Kama kweli Wazanzibari "wengi" wanataka watoke kwenye Muungano mbona ni rahisi sana...

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,476
39,995
Kuna maneno na kauli za baadhi ya watu wachache wakizungumza kana kwamba wanawakilisha "wengi". Utasikia mtu anayepinga Muungano anasema "Wazanzibari hatuutaki Muungano" na wakati mwingine kudai "Wazanzibari wengi hawautaki muungano". Sasa mara nyingi wanaposema "wengi" mtu wa kawaida (asiyetaka kufikiri sana) anaweza kuamini kabisa kuwa ni kweli "wengi" hawautaki Muungano.

Mfano unaotolewa siku za hivi karibuni ni "sahihi 500,000" za wanaodaiwa "Wazanzibari" wasiotaka Muungano. Sasa kwenye mahali ambapo pana watu milioni 1.5 hivi idadi hiyo ni kubwa sana; ni theluthi moja ya watu wote wa Zanzibar. Sasa kama kweli wapo watu wengi hivi njia rahisi ya kutaka kujitoa kutoka kwenye Muungano siyo mihadhara wala hawahitaji kabisa kuwalalamikia watu wa bara au serikali ya Muungano.

Kwa wanaokumbuka wananchi wa Zanzibar walishinikiza vyama vyao viwili vya CCM na CUF kuunda serikali ya umoja wa kitaifa na waliweza kufanya hivyo baada ya kupitisha sheria ya kura ya maoni ambayo hatimaye iliandika upya katiba ya Zanzibar. Wananchi wakaweza kujitokeza na kupiga kura ya maoni. Walifanya hivi bila kuomba kibali Muungano na kiasi cha kuweza kuandika kwenye Katiba Yao vitu ambavyo ni kinyume na Katiba ya Muungano.

Sasa kama waliweza kufanya hili ni kitu gani kinawashinda kutaka viongozi wao wa kisiasa kuandia sheria ya kupiga kura ya maoni kama wanautaka Muungano au la? Kwa vile hoja ya kupinga MUungano inadaiwa inakubaliwa na watu wa vyama vyote ni wazi kuwa ni rahisi sana kwa watu wa Uamsho na Wazanzibari wengine kuhakikisha kuwa BLW linapokaa linaazimia kupitisha kura ya maoni kuhusu Muungano na kutaka sheria iletwe ya kuuliza swali la Muungano.

Swali liwe rahisi tu:

Je unataka Zanzibar ibakie kwenye Muungano wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania?

a. Ndio ibakie - Ikibakia kero na matatizo ya Muungano kutatuliwa ifikapo Julai 1, 2014
b. Hapana isibakie - isipobakia Zanzibar itajitoa ifikapo Julai 1, 2014

Ijulikane mapema kuwa ikisemwa kuwa "ndio ibakie" manake ni kuwa masuala ya muundo na mfumo wa Muungano yatajadiiliwa na kushughulikiwa kwenye Katiba Mpya na yatakuwa tayari kumalizwa yote ifikapo 2014

Na ikisemwa Hapana isibakie manae ni kuwa mazungumzo ya kuvunja Muungano yataanza na ifikapo Julai 1, 2014 Zanzibar itajitoa kwenye Muungano.

Wazanzibar waandae kura hiyo ya maoni wao wenyewe kama walivyofanya kwenye ile ya mabadiliko ya Katiba na lolote watakaloamua Tanzania Bara WATAHESHIMU uamuzi huo.

Ni rahisi sana kumaliza hoja ya Muungano au kutokuwepo Muungano. Yote YAMO MIKONONI MWA WAZANZIBARI. Hawahitaji kutuambia hawautaki Muungano, hatuhitaji watuambie tunawakandamiza kama wanataka kutoka kweli na siyo mikwara mbuzi njia nyeupeeeee!!! Andikeni sheria, itisheni kura ya maoni, pigeni kuchagua 'b' and then mambo yatakua yameiva ifikapo 2014 tutawasaidia kufunga mizigo.
 
2014? Naona ni mbali sana, labda ingekuwa December 2012 kila mtu ajue ustaarab wake.

Waliomba chama chao cha mpira, wakaweza kupata bila muungano
Wimbo wa Taifa, Bendera, na wakabadilisha katiba hata mambo yanayohusu muungano, hakuna anayewakataza

Ilikuwa ni kuamua tu, wabunge wao wasiende Dodoma, wajumbe wa tume wajitoe, Makamu wa Rais anayechaguliwa kwa kigezo cha Uzanzibar ajiuzulu, mawaziri wa muungano wajiuzulu, wafanyakazi katika taasisi za bara waache kazi.
By July 1 wangeshakuwa na Zanzibar ya neema! I wish they could pack and go ASAP
 
Binafsi naomba sana hawa wanauamsho wafanikiwe kuitoa zanzibar yao kwenye huu muungano 'fake' ili Tanganyika yetu iwe huru kwa mara nyingine tena!
 
2014? Naona ni mbali sana, labda ingekuwa December 2012 kila mtu ajue ustaarab wake.

Waliomba chama chao cha mpira, wakaweza kupata bila muungano
Wimbo wa Taifa, Bendera, na wakabadilisha katiba hata mambo yanayohusu muungano, hakuna anayewakataza

Ilikuwa ni kuamua tu, wabunge wao wasiende Dodoma, wajumbe wa tume wajitoe, Makamu wa Rais anayechaguliwa kwa kigezo cha Uzanzibar ajiuzulu, mawaziri wa muungano wajiuzulu, wafanyakazi katika taasisi za bara waache kazi.
By July 1 wangeshakuwa na Zanzibar ya neema! I wish they could pack and go ASAP

Nguruvi, I was being a little bit generous. Mwenyewe nilikuwa nafikiria ifikapo 9 December 2012 tuwe tumelimaliza hili suala.... CCM imeshindwa kuepusha hatima iliyo wazi na kuichelewesha zaidi ni matatizo yasiyio ya lazima. Binafsi ningependa Wazanzibari waamue tu mapema zaidi...
 
Mkuu Mzee Mwanakijiji, nimekupata vizuri na nimekuelewa!.

Ama kweli mdharau mwiba, mguu huota tende!.

Kila nikilisemea hili mwishowe nitakuja kuonekana sisi ndio wale wale tusiolitakia mema taifa hili!.

Zanzibar walipopitisha yale mabadiliko ya katiba tulisema humu humu sheria kuu ya JMT ni Katiba ya JMT na sheria yoyote inayo kinzana na katiba ya JMT, then katiba ya JMT ndio ita prevail. Yale mabadiliko ya Katiba ya Zanzibar yanakwenda kinyume cha katiba ya JMT, lakini kwa vile serikali yetu ni lege lege, wamedharau mwiba, sasa na tusubiri mguu uote tende!.

Viongozi waliopo madarakani, wanakijua kilichomkuta Aboud Jumbe, hakuna wa kuthubutu kufuata ushauri wa Mzee Mwanakijiji unless hawajipendi!.

Pasco.
Zanzibar walipopitisha ile sheria ya kura ya maoni, nilikuwepo BLW na niliposti humu humu kuwa kupitishwa kwa sheria hiyo kunaweza kupelekea kufunguliwa kwa pandora box na kuitumia kuuhoji muungano!. Nitaisaka ile posti!.
 
do you think, inawezekana? Kuna tatizo lingine nalo ni faida ya magamba kwa wabunge wa bure toka Zenj! Hawawezi kukubali
 
Kwa nini unafikiri swala la muungano na Zanzibar linatakiwa kupigiwa kura na Wazanzibari tu?

Hufikiri kwamba kuna uwezekanao Wazanzibari wengi wakasema wanataka kuwa katika muungano, ila watu wa bara wakawa hawataki muungano?

Ili kura ya maoni iwe na maana, inafaa ipigwe nchi nzima. Usichukulie for granted kwamba wabara wanautaka muungano.

Unaweza kumaliza kura ya maoni Zanzibar bila ya kuwashirikisha watu wa bara, ukapata kura za kukubali muungano nyingi sana, only to find out kuna malalamiko kutoka kwa watu wa bara kwamba hawakushirikishwa.
 
Kiranga; wabara hawajawahi kuulalamikia Muungano kwa miaka mingi sana utaona wanacholalamikia sana na hili ni recent phenomenon ni Wazanzibari wanaolalamikia Muungano. Lakini la zaidi ni kuwa kuwauliza watu wa bara siyo sawa kwa sababu sisi hatujisikii kuwa annexed na Zanzibar au kukandamizwa na Zanzibar. Ndio maana Sudan haikupigwa kura ya maoni ya Sudan nzima bali watu wa Kusini tu; hata Quebec haikupigwa ya Canada nzima bali ni Quebec. Sababu ni nyepesi... tukipiga kura ya maoni ya nchi nzima na Bara wakasema wanataka Muungano na Zanzibar wanasema hawataki mnaamuaje stalemate hiyo?

La msingi ni kuwapa Zanzibar absolute freedom ya kuendesha kura yao ya maoni bila influence ya bara whatsoever. Watakachoamua bara will be fine either way. Lakini bara tukiamua Zanzibar haiwezi kuwa fine kwa namna yoyote.
 
Swali liwe rahisi tu:

Je unataka Zanzibar ibakie kwenye Muungano wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania?

a. Ndio ibakie - Ikibakia kero na matatizo ya Muungano kutatuliwa ifikapo Julai 1, 2014
b. Hapana isibakie - isipobakia Zanzibar itajitoa ifikapo Julai 1, 2014

MM mimi nichangie kwenye Swali la kura ya maoni. Ili kuwafanya hata wale wenye mashakamashaka kujiridhisha kuwa kuna kitu cha muhimu kitafanyika napendekeza mabadiliko kidogo. Ili kuyapa kipaumbele matatizo ya muungano na kuwafanya viongozi waoga wa kuvunjika kwa muungano kuwa serious.

Je unataka Zanzibar ibakie kwenye Muungano wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania?

(a). Ndio ibakie - Ikibakia kero na matatizo ya Muungano yawe yametatuliwa ifikapo July1, 2014. Isipowezekana Jibu litakuwa ni la (b) chini

(b). Hapana isibakie - Zanzibar itajitoa itakapofika October 31, 2014
 
2014? Naona ni mbali sana, labda ingekuwa December 2012 kila mtu ajue ustaarab wake.

Waliomba chama chao cha mpira, wakaweza kupata bila muungano
Wimbo wa Taifa, Bendera, na wakabadilisha katiba hata mambo yanayohusu muungano, hakuna anayewakataza

Ilikuwa ni kuamua tu, wabunge wao wasiende Dodoma, wajumbe wa tume wajitoe, Makamu wa Rais anayechaguliwa kwa kigezo cha Uzanzibar ajiuzulu, mawaziri wa muungano wajiuzulu, wafanyakazi katika taasisi za bara waache kazi.
By July 1 wangeshakuwa na Zanzibar ya neema! I wish they could pack and go ASAP
Muda uliopendekezwa na mwanakijiji ni muafaka kwa kuwa mzazi anatakiwa kuonyesha busara katika maamuzi hata kama mtoto amekosea.
Kikweli ni mambo yanayohitaji maandalizi sio suala la kulala na kuamka, na kwa kuwa mzazi hana hasira na hasara aliyojichagulia mtoto ni suala la kumuonyesha upendo,busara,uvumilivu na hekima hadi mwisho.

Hatumuombei mabaya lakini incase mambo yakaenda ndivyo sivyo hapo atakuwa na kumbukumbu nzuri kwamba ndugu yake wa kweli hapa duniani ni nani.
 
Sijui kama hili linawezekana lakini ningependa sana kusikia kauli rasmi ya Wabunge wanaowakilisha Zanzibar kwenye bunge la muungano. Hansard ya michango yao mwaka jana zipo, sasa nataka nisikie kama bado wana msimamo ule ule au wao ni miongoni mwa wanzanzibari "wengi" wanataka tugawane mbao.

Pili, kura ya maoni ni muhimu sana ili tuokoe fedha za Tume ya katiba. Lakini pia tukumbuke tunalo zoezi la vitambulisho vy utaifa. Saa ni muhimu sana tujue mapema kabisa wanzibari ni watanzania au la ili na kwenye hili tuokoe fedha.

2014 kwangu mimi ni mbali sana. Tufanye hii kazi kura ya maoni kuanzia kesho asubuhi na by Ijumaa tuwe tumemaliza. And I very serious kwenye hili maana June 12 bunge la muungano linaanza. We need to save every shilling. Ijumaa tujue nani anapanda shangingi kuelekea Dodoma kwa vikao vya bunge au nani anapanda boti kuelekea upande wa pili.
 
Kiranga; wabara hawajawahi kuulalamikia Muungano kwa miaka mingi sana utaona wanacholalamikia sana na hili ni recent phenomenon ni Wazanzibari wanaolalamikia Muungano. Lakini la zaidi ni kuwa kuwauliza watu wa bara siyo sawa kwa sababu sisi hatujisikii kuwa annexed na Zanzibar au kukandamizwa na Zanzibar. Ndio maana Sudan haikupigwa kura ya maoni ya Sudan nzima bali watu wa Kusini tu; hata Quebec haikupigwa ya Canada nzima bali ni Quebec. Sababu ni nyepesi... tukipiga kura ya maoni ya nchi nzima na Bara wakasema wanataka Muungano na Zanzibar wanasema hawataki mnaamuaje stalemate hiyo?

La msingi ni kuwapa Zanzibar absolute freedom ya kuendesha kura yao ya maoni bila influence ya bara whatsoever. Watakachoamua bara will be fine either way. Lakini bara tukiamua Zanzibar haiwezi kuwa fine kwa namna yoyote.

1. Bila ya kupiga kura ya maoni nchi nzima huwezi kujua wabara wanautaka muungano au hawautaki. Kwamba wamelalamika au hawajalalamika hapo nyuma is irrelevant.Usipowashirikisha unaacha mwanya wa mzozo ambao unaweza kuzibwa kirahisi tangu mwanzo. Ukitaka kuondoa feelings za kwamba muungano uko one sided itabidi kura ipigwe pande mbili zote.

2. Mfano wa Quebec hata mimi niliufikiria.Lakini haupo appropriate hapa kwa sababu Quebec ni jimbo la Canada lililokuwa linaamua kwamba libaki Canada au lijitoe. Zanzibar si jimbo la Tanzania, ni a quasi-state within a state.

3. Ukipiga kura ya maoni nchi nzima, Zanzibar wakasema wanataka Muungano, bara wakasema hawataki, muungano unavunjwa.Point ya kupiga kura ya maoni nchi nzima ni kupata maoni ya wananchi wa nchi nzima, kwa maana muungano unawahusu wananchi wa nchi nzima, si Wazanzibari tu.Huwezi kuita hii situation stalemate. Stalemate itatokea iwapo kura za maoni zitakataa na kukubali muungano kwa 50% kote bara na visiwani. Kitakachotakiwa kuendeleza muungano kiwe simple majority on both sides.

Moja ya matatizo tunayoyaona katika muungano wetu sasa hivi ni hii habari ya kufanya mambo nusunusu au juu juu. Kama kuupitisha muungano kibungebunge bila a thorough process iliyowahusisha wananchi wote directly.

Sasa tushaona hili ni tatizo.Tunatakiwa tujifunze. Tusitake kurudia makosa kwa kufanya swala la muungano liamuliwe na upande mmoja tu wa muungano.

Tutawapa msemo watu wa bara wanaosema Wazanzibari wanapendelewa.
 
Sijui kama hili linawezekana lakini ningependa sana kusikia kauli rasmi ya Wabunge wanaowakilisha Zanzibar kwenye bunge la muungano. Hansard ya michango yao mwaka jana zipo, sasa nataka nisikie kama bado wana msimamo ule ule au wao ni miongoni mwa wanzanzibari "wengi" wanataka tugawane mbao.

Pili, kura ya maoni ni muhimu sana ili tuokoe fedha za Tume ya katiba. Lakini pia tukumbuke tunalo zoezi la vitambulisho vy utaifa. Saa ni muhimu sana tujue mapema kabisa wanzibari ni watanzania au la ili na kwenye hili tuokoe fedha.

2014 kwangu mimi ni mbali sana. Tufanye hii kazi kura ya maoni kuanzia kesho asubuhi na by Ijumaa tuwe tumemaliza. And I very serious kwenye hili maana June 12 bunge la muungano linaanza. We need to save every shilling. Ijumaa tujue nani anapanda shangingi kuelekea Dodoma kwa vikao vya bunge au nani anapanda boti kuelekea upande wa pili.

Be serious my friend this thing is not as simple as that.
 
Be serious my friend this thing is not as simple as that.

Unajua kiongozi, kelele zimekuwa nyingi sana kiasi kwamba unaona 24 ni muda mrefu. Let's sort this one out ili tujue moja. Kwa mfano vitambulisho vya utaifa itakuwaje? Tumeacha mambo kwa muda mrefu sana lakini sasa we have to run.
 
Kwa nini unafikiri swala la muungano na Zanzibar linatakiwa kupigiwa kura na Wazanzibari tu?

Hufikiri kwamba kuna uwezekanao Wazanzibari wengi wakasema wanataka kuwa katika muungano, ila watu wa bara wakawa hawataki muungano?
Ili kura ya maoni iwe na maana, inafaa ipigwe nchi nzima. Usichukulie for granted kwamba wabara wanautaka muungano.
Unaweza kumaliza kura ya maoni Zanzibar bila ya kuwashirikisha watu wa bara, ukapata kura za kukubali muungano nyingi sana, only to find out kuna malalamiko kutoka kwa watu wa bara kwamba hawakushirikishwa.
Kiranga, nadhani wabara wamekuwa kimya muda mrefu na haina maana wameridhika. Ninachojua wao wanasema kama zipo tofauti za muungano ziangaliwe mezani ili malalamiko ya kila upande yashughulikiwe.

Tunachokiona kwa sasa ni 'reaction' kutokana na kauli za matusi, kejeli na hata ubaguzi kutoka Zanzibar.
Wazanzibar wanaoishi bara na kufadika na muungano ni wengi kuliko wanaoishi sehemu nyingine duniani.
Wazanzibar ni mafundi sana wa kugeuza hadithi na kulaani muungano. Hawaongelei jema la muungano hata siku moja tofauti na wabara ambao kwao muungano ni mahusiano ya kijamii, kiuchumi toka enzi.

Wabara hawajawahi kuwabagua wazanzibar kisiasa, kijamii, kiuchumi. Hakuna Mzanzibar aliyechomwa moto au kuchomewa moto mali zake kwasababu tu ya Uzanzibar au dini. Wapo huku bara wakiwa na ajira,biashara n.k.

Hii ni dalili kuwa wabara wana uvumilivu dhidi ya wenzao. Kama mbara angekuwa na chuki za kizanzibar basi asingekaa kimya kumuona mzanzibar akichukua nafasi ya ajira, akipewa heka 10,000 na akiruhusiwa kushiriki kila jambo.
Tofauti, wenzetu wanabagua kwa misingi ya dini, kwamba wakristo wanaoishi na wazanzibar bara hawana haki Zanzibar na haatakiwi hata kuonekana. Kwa kuogopa ubaguzi dhidi ya waislam ambao ni 'wenzao' Zanzibar hawasemi kuwa waislam marufuku, la hasha! wanatumia neno machogo, wakimaanisha Mtanganyika bila kujali dini.

Dhambi ya ubaguzi si kwa wakristo tu, hata waislam ambao wanaitwa machogo. Kwahiyo ubaguzi ni across the board ila kwa kutaka kuungwa mkono hawatamki waislam na hawawezi kuchoma misikiti yao. Lau kutakuwepo na msikiti wa watu wa bara basi utaangaliwa kwa jicho la msikiti wa machogo.

Ikifka hapo wabara wanajiuliza kwanini wao wawe donors na wenzao recipient? Je, wana lose nini wzanzibar wakiwa peke yao? mfano mdogo sana, je walipojiondoa ligi ya michezo kuna nini kimepungua Premier league? Kinyume chake ligi ya Zanzibar imezorota. Anyway!

Wao ndio wasiotaka maongezi, wanachotaka ni vurugu. Ili kuepusha shari basi wapewe kura ya maoni. Kama wengi watasema basi na 'ukoloni' hewala waachwe waondoke kabla ya december 31. Na ukweli siyo waachwe bali waamue kuondoka kabla ya July 1 2012.

Njia rahisi ni kupitisha mswada ndani ya BLW kutomtambua Mkamu wa Rais kutoka Zanzibar,Kutowatambua mawaziri wa muungano kutoka Zanzibar, kutoruhusu wabunge wao kuja Dodoma, kuweka visa ya kuingia Zanzibar. Tayari wana wimbo wa Taifa, bendera n.k.

Kitu ambacho sitakubali ni kuwa na serikali tatu au mkataba. Hivi vyote maana yake ni kunufaisha Mzanzibar kwa ujira wa ubaguzi wa imani, hata wasifu(wanatuita machogo). Hayo yatakuwa kumbebesha Mtanganyika mzigo usio na maana.
EAC ilipovunjika tulianza A na sasa bado tupo kama taifa sembuse Zanzibar!

Mimi ningependa waondoke mapema sana, na wala asitokee Mtanganyika akadhani kuwa atadhurika au kuathirika na hilo.
Wasichome moto nyumba za watu na makanisa au masinagogi, they have upper hand on union matter.

Wazanzibar amueni by July 1 2012 no more union! Nitawaunga mkono
 
Kwanini unaamini kuwa wasioutaka muungano ni wachache?
Kwa sababu kama wangekuwa wengi kihivyo wangeweza kuwashawishi wajumbe wa BLW kuleta sheria ya kura ya maoni ambayo ingependa kwa urahisi. Kama ile sheria ya Jussa ya kuwakatalia watu wa bara ajira Zanzibar ilizuiliwa kwa kura moja tu nina uhakika ya kujitenga itapita kwa kura nyingi tu.
 
Mfano unaotolewa siku za hivi karibuni ni "sahihi 500,000" za wanaodaiwa "Wazanzibari" wasiotaka Muungano. Sasa kwenye mahali ambapo pana watu milioni 1.5
Umejuaje Zanzibar kuna watu milioni na nusu, kwa chanzo gani?

Kwa sababu kama wangekuwa wengi kihivyo
"Wengi kihivyo" ndio wengi wangapi? "Wengi" ndio nini? "Watu wengi" ni watu wote kasoro mmoja au? Watu laki tano sio "wengi"?

Yote YAMO MIKONONI MWA WAZANZIBARI.
Kwa nini una assume kwamba wenye matatizo na Muungano ni upande mmoja tu, Zanzibar, umejuaje walio wengi huku Bara tunataka Muungano? Kwa nini unatuongelea?
 
Mengi yanaumiza ila inauma sana kwa wanaofahamu maana, ila kwa hapa ilipofika nadhani yatosha.
Ila ikumbukwe kwamba Dar itakuwa nchi jirani na sivyo ilivyo sasa kwani hata kwenda kumtembelea mpwa itabidi passport kama sio na visa kabisa!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom