Kama serikali itang'ang'ania kuwalipa DOWANS; CHADEMA kuitisha maandamano ya nchi nzima

Una maana mkataba wa Richard una saini ya Mkurugenzi wa Tanesco?

Sijui una signature ya nani. Lakini mkataba si kati ya Tanesco na Richard?

Tanesco ni mtu binafsi (a corporate body) na hivyo anasimamia mikataba yake mwenyewe na kudaiwa yeye, na kufilisiwa yeye.
 
Hoja ya serikali ni dhaifu sana kwenye hii kesi. Kwa ninachoelewa ni kuwa wanasema taratibu za serikali hazikufuatwa kwenye kusaini mkataba kwa hiyo mkataba sio halali.

Ni kama nije kwako kununua gari tukakubaliana na kusign mkataba kuwa umeniuzia gari kwa 10 million, kisha kesho kutwa naanza kupiga kelele kuwa sikukubaliana na mke wangu kabla ya kuja kununua gari kwa hiyo mkataba sio halali, huu ni upuuzi wa hali ya juu.

Zaidi ya hapo ICC sio mahakama yenye nguvu za kisheria, kazi yake ni kusuluhisha matatizo baina ya kampuni na masuluhisho hayo yote ni kwa hiari! So kwa kifupi huu ni mchezo wa kuigiza.

mhh...on the contrary, that is a very strong point kwenye sheria. Kama wewe una vitu unavyotakiwa kufanya kabla ya ku-sign mkataba, basi ukivivunja, huo mkataba unaweza kuwa voided! Hapa sio mambo ya baba na mama mkuu!hahaha
 
Hauwezi kuvunja, si makosa ya uiliyosign naye kuwa haukufuata utaratibu wako wa ndani, hiyo hoja ni bogus. Utaratibu wa ndani wa Tanesco au serikali hauwawhusu Dowans, ndo maana wameshinda ICC.
 
Sijui una signature ya nani. Lakini mkataba si kati ya Tanesco na Richard? Tanesco ni mtu binafsi (a corporate body) na hivyo anasimamia mikataba yake mwenyewe na kudaiwa yeye, na kufilisiwa yeye.

Na mimi naweza kusaini kama Tanesco
 
Tanesco: Kuilipa Dowans ni kuitia nchi katika giza
Tuesday, 18 October 2011 20:59
0diggsdigg

Waandishi Wetu
Mwananchi

SHIRIKA la Umeme Tanzania (Tanesco) limewasilisha Mahakama Kuu, maombi ya kusimamisha utekelezaji wa malipo ya fidia ya mabilioni ya fedha kwa kampuni ya kufua umeme ya Dowans likidai kuwa kama utekelezaji wa hukumu hiyo utaendelea, utaathiri uwezo wake wa kuzalisha na kusambaza umeme na kusababisha tatizo kubwa la ukosefu wa umeme.Tanesco kupitia kwa mawakili wake, Kampuni ya Rex Attorney iliwasilisha maombi hayo mahakamani hapo jana baada ya uamuzi wa mahakama hiyo kusajili tuzo ya kampuni hiyo iliyotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Kibiashara (ICC).

Mbali na Rex Attorney, pia Tanesco inatetewa na Kampuni ya FK Law Chambers Advocates pamoja na Mkuu wa Shule ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Palamagamba Kabudi.

Novemba 15, 2010 AICC, chini ya Mwenyekiti wake, Gerald Aksen akisaidiwa na wasuluhishi Swithin Munyantwali na Jonathan Parker, iliiamuru Tanesco iilipe Dowans fidia ya Sh94 bilioni kwa kuvunja mkataba baina yake na kampuni hiyo kinyume cha sheria.

Baada ya uamuzi huo wa ICC, Januari 25, mwaka huu Dowans iliwasilisha maombi Mahakama Kuu, Dar es Salaam ikiomba tuzo yake hiyo isajiliwe ili utaratibu wa ulipwaji wake uwe na nguvu ya kisheria, lakini Tanesco ilipinga usajili huo.

Septemba 28, mwaka huu Mahakama Kuu iliisajili tuzo hiyo na hivyo kuipa nguvu ya kisheria Dowans kulipwa mabilioni hayo uamuzi ambao Tanesco haikuridhika nao na hivyo kuanza mchakato wa kukata rufaa kuupinga.

Katika maombi ya jana, Tanesco imedai kuwa iwapo maombi yao ya kusitisha malipo ya Dowans hayatakubaliwa, itapata hasara kubwa isiyoweza kufidiwa kwa kuwa kiasi hicho cha fidia ni kikubwa hivyo kusababisha kusimama kwa shughuli zake za kila siku.

