Awali ya yote nakuomba radhi kwa kukosea kuliandika jina lako vilivyo. Si makusudi yangu kufanya hivyo bali ni vidole vilinipuruchuka kidogo badala kuandika D vikaweka G. Lakin nakuheshimu sana na kuliheshimu sana jina lako na michango yote humu barzani. Nakuomba radhi sana Mkandara.
Naomba nikujuze kuna Muungano wa KATIBA na wa MKATABA.
Tanganyika na Znz zimeungana KIMKATABA na hata Katiba yenu ya Muungano na hata ile ya Znz imelibainisha hilo. Kwa manaa nyingine Katiba zenu zote zinaongozwa na yale mliokubaliana tu katika muungano wenu na hilo limepelekea kila nchi kuwa na Katiba yake , Japo Tanganyika imehodhi na kuchukua madaraka kwenye muungano na yale ya Tanganyika.
Mengi nimebainisha kwenye bandiko hapo juu kuhusu mambo mlioungana.
Barubaru,
..unadai muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni wa mkataba.
..wenzako wa Zanzinet nao wanasema wanataka kutoka ktk muungano huu tulionao sasa hivi na kuwa na "muungano wa mkataba."
..sasa sisi wa-Tanganyika tuelewe vipi??