Kubwajinga
JF-Expert Member
- Jan 23, 2008
- 2,194
- 297
Mugabe Robert ana degree za kusoma kama nne hivi, na kapewa za bure tu kama sita vile kwa hiyo anazo za kutosha, lakini Uchumi wa Zimbabwe ndio tunaousoma wa quadrillion kununua sijui mkate au embe.
Bila kusahau mafisadi wengi wa Tanzania waliosoma Havard kwa pesa ya walipa kodi Mramba, nk. Lakini wapi? Kwa hiyo basi elimu ndio ufunguo wa maisha lakini sio elimu ya degree tu. Elimu iko kwa namna mbali mbali sio elimu ya kikasumba tu.
Suala la kuanguka kwa uchumi wa Zimbabwe sio la shule, ni la kisiasa. Kama Mugabe angekuwa ameishia form six kama muungwana Mbowe, angeweza kufanya kama ya Iddi Amini; kuendesha kama nyumba ndogo na kuiingiza vitani bila kujua ubavu wake. Lakini Mugabe bahati yake shule yake imemsaidia akaweza kung'ang'ania katika mazingira magumu kwe milongo kadhaa sasa.
La muhimu ni kutambua umuhimu wa shule katika nyakati zote, iwe neema ya Mauritius, au vikwazo vya Zimbabwe, na kuacha kung'ang'ania waliokimbia umande ingawa wana midomo mikubwa, Mbowe, Amini n.k.
Shule ni baba wa maendeleo, wanaoharibu nchi hawafanyi hivyo kwa sababu ya ukubwa wa shule bali kwa uchu na uzembe wao binafsi.