Kama mgambo wa jiji kumkamata Osama!

Magehema

JF-Expert Member
Aug 11, 2008
428
27
Ilikuwa jumamosi, mbili nane mwezi mei,
Siku ilojaa mikosi, kwa Man U nae Fegi,
Waliuanza kwa kasi, wakitafuta ushindi,
Dakika kumi za kwanza, Barca walikuwa hoi.

Runi alikosa goli, wanazi wakatapika,
Messi kapoteza boli, wakaanza kupayuka,
Wakaanza utabili, leo Barca twawazika
Dakika kumi za mwanzo Barca walikuwa hoi.

Mpira anao Xavi, kapiga chenga ya kwanza,
Katoa pasi kwa Messi, Mara Villa kawakosa,
Kapotezwa babu gigsi, kiungo wanacho Barca
Man U wapotea, mpira hawauoni.

Xavi ni bonge la mido, wembley anatamba,
Simuoni chicharito, wala paki kujigamba,
Wanafukuza upepo, Barca wazidi jipanga,
Mani U wapotea, mpira hawauoni.

Nimeishiwa maneno, kwa move ya goli lao
Xavi mtu wa matendo, kinara mipango yao
Ni pasi ya kilatino, alowaua ni Leo,
Mani U wapo nyuma, Barca goli moja mbele.

Mido kapewa kariki, baadae kaja Nani,
Usimsahau paki, naye alikuwa ndani,
Kupambana nae Messi, Iniesta nae Xavi,
Kama mgambo wa jiji, kumtafuta Osama

Embu acheni utani, tuzungumze ukweli,
Mlitegemea nini, au nguvu na misuli,
Wale sio evatoni, huwawezi kwa akili,
Kama mgambo wa jiji, kumtafuta Osama





 

Similar Discussions

Back
Top Bottom