko makaburi yetu.
 
Rais wa nchi ni yoyote anaye tambua matatizo ya msingi ya nchi na ambaye ana muelekeo ya kuyatatua kwa dhati athibitishe haya kwa kuyaelezea matatizo hayo na kupendekeza suluhu, na kwa taarifa tu tatizo la msingi ni elimu isiyo na tija(unproductive and theoretical education) na kupotea kwa utaifa. Swali ni nani anatambua mambo haya?
 
Tatizo la WaTanzania ni siasa tuuuuuu mwanzo mwisho, uchaguzi ukiisha tunaanza uchaguzi mwingine hatufikirii uchumi, wala maisha ya watanzania yalivyo chokest. Let us concetrate to the country economy then politician will fit in. sasa hivi tunaongelea siasa na wanasiasa wanajiona wako sawa.


lakini katika hao wote hamna hata mmoja anaefaa isipokuwa Salim A Salim tu naye ameshang'atuka mambo ya siasa. Rais atakayefaa ni ambae atakaayetooka nje ya walooza na system na awe nusu democracy na nusu dictator ili kubadilisha kabisaa attitude zawatanzania.
 
Mie kuangalia kwanini watanzania wenzetu ambao tumeona uzalendo wao wanashindwa kuwa maraisi kama vile mrema, lowasa, 6, magufuli, zito, lipumba, na wengine waliowahi kuwania na wanaotarajia ni naona kushindwa kwao kunatokana na sababu mbalimbali lakini mojawapo ni hizi ambazo dr wa ukweli kafanikiwa hivyo njia ya kuwa rais kama uchaguzi huru utafanyika. Sijadili sababu za kimfumo na jadili sababu za mtu kama mtu mwenyewe kukwama

1. Kutokujitambua kwenye chama:
Kama tunavyoelewa Tanzania ili uwe rais ni lazima upate ridhaa ya chama ni dr slaa peke yake amelitambua hili katika utendaji wake kwenye chama amezingatia sheria, kanuni katika kukitumikia chama na hata kukisemea amefanya kazi kama TEAM (together Archieve More) huku mnyika lissu wakijifunza kutoka kwake. Utendaji wa namna hii unakisaidia chama na hata kiongozi mwenye ndoto ya kuwa rais.

Wafuatao wameshindwa katika hli Zito kiongoz ambaye amekuwa akijifanya hazimtoshi akawa anataka yeye aonekane kuliko chama kila jambo chama kina sheria kanuni za kulitenda na kulisema yeye akatawaliwa na hisia matokeo ndani ya chama hisia zimewagawa na si rahisi kumpitisha mtu ambaye sheria na kanuni hakuzitumia akajikuta amewagawa wanachama na hata viongozi na ndivyo alivyofanya mrema cha sisimu miongozo haikumtuma kufanya afanye kila alichokuwa anafanya aliposhtukia hawatafanikisha ndoto yake kwa maamuzi ya pamoja kumpitisha akaenda nccr mwanzo akawaunganisha wakamsimamisha wananchi wakamkubali mfumo ukambania. 6 na Makufuli, membe ongeza wengine kwa kigezo cha ridhaa ya chama nyie ni mshaidi utendaji wao hauna uwalakini kwenye chama na hata mamuzi yao mtihani wa kukubalika kwenye chama wamefeli wakawagawa wanachama. Unaweza kusema walisimamia ukweli kama ningekuwa mimi ningekuwa mvumilivu na kutumia hekima na busara kwani kufanikiwa kwangu kuna tegemea ridhaa ya chama ni tende kutokana na miongozo, sheria na kanuni za chama wamekuwa watu wakugombana na hata mkuu wa nchi bila kutambua kesho wanakujakumwomba ridhaa kwenye michakato wawatumikie watanzania.

Wanachama wa chama ili wakupitishe wanaangalia utendaji na mamuzi yako yamezingatia taratibu za chama, mtihani wa chama wape maksi. Lowasa ametofautiana nao utendaji wake kwenye chama na wamhukumu na sababu ya 2 nitakayoijadili ya utumishi wao kwa wapiga kura. Yeyote aliye na atakayewaza ajitadhimini utendaji wake kwenye chama ukijenga makundi yatakuja kukukataa na ukikiuka miongozo kwenye matendo na maamuzi siku unasimama mbele yao vitakuhukumu. Ni hitimishe kwa sababu hii kwa kuwashauri wazalendo walioko kwenye vyama na watakaojitokeza wasipuuze utumishi wao kwenye vyama kwa kukiuka miongozo,sheria na taratibu Hisia wazitumie kwa uangalifu kwani zitawajengea makundi ya watakaozikubali na la wakatakaozipinga na watakaona ni nzuri kama zingetumia katika ya chama. Dr mpaka sasa viongozi wakimpima utumishi wake na utendaji wake hajawagawa na sheria na taratibu zinampa kura ya ndiyo pimeni na wengine wakisimama kwenye vyama vp Lowasa, lipumba, malimu wanaoutaka urais hawana mgogoro kwenye chama wa kikanuni taratibu na utumishi wapinzani wao na wawakatae kwa sababu ngingine

2. Utumishi wako kwa wapiga kura watanzania:
Licha ya ridhaa ya chama ili uwe rais unahitaji kura za watanzania wa kuanzia unakotoka na wengine. Dr slaa utendaji wake kwa umma wengi wanaukubali, kama vile makufuli, zito, 6 wanachakuwambia watanzania wakawasikiliza wanasiasa wengi wamefaulu kigezo hiki lowasa naye amefaulu swali moja ndilo lililomwangusha kwa kuwaonea huruma wengine akamua kubeba lawama richmond, membe utumishi wake wa mambo ya njee watanzania hawauelewi wanauelewa wanaosafiri issue ya vitambulisho vya uraia wa nchi mbili kuona ni vyema na kupigia chapuo watanzania wanamuona sio mzalendo hawana maslahi na uraia huo wa nchi mbili wanatafsiri ni janja ya wenye nazo kikinuka wasepe.