Katika maombi hayo pia limetoa hoja mbalimbali za kisheria ambazo linadai kuwa Mahakama ya Rufani inapaswa kuzitazama kabla kuruhusu utekelezaji wake.

Mawakili hao wa Tanesco wameiomba mahakama hiyo kuzingatia maombi hayo kwa madai kuwa hasara itakayotokana na tatizo la ukosefu wa umeme itakuwa kubwa na isiyoweza kufidiwa kwa namna yoyote ile.

Walidai kuwa ingawa taarifa ya kusudio la kukata rufaa siyo kigezo cha kuzuia utekelezaji huo, hoja za kesi yake ni nzito kiasi cha kutosha kuifanya Mahakama kutumia uwezo wake wa kisheria kuzingatia maombi yao.

“Mahakama ina uwezo wa kuamuru kusimama kwa utekelezaji huo kwa namna itakavyoona inafaa,” wamesisitiza mawakili hao wa Tanesco katika maombi hayo na kuongeza: “Ikiwa maombi ya amri ya kusimamisha utekelezaji hayatakubaliwa na Dowans ikiruhusiwa kutekeleza uamuzi huo, rufaa inayokusudiwa haitakuwa maana tena.”

Wakili wa Dowans, Kennedy Fungamtama alisema kwa sasa kiasi cha fidia ambayo Tanesco inapaswa kuilipa Dowans kinafikia Sh111bilioni ikiwa ni ongezeko la riba ya asilimia 7.5 kutokana na Tanesco kuchelewa kulipa tangu tuzo hiyo ilipotolewa na ICC.

Sitta hataki kusikia kuilipa Dowans
Katika hatua nyingine, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika wa Mashariki, Samuel Sitta amesisitiza msimamo wake kwamba hakubaliani na malipo ya Kampuni ya Dowans na kusema kama angekuwa na mamlaka, angepiga marufuku malipo hayo.

“Hakuna haki yoyote na wajibu wa kuilipa kampuni ya kitapeli ya Dowans kwa kuwa kuanzia mikataba yake hadi hii leo ni haramu, hivyo basi siyo sahihi kujichotea fedha hizo,” alisema Sitta jana katika kipindi kilichorushwa hewani na Kituo cha Televisheni cha ITV.

“Tanesco waliweka masharti 24 ili mtu akidhi kupata tenda hiyo, lakini kamati iliyoundwa na Serikali ikayapunguza hadi kufikia manne.

Hata hivyo, Richmond haikuweza kukidhi masharti hayo licha ya kupunguzwa na baada ya kushindwa ikamkabidhi binamu yake, Dowans wakati nayo haikuwa imekidhi masharti hayo, sasa huoni ni haramu na hawafai kulipwa?” alisema Sitta na kuongeza: “Hapa ni sawa na refa katika mpira anapolazimisha timu fulani kushinda wakati imeelemewa hivyo kuinyong’onyesha timu pinzani.”

Imeandikwa na James Magai na Elias Msuya.

Hauwezi kuvunja, si makosa ya uiliyosign naye kuwa haukufuata utaratibu wako wa ndani, hiyo hoja ni bogus. Utaratibu wa ndani wa Tanesco au serikali hauwawhusu Dowans, ndo maana wameshinda ICC.

Kama kuna sheria inayosema contract lazima ifanywe hivi na vile na haikufuatwa, ni wazi kuwa hiyo ni an illegal contract, hence a void contract. Utaratibu wa sheria lazima ufuatwe.

Ama sivyo mimi naweza kuingia katika contract na wewe ya kuua mtu na mwisho kwenda mahakamani kudai malipo. Hiyo contract ni illegal maana imevunja sheria za nchi! Kama ilivyokuwa ya Dowans.
 
Nimeomba Mods wafungue sub-forum ya Dowans ili tuweze kuweka info zake zote huku, na kuzisoma kirahisi, lakini wapi!

Ningependa kujua ni lini Dowans walirithi huo mkataba wa Richmond.
Ripoti na matokeo ya Kamati ya Bunge kufuatilia Richmond.

Na Richmond iliwezaje ku-assign mkataba kwa Dowans!
Pia hiyo hukumu ya ICC.
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo kimesema kitaandamana nchi nzima endapo serikali itaailipa kampuni feki ya Richmond a.k.a Dowans. Kauli hiyo ni imetolewa na Mnyika makao makuu ya CDM jijini Dar- Es - Salaam. Hii ni mara ya pili kwa CDM kusema kuwa itaandamana nchi nzima endapo serikali itailipa Dowans.

Swali la msingi je maandamano yatasaidia Dowans kutolipwa?
Source ITV Habari.

