Kama ningekuwa Mgombea....

Ningekuwa mgombea ningehakikisha yafuatayo yanakuwa ngao yangu kwenye kampeni.

1. Kurudisha na kuimarisha Heshima na Hadhi ya Mwananchi na Taifa la Tanzania.
2. Kurudisha na kuimarisha Heshima na Hadhi ya kazi na kufanya kazi kwa Watanzania wote, vijijini na mijini.
3. Kuimarisha Ufanisi na Ustawi wa Jamii katika kupiga vita Ujinga, Umasikini, Njaa na Maradhi.
4. Kubuni mbinu za kumpunguzia mzigo mwananchi wa kawaida(haswa wenye vipato vya chini na wakulima)au kama tunavyowaita Walalahoi.
5. Kuhakikisha kuwa Sheria, Katiba na Kanuni zilizowekwa zinafuatwa ipaswavyo na vyombo vyote husika na Wananchi. Aidha kuweka maamuzi na mipango ya Serikali wazi kwa wananchi wote, kwa kuwa wao ndio waliotoa dhamana.
6. Kuwaelimisha Wananchi haki zao,wajibu wao na sehemu yao katika Taifa.
7. Kuhakikisha kuwa vita dhidi ya Rushwa, Ubadhilifu, Udini, Ukabila na kutowajibika kwa watendaji wa Serikali na tasisi zake vinaendelezwa kwa kushirikisha Wananchi.
8. Kuhakikisha kuwa njia kuu za Uchumi zinaboreshwa na kutumika kwa manufaa ya Taifa.
9. Kuhamasisha na kuhakikisha kuwa Uzalishaji mali(Kilimo, Viwanda,Uvuvi, Ufugaji, Biashara, Madini, Utalii na Maofisini) unafanyika kwa dhati, Kisayansi,kiushindani, kiuwajibikaji na kwa ubora.
10. Kuhakikisha kuwa Huduma za Msingi zinafikishwa kwa Wananchi:- Afya, Elimu, Maji safi, Barabara na Chakula.
Mawazo ya huyu mchungaji ni kama ya malaika. Tindikali nakuunga mkono. Watu wengine bwana sijui wakweje. Anyway labda kashapata bia moja ndo maana anakuja na ndoto zake humu
 
Kwa nini mlipokee hili kama ni lazima Mchungaji agombee? Kwa nini mstumie hivi vigezo kuwapima hao wanaogombea katika majimbo yenu au hata kuwataka watimize haya kama mnayaona n bora na lazima kwa Taifa lenu?

Badala ya kukaa na kutafakari maana ya kilichoandikwa au kuoanisha na mfumo wa uongozi na wanasiasa wetu, mnaimbilia ujuvi wa kebehi!

Mara nyingine inasikitisha kama si kuudhi mtu anapopewa mkate autumie kisha anang'aka, mbona hujanipa siagi au nyama ya kuendana na mkate! Damn it!
 
wote wanabeba ngao iyoiyo, so hakuna chakuchukua hapo. kwanza tumechoka na wanasiasa tutajiongoza wenyewe
 
Badala ya kukaa na kutafakari maana ya kilichoandikwa...
Hivi kuna kutafakari gani katika sentensi hii: Kuhakikisha kuwa Huduma za Msingi zinafikishwa kwa Wananchi:- Afya, Elimu, Maji safi, Barabara na Chakula. au hii: Kuhakikisha kuwa njia kuu za Uchumi zinaboreshwa na kutumika kwa manufaa ya Taifa.

Eti umetupa mkate, huu nao mkate: Kuimarisha Ufanisi na Ustawi wa Jamii katika kupiga vita Ujinga, Umasikini, Njaa na Maradhi.?

Mambo ya siasa za darasa la tatu, adui yetu ni? Watoto wote wananyosha vidole, mwalimu anasema haya jibuni wote kwa pamoja watoto wazuri: UJINGA, UMASIKINI NA MARADHI! Ndio unaleta JF tutafakari eti ungegombea? Ungeshindwa hata kiti cha katibu wa balozi wa shina wewe. Eti utahakikisha njia kuu za uchumi zinaboreshwa. Kivipi? Wakosoaji kwenye makochi ya kubinjuka, hata hawajui nini kinaendelea eneo la tukio.

Nini kinafuatia, ungeleta mvua? Unashindwa hata na mwenzio Profesa Maji Marefu kajitosa kugombea.
 
I second position ya Tindikali kwa 110%.
Nadhani anachokosea kidogo (au pengine labda haeleweki tu) ni method ya kukitanabaisha anachokisema.
Haya anayoyasema Rev Kishoka utayakuta kwenye mlolongo wa ahadi (sijui ilani?) za viongozi wengi tu (waliopo na waliopita) - hivyo inafanya arguments za Rev (japo on paper zinakupa impression ni nzuri sana) zionekane ni nadharia zilezile tulizozizoea.
Anachotakiwa kutufundisha zaidi Rev.....how can he tangibilise them without necessarily kugombea kama anavyo-argue Tindikali??
 
Issue kubwa sio What is the problem issue kubwa ni HOW , mbinu gani, njia gani waheshimiwa wanatakiwa kusema watatatuaje matatizo.

Matatizo ya sisi watanzania ni common ndio maana binfsi sioni kama kuna haja ya kuwa wa bunge zadi 100. Mtatatizo ya jimbo na mwanza vijijini hayana tofauti na Matatizo ya jimbo la Urambo au Rungwe. Wenzetu wameshamaliza coomon problem na wana area specific problem ndo maana wanahitaji wawakilishi wengi.

Ningekuwa mbunge ningependekeza idadi ya majimbo mkoa wangu upunguzwe na gharama za mishahara na kuendesha uchaguzi zitakazookolewa ziingizwe kwenye maendeleo ya wilaya/mkoa

Yes Kama tukifuta mbunge 1ja Wilayani tuna uwezo wa kupeleka visma 12 vya maji kwenye vijiji kwa mwaka kutokana na mshahara wa mbunge.

Ni mfano wa ideas kama hizi watu ndo wanataka kusikia no matter zitakubalika au vipi. wa hiy usiwe mkali Rev ni changamoto watu wanataka waone data zaidi. Japo hugombei lakini umeshajivika ugombea.
 
Kwa nini mlipokee hili kama ni lazima Mchungaji agombee? Kwa nini mstumie hivi vigezo kuwapima hao wanaogombea katika majimbo yenu au hata kuwataka watimize haya kama mnayaona n bora na lazima kwa Taifa lenu?
Badala ya kukaa na kutafakari maana ya kilichoandikwa au kuoanisha na mfumo wa uongozi na wanasiasa wetu, mnaimbilia ujuvi wa kebehi!

Mara nyingine inasikitisha kama si kuudhi mtu anapopewa mkate autumie kisha anang'aka, mbona hujanipa siagi au nyama ya kuendana na mkate! Damn it!

Usesha ambiwa viongozi wengi huwa na lugha nzuri na ahadi ,mikakati mizuri kushinda uliyo hainisha hapa.
Ndio maana watu hawoni kipya hapa ktk maneno yako is all same old stories.
So huwezi kuwa mkombozi kwa kusema haya hapa hujatoa Mkate wala bumunda kwa hivyo hatulili hiyo wala hatuhitajia siagi.
Pia kwa nini unajitoa na kusema "nimewapatia siagi" wewe si nchi yako ? dam ! its wacky man dont be with that attitude
.
 
Issue kubwa sio What is the problem issue kubwa ni HOW , mbinu gani, njia gani waheshimiwa wanatakiwa kusema watatatuaje matatizo.

Matatizo ya sisi watanzania ni common ndio maana binfsi sioni kama kuna haja ya kuwa wa bunge zadi 100. Mtatatizo ya jimbo na mwanza vijijini hayana tofauti na Matatizo ya jimbo la Urambo au Rungwe. Wenzetu wameshamaliza coomon problem na wana area specific problem ndo maana wanahitaji wawakilishi wengi.

Ningekuwa mbunge ningependekeza idadi ya majimbo mkoa wangu upunguzwe na gharama za mishahara na kuendesha uchaguzi zitakazookolewa ziingizwe kwenye maendeleo ya wilaya/mkoa

Yes Kama tukifuta mbunge 1ja Wilayani tuna uwezo wa kupeleka visma 12 vya maji kwenye vijiji kwa mwaka kutokana na mshahara wa mbunge.

Ni mfano wa ideas kama hizi watu ndo wanataka kusikia no matter zitakubalika au vipi. wa hiy usiwe mkali Rev ni changamoto watu wanataka waone data zaidi. Japo hugombei lakini umeshajivika ugombea.
Tuko pamoja. Walau hii umetoa a tip of iceberg ya tangibles we are craving for.
 
Hivi kawaida wabunge wenu huahidi kitu gani? na baada ya miaka mitano mnawapima kwa vitu gani?

Ukiangalia sikuahidi mvua au kile ambacho hakipo kwenye uwezo, si suala la shule, barabara au pembejeo, bali ni haki za msingi za Mtanzania ambazo tunazipuuzia kila siku.

Kwani hadhi ya Mtanzania ikoje au hamuijui? Kwa nin mfananishe kauli zangu na wagombea wengine? kwani wao wametoa kauli gani mpaka mfanye zangu kuwa ni sawa na zao?

Nimetumia neno ngao, kwa makusudi ikiwa na maana ya kuonyesha wazi kuwa kwa kuwa nitakuwa nimeishi na wananchi, na wanajua utendaji kazi wangu, haiba yangu na dhamira yangu, iweje iwe vigumu kwao kuelewa anachokisema Mchungaji?

Mchungaji anatoa ahadi si ya mali au vitu, bali ni vitendea kazi na vitu vya kawaid akabisa ambavyo vinawekwa nyuma ya basi kwa kuwa kila mtu hukimbilia kujenga kisima cha maji, kuleta pikipiki, lakini anawadhalilisha watu wake, anawafanya watwana na kuwapuuza kwa kuwa kawanunua kwa kutumia misaada.

Mwenye akili bora angeuliza, Mchungaji hatujakuelewa, tufafanulie ni vipi unayoyasema yawe bora kwa Mtanzania, nami ningemfafanulia. Lakini kwa kuwa ni ujuvi wa hoja za kibabe, basi endeleeni kujijengea wagombea na mazingira yenu muyapendayo ya kuahidi maji, huku mtu hata jhaki yake ya kikatiba haielewi na weye kama mwkilishi huoni umuhimu wa kumpa Mtanzania huyu nguvu yake kikatiba, ki-utu na kumfikisha kwenye uwezo wa kujiamini.
 
Maswali kwa mgombea....ivi sikuizi kwanini wachungaji mmecharukia siasa sana na kulikimbia hekalu....au sadaka haifikii hesabu ile ya per diem? au kondoo wa hekaluni hawatoshi mnaona ni vema kuwafuata na wa mbugani
 
Back
Top Bottom