Nihitimishe ili wengine mchangie kwa kusema 2015 atafanikiwa mtanzania kuwa raisi kwa sababu au vigezo mbalimbali Lakini kama ni katiba iliyopo unayohitaji wagombea wanatokana na vyama kupita kwenye chama wewe mwenye nia utendaji wako kwa kuzingania maamuzi ya pamoja, miongozo, katiba na kanuni si jambo la kupuza liliwagarimu wengi na litawagari wengi maana hawalitambui pia utumishi wako kwa wapiga kura uliotukuta usiokuwa na mawaa ili wakuridhie ni jambo la muhimu hata kama ni udiwani wataulizia. Ni vyema kufanikiwa katika haya mawili kama dr slaa kwenye chama na wapiga kura kwani tatizo la mfumo kama wa uchaguzi kura. Watanzania wanaweza wakaupinga ndio maana alama za nyakati zinaushulikia kuepusha vita.

Nb: ni alike maoni, sababu ngingine zinazowakwamisha watanzania waliohata hatarisha kazi zao na kufanya mambo ya kipekee ila walipoomba nafasi wakashindwa kwenye chama au kwa wapiga kura ili waliopo na watakaokuja wajifunze namna watakavyoweza kuridhiwa na chama na watanzania kama dr anavyo jitahidi.

Mie nimeona SLAA amefanikiwa katiaka sababu hiz 2015 ni kumuombea jia njeupe na Akosee TOA MAONI KWAKE NA KWA WENGINE KWA HOJA
 
dr.slaa ana uzalendo utash na weledi....na pia ni chaguo namba moja la watz.,
 
Maoni yangu;rais atakuwa Mkristu. We want Christian values for a change. Watu wakimchagua Mwislamu,chances ni kwamba wakirudi tena kupiga kura watamchagua Mwislamu.Aspect ya Lowassa ni kwamba yeye ni fisadi,whether he agrees with that or not. Kumchagua Lowassa maana yake ni kufumbia macho yeye kuitwa fisadi. Asha Rose Migiro anaweza kuwa rais,lakini sijui kama anaweza kuchaguliwa kuwa rais.
 
Maoni yangu;rais atakuwa Mkristu. We want Christian values for a change. Watu wakimchagua Mwislamu,chances ni kwamba wakirudi tena kupiga kura watamchagua Mwislamu.Aspect ya Lowassa ni kwamba yeye ni fisadi,whether he agrees with that or not. Kumchagua Lowassa maana yake ni kufumbia macho yeye kuitwa fisadi. Asha Rose Migiro anaweza kuwa rais,lakini sijui kama anaweza kuchaguliwa kuwa rais.

Sio maoni yako raisi atakuwa mkristo,bt ni zam ya mkristu ss,coz tunaenda kwa zam......slaa pekee ndo anaweza,mzalendo
 
Sio maoni yako raisi atakuwa mkristo,bt ni zam ya mkristu ss,coz tunaenda kwa zam......slaa pekee ndo anaweza,mzalendo

Kama ni mambo ya zamu basi mwaka huu ni zamu ya Wazanzibari kwa maana sisi wabara tumetoa Rais kwa miaka 20 mfululizo!!
 
Watanzania walikuwa wameamini baada ya kushindwa Arumeru basi Lowassa atakuwa amekufa kisiasa. Lakini kambi yake ni makini sana na wanaijua vema fitna ya kisiasa na wana ngawira balaa. Sasa ni dhahiri mgombea wa CCM atakuwa Lowassa, Chadema Dr Slaa na CUF Prof Lipumba. Unless afya ya mmoja wao au baadhi yao iwe ni mgogoro sioni namna ya kuwashinda hawa katika vyama vyao. Je, wakiingia ulingoni nani unadhani atashinda?
 
Itakuwa vita ngumu sana ila naamini Dr Slaa ataibuka mshindi. Tatizo kutakuwa na hila nyingi hasa kuwanunua watu wa chadema na kuiba kura ila nadhani Chadema nao wamejitayarisha vilivyo na hilo
 
Dr.WP Slaa ni rais wa mioyo ya watanzania sasa na mpaka 2015.....Ee Mola wetu mlinde rais huyu umpe afya njema atufikishe kwenye nchi ya ahadi.
 
Tuwe wakweli jamani, hivi CUF na Chadema ni chama gani kinaonekana cha kidini zaidi. Cuf mikutano yake waislam watupu, viongozi wake na wanachama wake waislam watupu, chadema ni cha kitaifa zaidi. Mimi kura yangu no kwa Dr wa ukweli
chadema wakitaka ku win wa msimamishe mwingine ila siyo padrii slaaa
 
Mtoeni Lipumba hapo amejaribu vya kutosha na majibu anayo kwamba kura zake hazitoshi. Maybe akagombee uraisi Zanzibar this time.
 
Back
Top Bottom