Sasa wakiandamana baada ya malipo itasaidia nini? mimi nashauri waandamane kabla ya malipo ili washinikize yasilipwe? Serikali inaweza kusita kulipa ikiwa maandamano yataonesha kuwa watu wengi hawayaungi mkono.
 
Tanzania ni lazima ilipe hili tuzo. Hauwezi ukaingia mkataba na watu halafu ukaja kuuvunja kienyeji na utegemee kupona hivi hivi.

Kama Tanzania ikilazimisha kutolipa, hili taifa litaonekana ni taifa ambalo hauwezi ukafanya nalo biashara. Tutaonekana sisi ni ma Bob Mazishi. Watu wataogopa kuwekeza Tanzania wakihofia kupoteza hela na nguvu zao.

Jamani, mkataba ni mkataba. Hakuna mkataba feki - hizi ni Siasa. Tumeingizwa hapa tulipo kutokana na wanasiasa wawili kutoelewana na koneshana umwamba.

Tunatakiwa tufunge huu ukurasa wa Dowans na kuendelea na maisha yetu. Tanzania haiwezi kuangamia kwa kuwalipa hiyo tuzo, ni pesa ndogo sana kwa nchi inayojituma. Lakini kutolipa hiyo tuzo kunaweza kabisa kuligharimu taifa kwa kukosa heshima ya kuwa ni taifa unaloweza kufanya nalo biashara.

Mwisho kabisa; tunahiotaji wawekezaji, siyo wafadhili.
 
Nakubaliana nawewe. Ni bora busara zaidi ikatumika maana watanzanai hatuishi katika visiwa. Kama makosa yalishafanyika tutafute suluhisho bila kwenda kinyume na utaratibu wa kistraarabu unaokubalika kimataifa na bila kuvunja katiba yetu wenyewe.

Maamuzi ya ICC japo yanawahusu watu waliafikiana kwa hiyari yao wenyewe ni ya kimahakama na yana nguvu ya kisheria kama maamuzi ya Mahakama Kuu ya Tanzania yanaposajiliwa.

Nionavyo mimi sio muda muafaka sana katika kujadili kutekeleza au kutotekeleza hukumu ya Dowans kujadili uhalali wa assignment ya mkatba wa Richmund. Maana, mali zilizopatikana kutokana na assignment hiyo hiyo zimeshauzwa katika kampuni nyingine ya kimarekani na hilo halilalamikiwi.
 
Ningekuwa mimi serikali ningefanya hivi:
1. Tanesco ikubali kuilipa Dowans.
2. Tanesco inavunjwa na kutengenezwa kampuni nyingine ya Umeme kwa kupitia Statutory Law (kumbuka Statute tramps Case Law)
3. Tanesco seizes to exist and Dowans has no claims on the new company.

End of Story
 
Wasiwawasi wangu ni kama inawezekana kupinga maamuzi ya mahakama, Ninachodhani mimi ni kudai hawa waliotufikisha hapa washikishwe adabu
 
Ningekuwa mimi serikali ningefanya hivi:
1. Tanesco ikubali kuilipa Dowans.
2. Tanesco inavunjwa na kutengenezwa kampuni nyingine ya Umeme kwa kupitia Statutory Law (kumbuka Statute tramps Case Law)
3. Tanesco seizes to exist and Dowans has no claims on the new company.

End of Story
[/QUOTE

Kaka hiyo imetulia. Issues zitakuwa mbili. Mosi, wanaweza kutrace mali za Tanesco zimehamiaji kwa kampuni mpya. Pilli, Tanesco kama kampuni haiwezi kujiwind up na hatimaye kuwa liquidated bila notice kutolewa kwa umma na mrajisi wa makampuni. Ni wazi wadeni wake wakiona Tangazo kwamba Tanesco wanataka kuundergo voluntary winding up watajitokeza kama wadeni na kama Tanesco watashindwa kuthibitisha ukwasii wao (solvency) Dowans wanaweza kulazimisha compulsory winding up. Tatu, hata kama zoezi la winding up na dissolution litafanikiwa mali za Tanesco zitakazobaki baada ya kulipa madeni zitaenda kwa Msajili wa Hazina na Dowans wanaweza kudai utekelezaji wa haki yao kwa Msajili wa Hazina
 
ni kweli uliyosema, lakini hivi vyote vinaweza kuwa blocked by sheria mpya itakayotungwa na bunge na kuilinda hiyo kampuni mpya. I have seen this happening mara nyingi katika nchi zilizoendelea. Mahakama inaweza kusema kitu fulani, alafu ghafla bunge linatunga sheria ku-circumvent hiyo hukumu ya mahamaka na interpretation yake.
Nakubali kuwa its not a good thing, na itaogopesha wawekezaji, lakini ni moja ya njia za kuzuia malipo kisheria kama unavyotaka.
 
Back
Top Bottom