Bila ya shaka mmeanza kuona pembeni kuna sanduku la Kura. Swali la Msingi ni kuwa Kuendelea na habari binafsi za ngono za viongozi ambazo hazihusishi uvunjaji wa sheria au kuingilia utendaji wao wa kazi hapa JF. Chukua msimamo na kura za wengi basi ndio wapewe na uamuzi wao uheshimiwe. Kwa vile JF ni eneo la demokrasia ambapo panastahili kuwa na heshima yake basi tuamue suala hili kwa kupiga kura na uamuzi wowote wa walio wengi uheshimiwe.
M. M
Mwanakijiji,
Ni kura gani hiyo inaandaliwa utafikiri na ile tume ya uchaguzi ya Saddam?
Huwezi kuja ghafla na kuwaambia wana JF piga kura, wewe ni nani? Ni tume ya uchaguzi? Ni mmiliki wa JF?
Kura ina maana kubwa mno kuliko unavyodhani Mwanakijiji. Demokrasia sio tu maana ya watu kupiga kura, badala yake ni process nzima kuanzia uamuzi wa kupiga kura, utayarishaji wa maswali , njia ya kutumia kura na namna ya kuhesabu hizo kura.
Nafikiri Mwanakijiji ukipewa power utakuwa dikteta mkubwa sana.
Kinachotokea hapa ni kwamba hutaki kukubali kwamba kwenye ile issue ya JK ulifanya makosa na sasa unatafuta kila njia ili uonyeshe ulikuwa right.
Come on brother! Grow up, endelea mbele, maisha sio kung'ang'ania jambo moja mpaka ushinde. Hakuna binadamu anayekuwa right wakati wote, kuna wakati inabidi kukubali kushindwa na ku move on.