Kama mh.zitto kabwe akipewa wizara ya fedha, cdm watakuwa tayari kuunga mkono?

Mbelwa Germano

JF-Expert Member
May 7, 2011
789
289
  1. Kwa kuwa Raisi JK anao uhuru wa kuchagua waziri toka chama cha upinzani (akitaka), na kwa kuwa serikali inaongozwa na sera za CCM chini ya mwamvuli wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo ni kinga ya CCM, na iwapo uteuzi huu utafanyika, je CDM watakuwa tayari kuunga mkono?
  2. Kwa kuwa idadi kubwa ya wabunge wanatoka CCM, Je wabunge hawa wanatuwa tayari kuheshimu maamuzi ya Rais?
  3. Iwapo CDM watakubaliana na uteuzi huu na Wabunge wa CCM kuheshimu maamuzi ya Raisi,lakini wabunge wa CCM wakaamua kumjengea zengwe Mh.Zitto la kumkwamisha katika maazimio ya wizara, Je CDM watakuwa kwenye nafasi salama?
 
Mpaka apewe ndo tutajua hamna haja ya kuumiza kichwa.Wakati wanajua uchafu wao wote utagundulika wakimpa mtu baki.Wakijitahidi sana watatatoa wizara ya michezo.
 
Huyo ananjaa anaweza kusababisha hata serikali ikakopa kwenye maduka ya wahindi, so it better 2kawachagua CCM wenzetu ambao tayari wameshiba...
 
Mpaka apewe ndo tutajua hamna haja ya kuumiza kichwa.Wakati wanajua uchafu wao wote utagundulika wakimpa mtu baki.Wakijitahidi sana watatatoa wizara ya michezo.

NA HAWEZI PEWA HATA IKIFIKA IYO 2015 HAWEZI KWANI MAGWANDA WANAJIFARIJI2 kuchukua dola ila n ndoto za mchana
 
Hata akipewa CDM hawawezi kukubali, wataendeleza mapambano mpaka kieleweke.

Kupewa uwaziri halafu waje wamuundie kashfa ili mfurahi hilo halipo.
 
mi ntaunga mkono hoja pia na lema kupewa wizara ya ulinzi,tundu lisu wizara ya katiba na sheria pamoja na dr slaa kuwa naibu waziri mkuu,mana kwa sasa tuna waziri mkuu asiye waziri mkuu anayeshindwa kumdhibiti mkuu wa inchi mtoro-jen.ulimwengu 2012
 
  1. Kwa kuwa Raisi JK anao uhuru wa kuchagua waziri toka chama cha upinzani (akitaka), na kwa kuwa serikali inaongozwa na sera za CCM chini ya mwamvuli wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo ni kinga ya CCM, na iwapo uteuzi huu utafanyika, je CDM watakuwa tayari kuunga mkono?
  2. Kwa kuwa idadi kubwa ya wabunge wanatoka CCM, Je wabunge hawa wanatuwa tayari kuheshimu maamuzi ya Rais?
  3. Iwapo CDM watakubaliana na uteuzi huu na Wabunge wa CCM kuheshimu maamuzi ya Raisi,lakini wabunge wa CCM wakaamua kumjengea zengwe Mh.Zitto la kumkwamisha katika maazimio ya wizara, Je CDM watakuwa kwenye nafasi salama?

Ndoto za mchana hizo. kama ameshindwa kubadili mawaziri bila kibali cha CC CCM, unategemea atatangaza mabadiliko bila CC CCM kuridhia? AU unataka kusema CCM imeishiwa watu kiasi cha kuazima kwa vyama pinzani?

Mkuu forget that will never happen.

Hata ikitokea hivyo maanake ni kuwa atapoteza nyazifa zote alizonazo bungeni, kitu ambacho sioni kama CDM na Zitto wanaweza kuwa tayari kwa hilo.
 
Hatutegemei kitu kama hichi, lengo letu ni CCM waondoke kwenye hizi anga za siasa Tanzania na si kuwasaidia.

Hakuna pango wa kushirikiana na CCM
 
Back
Top Bottom