Kama Mwakyembe amelishwa sumu hata Kolimba pia. Matukio yao yanafanana

Malyenge

JF-Expert Member
Jan 16, 2012
6,658
3,646
Wakuu, nimesoma sana issue ya mbunge wa Kyela na naibu wa Wizara ya Ujenzi kuhusu sakata la ugonjwa unaosemekana umetokana na kulishwa sumu.

Nikakumbuka na sakata la katibu mkuu wa CCM Horace Kolimba aliyefariki mwaka 1997 mara tu alipomaliza kuhojiwa juu ya tuhuma alizotoa kwamba "CCM Haina Dira wala Mwelekeo". kauli ambayo ilimgharimu maisha yake mpaka umauti.

Vyombo vya habari wakati huo viliandika sana kuhusu utata wa kifo cha Kolimba mpaka vikahusisha kifo chake kimetokana na "mkono wa ccm". Na ndipo Mwalimu Nyerere aliposimama na kusema kuwa "CCM hakuna wachawi" kifo cha kolimba ni cha kawaida.

Naanza kupata mwanga kwamba yawezekana CCM na serikali ni mafia wakubwa! Ni wauwaji pindi wanapogundua kuna mtu anatishia kuwanyang'anya ulaji.

Namalizia kwa kusema kuwa ikiwa Mwakyembe amelishwa sumu, basi hata Kolimba, Imrani Kombe nao waliuawa na serikali!!!!
 
Back
Top Bottom