Kama noma na iwe noma!

Zamaulid

JF-Expert Member
May 25, 2009
18,654
13,475
wakuu, heshima mbele!
nimevumilia kugombania daladala kila nitokapo na kurudi nyumbani nimechoka!!nimeamua potelea mbali kama noma na iwe noma na mm nataka nishiriki kuongeza foleni ya magari Dar!

naomba mnisaidie yafuatayo!
1.nimejikusanya na bajeti yangu inafikia 13m!
2.je kwa hela hiyo naweza kuagiza Mitsubish pajero i10?
3.nina stay 25 km hadi kazini kwangu,je nitahitaji lita ngapi ya mafuta go and return?

naomba kuwasilisha, mkinishauri na mambo mengine mnayodhani yatanisaidia ili nisiingie kichwa kichwa!
 
ndo maana nimeamua kutafuta ka-mkoko maana kukimbia kimbia kama inavyoonyesha hiyo avatar nimechoka!
 
Nakushauri tafuta Toyota. Pajero ni nzuri bali spare parts zake si rahisi kupatikana.
 
sikushauri kwenye Pajero check brand ingine kama toyota, suzuki hivi ni poa

kwanini boss!naviona viko vingi barabarani nikadhani viko poa!!ila muundo wake naupenda,hiyo injini ndo sijui utendaji wake na mapungufu yake!!
 
Toyota Escudo... You cant go wrong

kuna kipindi nilikuwa napenda sana escudo!tatizo kila nikichungulia kwenye mtandao bei yake naona iko juu,unadhani kwa hiyo figure niliyo iweka hapo naweza pata escudo!!
 
Toyota iko poa,pajero spare ziko juu na nadra kupatikana.Na pia Pajero mafuta inapakia sana .Kibongo bongo TOYOTA ziko sawa kaka.But kama upo sawa financially chukua kitu roho inapenda tofauti na hapo utazua utata
 
Magari ya Mitsubishi ni vimeo sana hasa haya madogo...usijaribu kabisa hiyo brand!!! ni wazuri katika kutengeneza trucks tu.....cheki Toyota family itakufaa
 
Kaka hongera kwa kuwa na malengo ya maendeleo! lakini kuwa makini kama utafanya uamuzi wa kununua hapohapo dar, maana hapo kuna gri nyingi zilizozungushwa sasa nyingi card zao ni famba.
Tulia utapata gari nzuri na yenye vielelezo halali.
 
wakuu gusieni basi na hiyo bajeti niliyowapa!ka-4wheel katapatikana?
 
wakuu gusieni basi na hiyo bajeti niliyowapa!ka-4wheel katapatikana?

ka 4wheel kanapatikan ila suzuki model ya zamani naana ya 1996 mpaka 98 kwa kuagiza iatakutafuna kidogo kwa sababu in kodi zaidi ya 4 hiyo new model yake yaani ya 2001 imekomaa bei kidogo bajeti yako pungufu mkuu. mi nakushauri ingawa umesema hupendi garizinazofana na taxi nunua toyota corrola x nze121 kwanza ni nzuri sana pili concumption ya mafuta ni nzuri sana sababu cc zake ni 1300 mpaka 1500 kwa umbali wako wa kilimeta 25 itakufaa mkuu ila kama barabara ni nzuri ya uendako, kama barabara zetu hizi tafuta hiyo 4wheel kama suzuki ipo juu kidogo na bei za hapa utapata kuanzia 9m mpaka 10m ila uwe mwangalifu sana madalali wana njaaaa sana wasije kukuingiza town. usiwe na haraka fanya taratibu na kwa maringo ok mkuuu
 
mkuu ahsante sana kwa ushauri nitaku pm baadaye kwa ushauri zaidi!
 
Mkuu, tuliambiwa hapa kwamba serkali inauza yale mashangingi yake ya mwaka jana kwa sh 300,000 tu. Hebu jaribu mkuu uone Kama watakuuzia kisha utuhabarishe
 
Mkuu, tuliambiwa hapa kwamba serkali inauza yale mashangingi yake ya mwaka jana kwa sh 300,000 tu. Hebu jaribu mkuu uone Kama watakuuzia kisha utuhabarishe
ha ha ha!mkuu kwa 300,000 naweza nunua hata 10!ila running cost naweza kuweka poni mke!any way wazo lako zuri limenifurahisha!
 
tembelea mtandao wa www.tradecarview.com angalia brand za magari december hii wako cheap kiasi.mtafute agent wa kuclear unaemjua.nakushauri uagize moja kwa moja na kama upo serikalini utachukua excemption.ni mpango mzuri angalia magari ya toyota ndo mazuri NEVER TRY MITSUBISHI. PROCESS ZA KUAGIZA ZIPO.kazi kwako. kwa hela yako ukipata gari ya FOB $5000 INATOSHA TENA YA KUANZIA 2003.ANGALIA PIA SUZUKI.
HONGERA KWA UAMUZI MZURI
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom