Kama Kuna Kazi Ngumu Kwa Sasa TZ....

Mtoboasiri

JF-Expert Member
Aug 6, 2009
5,101
1,946
..basi ni hii waliyopewa wenzetu ya kujaribu kuwafanya watu wenye akili zao wakubali kugeuza uongo kuwa kweli kwa manufaa ya Chama Cha Magamba. Nakupa mifano michache (mdau ongeza nitakayokuwa nimeisahau):


  • CHADEMA ni chama cha Wachaga na Wakristo (soma Wakatoliki)
  • CHADEMA ni chama cha kanisa Katoliki
  • CHADEMA hakikubaliki na umma (lakini ndicho hicho wanachokisakama kila kukicha - kama hakikubaliki na umma ina maana hakina madhara kwa Chama Cha Magamba, iweje hakiishi kutajwa midomoni mwao?) Mbona vyama vingine havitajwi tajwi namna hii ya CHADEMA?
  • Akipigwa mawe mbunge kutoka Chama Cha Magamba, alietupa mawe katumwa na CHADEMA
  • Hakuna matatizo Tanzania, kuwa kuna hali ngumu ya maisha hizo ni propaganda za CHADEMA.
  • CHADEMA inapotosha wananchi (wakati huo huo watu hao hao wanasema Watanzania hawawezi kudanganyika!)
  • Viti maalumu vifutiliwe mbali - maana vinaiongezea ruzuku CHADEMA (utadhani viti maalumu vipo kwa ajili ya CHADEMA pekee)
  • JF inafadhiliwa na CHADEMA (wenyewe wakiwemo humu humu - wengine wanaaga mara tatu tatu kuwa wanajiondoa JF kwa kuwa MODS wanapendelea CHADEMA lakini hatuoni wakitoka).
  • ....
  • ....
  • ....
Jamani, mnazima moto kwa petroli!!!
 
Back
Top Bottom