Kama kweli Wazanzibari "wengi" wanataka watoke kwenye Muungano mbona ni rahisi sana...

Kuna njia. Nyingi tu za kuvunja huo Muungano za Kistaarabu zinaweza fatwa kama kweli Zanzibar Hawatak Muungano ...Lakini sio Kihuni-huni kama ivi...
Jasirii aachi Asili

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
do you think, inawezekana? Kuna tatizo lingine nalo ni faida ya magamba kwa wabunge wa bure toka Zenj! Hawawezi kukubali
Kwani hao wabunge wa Zenji sio wazanzibar? Na mbona wote wako kimya wakati ushenzi huu ukiendelea? Nashauri Waliozanzibar waprint huu uchauri wa Mwanakijiji na kuusambaza misikiti yote Zanzibar, sababu naona uko pekee ndio kuna watu wanafikiria.
 
Kwa nini unafikiri swala la muungano na Zanzibar linatakiwa kupigiwa kura na Wazanzibari tu?

Hufikiri kwamba kuna uwezekanao Wazanzibari wengi wakasema wanataka kuwa katika muungano, ila watu wa bara wakawa hawataki muungano?

Ili kura ya maoni iwe na maana, inafaa ipigwe nchi nzima. Usichukulie for granted kwamba wabara wanautaka muungano.

Unaweza kumaliza kura ya maoni Zanzibar bila ya kuwashirikisha watu wa bara, ukapata kura za kukubali muungano nyingi sana, only to find out kuna malalamiko kutoka kwa watu wa bara kwamba hawakushirikishwa.
Mkuu Kiranga, sisi bara hatuna sheria ya kura ya maoni. Zanzibar tayari wanayo sheria ya kura ya maoni hivyo kwao ni straight forward.

Hapa kwetu pia sheria hiyo italetwa baada ya kukusanywa maoni na bunge la katiba, then kura ya maoni itakuwa ndio last option kuipitisha katiba mpya!.

Hoja ya Mwanakijiji ni very valid, maadam wamethibitisha kwa saini 500, 000 ambayo ni theluthi moja, na wanaamini Wazanzibari wengi hawautaki muungano, kwa nini wasiupinge kwa kuitumia hiyo sheria yao ya kura ya maoni na matokeo kuwa endorsed na BLW hiyo kutoa tuu azimio la utekelezaji huku bara!.

Kama walibadili katiba yao kuunda SUK ikiwemo kuvunja cheo cha Waziri Kiongozi na badala yake kuweka hao makamo wawili, katiba ya JMT haiyatambui mabadiliko hayo. Kwa mujibu wa katiba ya JMT bado tunamtambua Waziri kiongozi ambaye hayupo na hatuwatambui hao makamo wawili kikatiba ila in reality wapo na huja huku bara na protocal inawatambua.

NB. Nazidi kusisitiza japo muungano ni illegal before the eyes of the law kwa vile haukuwa ratified na BLW au BLM kwama ilivyotaka sheria, Wanzanzibar wanayo very valid reasons ya kujitoa kwa heshima, tena kihalali bila jinai ya uhaini kwa kuvunja muungano, wakiamua kwa kauli moja kuwa kabla ya BLW kuridhia tume yakukusanya maoni ya katiba mpya ifanye kazi Zanzibar, kwanza vile vipengele vya yale makubaliano ya muungano ambavyo vilikiukwa kwanza viridhiwe na BLW ili kuulegitimize huu muungano kule kwao Zanzibar!. Na kwa kuutumia mwanya huo then wagome kuuratify muungano hivyo muungano huu kuwa rendered illegal na legal process za kuuvunja kufuata!.

Kwa vile Karume hakujua Kiingereza, I wala hakujua kusoma wala kuandika zaidi ya kusaini kwa dole gumba, then washeria pia wanaweza kuchalenge makubaliano before the court of law kwa kutumia kipengele kiitwacho "privity" kwa kujenga hoja kuwa wakati Karume ikitia dole gumba, hakujua anasaini nini!.

Baba wa Taifa aliundesha muungano kwa utaratibu wa "the end justifies the means". sheria, taratibu na kanuni, hazikufuatwa!.
 
Kwanini unaamini kuwa wasioutaka muungano ni wachache?
Kuna mawili
Kwanza: wangekuwa wengi wangefanya kama walivyofanya kwenye serikali ya umoja wa kitaifa.
Pili: Kama ni wengi basi watakuwa ni wale wasiokuwa na nguvu.

Au la, kwa moyo mkunjufu kabisa na mimi naunga mkono hoja, wafanye kama jadi yao
 
Kwani wajameni, haiwezekani by 1st of July mwaka 2012 Muungano ikawa imevunjika?

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Kwanini unaamini kuwa wasioutaka muungano ni wachache?

Ni sawa na wewe unavyotaka tuamini kuwa wengi hawautaki. Mzee Mwanakijiji hajasema wengi hawautaki (na hili ndio tatizo lenu: kutopenda kusikiliza) alichosema ni kuwa jambo hili halina uhakika na njia pekee ya kupata uhakika ni kwa A au B voting.

Ama kama unaquote namna aliyoandika, bado yupo sahihi. Idadi ya wanaopiga kelele majukwaani ni ndogo kulinganisha na idadi ya walionyamaza ambao hatujui wanasema nini
 
Hapa waZ'bar nina uhakika hawataki kuvunja muungano, wangetaka hivyo wawakilishi wa waZ'bar ambao wamewatuma kwenye Bunge la muungano wasingemzomea TS alipowaonyesha njia muafaka kabisa! Kinacho wasumbua ni UROHO Huku Z'bar wanaitaka iwe yao tu bila Tanganyika, na neema ya Tanganyika wanaitaka bila kuwekewa masharti! Fanyeni hivyo kama mtasikia kelele zao!
 
aaaaaaah....
unadhani itaishia hapo??
sisi tutapiga kura nyingine kuomba COASTAL STRIP ya 16 miles tujiunge na new ZANZIBAR REPUBLICS....
ina maana miji yaTANGA, MTWARA, BAGAMOYO NA DSM....tutajiunga mso tuuu

HAPO ITAKUWA NCHI IMETENGAMAA, kama sudan , waislam na bara ya wakristu...

JE MZEE MWANAKIJIJI KUNA K2 UMEJIFUNZA HAPA?????

Kabla hizi ILLUSIONS zako hazijatokea, Unguja na Pemba zitakuwa zimeshatengana. Kutapatikana Watumbatu na Washirazi watakaolumbana juu ya nani ana haki ya kuitawala Jamhuri ya Zanzibar.

Labda ujiunge na Jamhuri ya Watu wa Kojani.
 
aaaaaaah....
unadhani itaishia hapo??
sisi tutapiga kura nyingine kuomba COASTAL STRIP ya 16 miles tujiunge na new ZANZIBAR REPUBLICS....
ina maana miji yaTANGA, MTWARA, BAGAMOYO NA DSM....tutajiunga mso tuuu

HAPO ITAKUWA NCHI IMETENGAMAA, kama sudan , waislam na bara ya wakristu...

JE MZEE MWANAKIJIJI KUNA K2 UMEJIFUNZA HAPA?????
Aiseee umenikosha roho yangu wewe! yaani umenifanya niazne kuota mchanamchana
 
1. Bila ya kupiga kura ya maoni nchi nzima huwezi kujua wabara wanautaka muungano au hawautaki. Kwamba wamelalamika au hawajalalamika hapo nyuma is irrelevant.Usipowashirikisha unaacha mwanya wa mzozo ambao unaweza kuzibwa kirahisi tangu mwanzo. Ukitaka kuondoa feelings za kwamba muungano uko one sided itabidi kura ipigwe pande mbili zote.

2. Mfano wa Quebec hata mimi niliufikiria.Lakini haupo appropriate hapa kwa sababu Quebec ni jimbo la Canada lililokuwa linaamua kwamba libaki Canada au lijitoe. Zanzibar si jimbo la Tanzania, ni a quasi-state within a state.

3. Ukipiga kura ya maoni nchi nzima, Zanzibar wakasema wanataka Muungano, bara wakasema hawataki, muungano unavunjwa.Point ya kupiga kura ya maoni nchi nzima ni kupata maoni ya wananchi wa nchi nzima, kwa maana muungano unawahusu wananchi wa nchi nzima, si Wazanzibari tu.Huwezi kuita hii situation stalemate. Stalemate itatokea iwapo kura za maoni zitakataa na kukubali muungano kwa 50% kote bara na visiwani. Kitakachotakiwa kuendeleza muungano kiwe simple majority on both sides.

Moja ya matatizo tunayoyaona katika muungano wetu sasa hivi ni hii habari ya kufanya mambo nusunusu au juu juu. Kama kuupitisha muungano kibungebunge bila a thorough process iliyowahusisha wananchi wote directly.

Sasa tushaona hili ni tatizo.Tunatakiwa tujifunze. Tusitake kurudia makosa kwa kufanya swala la muungano liamuliwe na upande mmoja tu wa muungano.

Tutawapa msemo watu wa bara wanaosema Wazanzibari wanapendelewa.
waznz ndio walalamikaji katika muungano huu,hakuna haja ya kupoteza pesa kupiga kura nchi nzima, kama hao waznz wakisema wanautaka basi utaendelea na waache chokochoko,kama wao hawautaki utavunjika,hiyo haina hata haja ya kuwauliza wabara maana wautake wasiutake kama waznz wameukataa utavunjikaa tu na wao tu wanatosha.
 
Utajuaje Wazanzibari ndio walalamikaji bila kuomba maoni ya watu wa bara? If JF is any indication kuna watu wa bara wengi tu hawaupendi muungano pia.

At least katika mfumo wake wa sasa.
 
Mkuu Kiranga, sisi bara hatuna sheria ya kura ya maoni. Zanzibar tayari wanayo sheria ya kura ya maoni hivyo kwao ni straight forward.

Hapa kwetu pia sheria hiyo italetwa baada ya kukusanywa maoni na bunge la katiba, then kura ya maoni itakuwa ndio last option kuipitisha katiba mpya!.

Hoja ya Mwanakijiji ni very valid, maadam wamethibitisha kwa saini 500, 000 ambayo ni theluthi moja, na wanaamini Wazanzibari wengi hawautaki muungano, kwa nini wasiupinge kwa kuitumia hiyo sheria yao ya kura ya maoni na matokeo kuwa endorsed na BLW hiyo kutoa tuu azimio la utekelezaji huku bara!.

Kama walibadili katiba yao kuunda SUK ikiwemo kuvunja cheo cha Waziri Kiongozi na badala yake kuweka hao makamo wawili, katiba ya JMT haiyatambui mabadiliko hayo. Kwa mujibu wa katiba ya JMT bado tunamtambua Waziri kiongozi ambaye hayupo na hatuwatambui hao makamo wawili kikatiba ila in reality wapo na huja huku bara na protocal inawatambua.

NB. Nazidi kusisitiza japo muungano ni illegal before the eyes of the law kwa vile haukuwa ratified na BLW au BLM kwama ilivyotaka sheria, Wanzanzibar wanayo very valid reasons ya kujitoa kwa heshima, tena kihalali bila jinai ya uhaini kwa kuvunja muungano, wakiamua kwa kauli moja kuwa kabla ya BLW kuridhia tume yakukusanya maoni ya katiba mpya ifanye kazi Zanzibar, kwanza vile vipengele vya yale makubaliano ya muungano ambavyo vilikiukwa kwanza viridhiwe na BLW ili kuulegitimize huu muungano kule kwao Zanzibar!. Na kwa kuutumia mwanya huo then wagome kuuratify muungano hivyo muungano huu kuwa rendered illegal na legal process za kuuvunja kufuata!.

Kwa vile Karume hakujua Kiingereza, I wala hakujua kusoma wala kuandika zaidi ya kusaini kwa dole gumba, then washeria pia wanaweza kuchalenge makubaliano before the court of law kwa kutumia kipengele kiitwacho "privity" kwa kujenga hoja kuwa wakati Karume ikitia dole gumba, hakujua anasaini nini!.

Baba wa Taifa aliundesha muungano kwa utaratibu wa "the end justifies the means". sheria, taratibu na kanuni, hazikufuatwa!.

