Chapa Nalo Jr
JF-Expert Member
- Dec 8, 2010
- 7,515
- 6,489
unamshukuru Mungu kwa kukujulisha siri. baada ya hapo unatafuta amani kwanza na mkeo kisha na huyo mwizi. kumbukeni imeandikwa kuwa "ndoa na iheshimiwe na watu wote na malazi yawe safi", na pia "tafuteni kuwa na amani na watu wote na huo utakatifu ambao hakuna atakayemona Mungu asipokuwa nao". kwa kifupi hakuna haja ya magomvi, hayasaidii kitu. tunapaswa kuushinda ubaya kwa wema
Lakini dada kumbuka hata Paulo katika Biblia(sikumbuki mstari) amekataza watu kuachana ila katika suala la uzinzi hata yeye kigugumizi kilimshika.
Ok, msimamo wangu: Mimi nitamsamehe tu ila sitataka iwe siri kuu, lazima tuitane ndugu kadhaa(wachache tu) wa pande zote wafahamishwe kilichotokea na yeye atubu mbele ya hao ndugu. Lakini kabla ya kuita ndugu nitamuuliza kama bado anapenda kuendelea na mimi au kakolea kwa mgoni wangu, kwani naogopa kusamehe mke ambaye moyoni kumbe hanipendi tena. Baada ya yote nitamfuata mgoni wangu na kutaka fidia ya alichokifanya maana nikimkalia kimya atajiona mshindi ili hata akirudia tena kuwe na record tayari. Mengine yatategemea jinsi hali itakavyokua.