Elections 2010 Kama ndivyo fikiri kikwete kampeni za nini?

Jan 16, 2007
721
176
Mgombea wa urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrid Slaa, akilakiwa na wananchi wa mji wa Bunda, alipowasili katika Uwanja wa sabasaba mjini huomo jana, akiwa katika kampeni zake jana. (Picha na Joseph Senga)

Waandishi Wetu

WAKATI kampeni za uchaguzi mkuu zikikaribia kumaliza mwezi mmoja, mashambulizi baina ya wagombea yanazidi kuwa makali baada ya mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Dk Willibrod Slaa kutangaza nia ya kumpandisha kizimbani mke wa rais, huku Jakaya Kikwete wa CCM alirushia makombora wanachama waliokimbilia upinzani.

Kampeni za uchaguzi zilianza rasmi Agosti 21 na kasi yake ilipunguzwa kutokana na mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan, lakini sasa zinazidi kupamba moto baada ya vyama vyote kuanza rasmi kuwania tiketi ya kuingia Ikulu, Bunge la Jamhuri ya Muungano, Baraza la Wawakilishi na kwenye mabaraza ya madiwani.

Dk Slaa, ambaye amekuwa akieleza jinsi mke huyo wa rais, Mama Salma Kikwete anavyotumia mali za serikali kumpigia debe mkewe, jana alikwenda mbali zaidi alipotangaza kuwa atamfungulia mashtaka ya kutumia vibaya mali za umma.

Akihutubia wananchi wa Kibara kwenye Jimbo la Mwibara jana, Dk Slaa, ambaye amebobea kwenye sheria, alisema Chadema inafikiria kumfungulia kesi Mama Kikwete dhidi ya matumizi hayo ya mali za umma.

Dk Slaa aliueleza umati uliokusanyika kwenye mkutano wake huo kuwa katiba ya Jamhuri ya Muungano haimtambui Mama Salma Kikwete kama mfanyakazi wa umma, hivyo hapaswi kutumia mali za umma.

"Mama Kikwete amekuja Musoma kwa kutumia ndege ya serikali yenye namba za serikali 5HTGF kitu ambacho ni kinyume cha makubaliano yaliyopo,'' alidai Dk Slaa.
Alisema tangu kampeni zianze, Mama Kikwete amekuwa akifuja fedha za serikali wakati hana mkataba na umma wa Watanzania.

Kwa mujibu wa Dk Slaa anachofanya mke huyo wa Rais Kikwete ni kama alichofanya mke wa rais wa Zambia kumpigia kampeni mumewe kimakosa na ndiyo maana amefikishwa mahakamani kwa kufanya kosa.

Alisema kuwa bajeti ya Kikwete ya Sh150 bilioni si ya mke wake bali ni za Kikwete mwenyewe kuutumikia umma.

Mama Kikwete ni mwenyekiti wa taasisi ya Wanawake na Maendeleo (Wama) na amekuwa akifanya ziara mikoani kwa muda mrefu, lakini katika siku za karibuni amekuwa akikaririwa na vyombo vya habari akishawishi wananchi wampigie kura mgombea huyo urais wa CCM.

Akiwa mkoani Singida hivi karibuni, Mama Kikwete aliwataka wananchi wawachague wagombea wa CCM kabla ya kuwatambulisha na baadaye kutaja orodha ya ahadi zilizo kwenye ilani ya uchaguzi ya CCM.

Kumekuwepo na kauli mbili tofauti kutetea safari zake mikoani na kujihusisha kwake na kampeni. Ikulu iliwahi kukaririwa ikisema kuwa mke wa rais naye ana fungu lake, wakati CCM ilishakaririwa pia ikisema kuwa safari za Mama Salma zinagharimiwa na chama hicho.

Mbali na Mama Kikwete, Dk Slaa alimtaka Kikwete asipoteze muda kuwadanganya Watanzania kuwa amejenga madarasa wakati elimu bora hakuna na darasa la saba halimsaidii Mtanzania kufika mbali.

"Serikali ya CCM ni wizi mtupu kwa matumizi mabaya ya fedha za serikali,'' alisema Dk Slaa.
Katika hatua nyingine, Mama Kikwete jana alikuwa Mwibara kusuluhisha mgogoro ambao unadaiwa kuwepo baina ya wana-CCM wa jimbo hilo baada ya kuchakachuliwa katika kura za maoni kwa aliyekuwa mbunge wajimbo hilo, Charles Kajege.

Wakati Dk Slaa akielekeza shutuma hizo kwa mke huyo wa rais, mumewe alikuwa akiendelea kuwashukia makadawa chama hicho waliohamia upinzani akisema kuwa wamepotea kwa kuwa wapinzani hawana sera.

Kikwete alisema hayo jana alipokuwa akizungumza kwenye kampeni zake zilizofanyika mji mdogo wa Maramba wilayani Mwibara.

Ingawa Kikwete hakuwataja makada hao walioihama CCM baada ya kura za maoni, baadhi yao ni aliyekuwa mbunge Jimbo la Maswa, John Shibuda na Thomas Nyimbo ambao wote wamehamia Chadema.

Kikwete alisema ni vyema makada hao wangekubali matokeo kuliko kukasirika na kujiunga na vyama vya upinzani.

"Wale waliojiunga na vyama vya upinzani baada ya kura za maoni wamepotea kwa kuwa wamekwenda kusiko na sera, mtandao wala miundo thabiti bali baadhi huibuka tu wakati wa uchaguzi," alisema Kikwete.

Alisema kimsingi hakuna chama kinachofanana na CCM kwa kila kitu ikiwamo muundo, sera, mtandao na hata mpangilio kwani chama hicho kiko kila kona nchini na kinatambulika kwa wananchi.

“Vyama vingine ni vya uchaguzi tu, utaona bendera nyingi wakati huu tena zote mpya, lakini uchaguzi ukipita huoni wanachama wala chama,” alisema Kikwete ambaye aliwataka wagombea wa CCM wasikose usingizi kwa sababu ya wapinzani.

“Unapochukua fomu kuwania uongozi usijiwekee asilimia 100 ya kushinda, bali jione kuwa unaweza kushinda au kushindwa hiyo haitakupa presha ukishindwa,” alisema Kikwete.
Mgombea huyo alisema iwapo atachaguliwa kuwa rais katika kipindi kingine cha miaka mitano, Serikali yake itaanzisha kilimo cha zao la kakao ili kuwawezesha wakulima kujikwamua kiuchumi.

Alisema kwa maeneo ya pwani zao hilo litasaidia kuongeza kipato kwani hivi sasa minazi imeingiliwa na ugonjwa aliouita ukimwi ambao hata hivyo alisema serikali yake ipo katika harakati za kulitafutia ufumbuzi.

Kikwete aliahidi pia kuwa kati ya mwaka 2011 na 2015 vijiji 11 vilivyopo wilayani Mkinga, vitakuwa vimepatiwa maji safi ili kuondokana na tatizo sugu la uhaba wa maji.
Alisema mradi huo utakaogharimu Sh427 milioni utakuwa kuwa mwarobaini wa tatizo la maji wilayani humo.

Akiwa uwanjani hapo, Kikwete aliwanadi wagombea udiwani akiwamo wa Kata ya Maramba, Said ambaye alisoma naye Shule ya Sekondari ya Tanga.

“Huyu Said nilisoma naye Tanga School nikiwa kiranja wake. Naomba mumpe kura ili niendelee kuwa kiranja wake nikiwa Rais wa Jamhuri,” alisema Kikwete na kuomba pia Dastan Kitandula achaguliwe kuwa mbunge wa jimbo la Mkinga.
 
Ni kweli hakuna chama kama CCM maana inajua kuchakachua kura kuanzia udiwani hadi Rais. Pia ni chama chenye ahadi nyingi kuliko utekelezaji. Ni chama ambacho uwezo wa viongoizi wake kufikiri ni mdogo mf. Wilaya ina shule za sekondari 30 na walimu 40. Unategemea nini? Kama kweli hata JK anafikiri vizuri hapo kutakuwa na ubora gani? Ratio is 1:1.3!!!!! Shame.

Ujinga wa watanzania ndio unaoweza kuirudisha CCM madarakani na kuitumbukiza katika matatizo zaidi.
 
Ni kweli kabisa Advocate Jasha,kwa mtaji huo alitakiwa akae tu ikulu asubiri kuapishwa kwa mara nyingine.
 
Back
Top Bottom