Inaonekana hapa Bunge la Tanganyika lili ratify, lakini hakuna document yoyote ya ku ratify muungano kutoka Zanzibar

http://www.zanzinet.org/files/legality_union.pdf pp 30/31

One can make an argument kwamba muungano hauhitaji kura ya maoni bara kwa sababu ulishakuwa ratified na bunge la Tanganyika. Although the best ratification would have been involving the people directly.

One can also make an argument that so much has changed since then it deserves an fresh, all encompassing, all inclusive second look.

Muungano ukipigiwa kura ya maoni pande zote ndipo tutapata jibu la kudumu.
 
Mwanakijiji kwa idadi ya watu umepotosha kidogo. Kama Zanzibar inawatu 1.5 million wenye haki ya kupiga kura ni wangapi? unataka kuniambia kuwa wote hao 1.5 million ni wapiga kura? Kama sio wote wapiga kura, sahihi za watu 500,000 ni asilimia ngapi ya wapiga kura wote. Na ukishapata % ndipo utuambia kuwa ni wachache au ni wengi
 
Kwa mazingira yapi tuaweza kuachiwa kufanyi hivi mwanakjj anavyoshuari! Wao walishapiga mstari kuwa kuhusu muungano hakuna kitakachobadilika zaidi ya ulivyo labda kutolewe mawazo ya kuuboresha! sasa unafikiri watatuacha tuuvuke mstari waliokwisha upiga!
Busara ni kufanya jambo kwa wakati sahihi na sehemu sahihi! busara yako mwanakjj haina msaada kwetu sisi kwa wakati huu!
 
Ningependa kujua TOR watakazotumia tume ya katiba kama zitakua zimelizungumziaje swala la mjadala wa uwepo/kutokuwepo kwa muungano...maana kama sikosei wakati wa kuikabidhi kazi tume rais alisema swala la uwepo/kutokuwepo muungano halina mjadala...Sasa baada ya hizi vurugu zenj nimeanza kusikia rhetorics toka kwa hawa marais wa pande zote...Jk na dr.Shein ...kuwa hili suala lijadiliwe kwenye tume ya katiba..Swali langu ni je..tume ya katiba wataliingiza kwenye TOR zao swala la uwepo/kutokuwepo kwa muungano?????..maana kwa mazoea hapa TZ..ni rahisi sana kwa viongozi kusema mambo...lakini utekelezaji huwa hamna....Navyojua swala la muundo wa serikali litakuwepo kwenye TOR za tume ya katiba...Ni jambo la msingi sana kwa sasa....wakati wa fujo hizi za zenj..hawa tume ya katiba wachukue kila kitu kinacholalamikiwa na wazanzibari sasa hivi wakiingize kwenye TOR zao ili wapate maoni ya wazanzibari wote ...na itakapofika wakati wa ile final kura ya maoni ya katiba kwa nchi nzima(referendum) hili jambo nalo lipigiwe kura.......yaani kiwepo kipengele pekee kitakachohusisha kura ya uwepo/kutokuwepo kwa muungano.....maana sioni njia ya haraka tuliyo nayo kama nchi ya jinsi ya kushughulikia hii issue.....maana hawa jamaa wazenj naona wamefanya nao timing wakati huu kabla tume haijaanza kazi ili hili swala lishughulikiwe kipekee.......nadhani this is the time to do it.....
 
Kuna maneno na kauli za baadhi ya watu wachache wakizungumza kana kwamba wanawakilisha "wengi". Utasikia mtu anayepinga Muungano anasema "Wazanzibari hatuutaki Muungano" na wakati mwingine kudai "Wazanzibari wengi hawautaki muungano". Sasa mara nyingi wanaposema "wengi" mtu wa kawaida (asiyetaka kufikiri sana) anaweza kuamini kabisa kuwa ni kweli "wengi" hawautaki Muungano.

Mfano unaotolewa siku za hivi karibuni ni "sahihi 500,000" za wanaodaiwa "Wazanzibari" wasiotaka Muungano. Sasa kwenye mahali ambapo pana watu milioni 1.5 hivi idadi hiyo ni kubwa sana; ni theluthi moja ya watu wote wa Zanzibar. Sasa kama kweli wapo watu wengi hivi njia rahisi ya kutaka kujitoa kutoka kwenye Muungano siyo mihadhara wala hawahitaji kabisa kuwalalamikia watu wa bara au serikali ya Muungano.

Kwa wanaokumbuka wananchi wa Zanzibar walishinikiza vyama vyao viwili vya CCM na CUF kuunda serikali ya umoja wa kitaifa na waliweza kufanya hivyo baada ya kupitisha sheria ya kura ya maoni ambayo hatimaye iliandika upya katiba ya Zanzibar. Wananchi wakaweza kujitokeza na kupiga kura ya maoni. Walifanya hivi bila kuomba kibali Muungano na kiasi cha kuweza kuandika kwenye Katiba Yao vitu ambavyo ni kinyume na Katiba ya Muungano.

Sasa kama waliweza kufanya hili ni kitu gani kinawashinda kutaka viongozi wao wa kisiasa kuandia sheria ya kupiga kura ya maoni kama wanautaka Muungano au la? Kwa vile hoja ya kupinga MUungano inadaiwa inakubaliwa na watu wa vyama vyote ni wazi kuwa ni rahisi sana kwa watu wa Uamsho na Wazanzibari wengine kuhakikisha kuwa BLW linapokaa linaazimia kupitisha kura ya maoni kuhusu Muungano na kutaka sheria iletwe ya kuuliza swali la Muungano.

Swali liwe rahisi tu:

Je unataka Zanzibar ibakie kwenye Muungano wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania?

a. Ndio ibakie - Ikibakia kero na matatizo ya Muungano kutatuliwa ifikapo Julai 1, 2014
b. Hapana isibakie - isipobakia Zanzibar itajitoa ifikapo Julai 1, 2014

Ijulikane mapema kuwa ikisemwa kuwa "ndio ibakie" manake ni kuwa masuala ya muundo na mfumo wa Muungano yatajadiiliwa na kushughulikiwa kwenye Katiba Mpya na yatakuwa tayari kumalizwa yote ifikapo 2014

Na ikisemwa Hapana isibakie manae ni kuwa mazungumzo ya kuvunja Muungano yataanza na ifikapo Julai 1, 2014 Zanzibar itajitoa kwenye Muungano.

Wazanzibar waandae kura hiyo ya maoni wao wenyewe kama walivyofanya kwenye ile ya mabadiliko ya Katiba na lolote watakaloamua Tanzania Bara WATAHESHIMU uamuzi huo.

Ni rahisi sana kumaliza hoja ya Muungano au kutokuwepo Muungano. Yote YAMO MIKONONI MWA WAZANZIBARI. Hawahitaji kutuambia hawautaki Muungano, hatuhitaji watuambie tunawakandamiza kama wanataka kutoka kweli na siyo mikwara mbuzi njia nyeupeeeee!!! Andikeni sheria, itisheni kura ya maoni, pigeni kuchagua 'b' and then mambo yatakua yameiva ifikapo 2014 tutawasaidia kufunga mizigo.

Nyinyi Watanganyika ndio msioruhusu kuitishwa kwa kura hiyo kwani huyu Raisi wenu Kikwete hata anapinga Muungano usijadiliwe katika katiba hiyo mpya. Vingine hawa viongozi wetu wa Zanzibar wote wanaogopa kuitisha kura hiyo ya maoni kwani wote ni vibaraka wa vyama vyao ambavyo vyote viko mikononi kwa Watanganyika. Usidanganyike kura hile ya maoni ilifanyika kwa ruhusa ya CCM na mataifa makubwa ya nje waliotaka Zanzibar kuwe na usalama. Hapo awali Rais Aboud Jumbe alipoonesha tuu kwamba anataka kuwe na serikali tatu, mara moja aliitwa Dodoma na kufukuzwa kazi. Zanzibar tunataka uhuru wetu na hii katiba mpya tutaikubali iwapo muungano utakuwa kama hule wa mfumo wa nchi za ulaya magharibi vinginevyo sote wazanzibari tutaukataa mpaka milele. Angalia watu waliojitokeza kupinga muungano, wengi wao ni vijana hii inaonyesha tatizo hili litaendelea kwa muda mrefu sana mpaka zanzibar iwe huru.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom