Kama noma na iwe noma!

ha ha ha!mkuu kwa 300,000 naweza nunua hata 10!ila running cost naweza kuweka poni mke!any way wazo lako zuri limenifurahisha!

Nikweli hayafai hata kidogo maana chanzo cha habari za magari hayo kilisema yameenda over 150,000 KM maana yake fuel consumption ipo around 3 to 4 km per litre sasa piga hizo 25 km toka kwako utahitaji karibu litre 8 per trip au litre 16 kwenda na kurudi (achilia mbali foleni za dar).
 
tembelea mtandao wa www.tradecarview.com angalia brand za magari december hii wako cheap kiasi.mtafute agent wa kuclear unaemjua.nakushauri uagize moja kwa moja na kama upo serikalini utachukua excemption.ni mpango mzuri angalia magari ya toyota ndo mazuri NEVER TRY MITSUBISHI. PROCESS ZA KUAGIZA ZIPO.kazi kwako. kwa hela yako ukipata gari ya FOB $5000 INATOSHA TENA YA KUANZIA 2003.ANGALIA PIA SUZUKI.
HONGERA KWA UAMUZI MZURI
FOB ndo nini mkuu hebu chakachua kabisa $ 5000 kwa madafu mkuu!

.
 
FOB ndo nini mkuu hebu chakachua kabisa $ 5000 kwa madafu mkuu!

.
kaka FOB ni bei ya gari kama linavouzwa bila kuweka usafirishaji wake na ukaguzi .Hivo tuseme kwa dola 3500 unapata gari zuri sana kuanzia mwaka 2003 ukaguzi huwa ni dola 200 au 300 na shipping ni 1200 jumlani dola 5000 ndo wanaita CIF mimi si mchumi wa hizo terms inategemea na kampuni unayoagiza.kama uko serious ntakupa agent ukamwone yeye atakusaidia zaidi au ukamwona agent ambae unamwamini manakae wao wakiagaiza kwa jina la kampuni yao huwa wanapunguziwa dola kama 300 au zaidi.cha muhimu kuagiza lazima iwe oda yako mwenyewe ili gari lije kwa jina lako kupitia kwa huyo agent.kulipa ulipie mwenyewe bank ukishatumiwa profoma invoice na hiyo kampuni ya magari unayoagizia then ukipata TT unampa agent wako aprocess mengineyo.ni rahisi tu kwa makampuni yanayofahamika kama hilo nlikupa web address yake.hope umeridhika kaka.Kwa hela yako unaweza pia kuchagua gari la dola 4500 pia.
 
Nikweli hayafai hata kidogo maana chanzo cha habari za magari hayo kilisema yameenda over 150,000 KM maana yake fuel consumption ipo around 3 to 4 km per litre sasa piga hizo 25 km toka kwako utahitaji karibu litre 8 per trip au litre 16 kwenda na kurudi (achilia mbali foleni za dar).
Mkuu umenigusa. Ina maana consumption ya fuel per km inaongezeka kadri gari linavyokuwa zee mimi niliagiza toyota noah ya mwaka 2001 ikiwa na km 135,000 nashangaa natumia lita 6 hadi 7 per km wakati jamaa yangu aliniambia noah zinatumia lita 10 hadi 12 per lita. Nifahamishe mkuu ili nianze process za kuliuza
 
Magari ya Mitsubishi ni vimeo sana hasa haya madogo...usijaribu kabisa hiyo brand!!! ni wazuri katika kutengeneza trucks tu.....cheki Toyota family itakufaa

Kwa ushauri wa wabongo lazima uambiwe toyota, ila kwa ushauri wangu hata mitsubishi ni poa tu, nimetumia aina tofauti za magari kwa muda sijaona tofauti yoyote tena unapokuwa na brand tofauti na toyota mara nyingi unajikuta una gari la kipekee... swala la spare ukweli siku hizi zimejaa na isitoshe ukiagizia ni siku chache unapokea..

Best of luck....
 
post ya huyo ndugu Polisi sijaelewa...
Km 6 au 7 per litre? Au anakusudia vipi? Maana ndio twajifunza wote ili tusiingie mikenge ya moto-kaa.
 
post ya huyo ndugu Polisi sijaelewa...
Km 6 au 7 per litre? Au anakusudia vipi? Maana ndio twajifunza wote ili tusiingie mikenge ya moto-kaa.
Maalim niliquote maneno ya nyantella. Yasome vizuri. Hata mimi nilipigwa na mshtuko. Ukisoma vizuri post ya nyantella utagundua kuwa ni kama anamaanisha kuwa kadri gari linavyokuwa na km nyingi ndo na consumption ya fuel inavyoongezeka. Na mimi nilikuwa naomba ufafanuzi. Tusaidieni jamani
 
post ya huyo ndugu Polisi sijaelewa...
Km 6 au 7 per litre? Au anakusudia vipi? Maana ndio twajifunza wote ili tusiingie mikenge ya moto-kaa.

nilivyo muelewa mm nikuwa akiweka mafuta lita 1 yataisha baada ya kusafiri kilometa 6 au wakati mwingine 7
 
nami nlielewa vzuri...ndio vile nkaweka swali langu kwenye thread ili nimkumbushe kaka Polisi a.k.a Afande. Namshukuru ameelewa...
Siku hizi wanaelewa(joke).
Nyantella nimemkubali hisabu zake! Ahsante kwa kuweka sawa haya mahisabu.
 
Zamaulid,ahsante kwa ufafanuzi!
Niliogopa kumwachia atuchanganye humu GF....nlijua humu gf wapo watu makini.
Ukirejea thread yake utaona alikua anatumia uzoefu wake kutaka atuchanganye!
 
wakuu, heshima mbele!
Nimevumilia kugombania daladala kila nitokapo na kurudi nyumbani nimechoka!!nimeamua potelea mbali kama noma na iwe noma na mm nataka nishiriki kuongeza foleni ya magari dar!

Naomba mnisaidie yafuatayo!
1.nimejikusanya na bajeti yangu inafikia 13m!
2.je kwa hela hiyo naweza kuagiza mitsubish pajero i10?
3.nina stay 25 km hadi kazini kwangu,je nitahitaji lita ngapi ya mafuta go and return?

Naomba kuwasilisha, mkinishauri na mambo mengine mnayodhani yatanisaidia ili nisiingie kichwa kichwa!



model ya engine tafuta 4s ni roho ya paka
 
Vipi wewe ni mtumishi wa umma?kama ni mtumishi wa unaweza kupata msamaha wa kodi!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom