Kama kondomu zinatumika ............................kwanini mimba zitungwe???

WomanOfSubstance

JF-Expert Member
May 30, 2008
5,457
956
Kuna mjadala unaendelea Re: Maiti za vitoto zaidi ya 10 zafukuliwa shimo moja

Vincent Augustino mwanzisha thread kauliza:
Kama hizo ni mimba zimetolewa ndani ya siku moja; jee wiki, mwezi na mwaka? Bei ya condom nayo imepanda sana au; kwanini mimba zitungwe kama kondomu zinatumika?

Hili mnalionaje wajameni? Kama mimba zinatungwa na kutolewa kwa kasi hivi, je UKIMWI upo?..Iweje mtu mwanaume na mwanamke wanaoshiriki kitendo wazembee hadi haya yatokee?

Naombeni michango yenu tafadhali.
 
Sio watu wengi wanatumia kondomu kama tunavyofikiria.

Mimba zinatungwa na watu ambao wako pamoja kwa mda mrefu, wanaaminiana lakini hawataki kutumia kondomu na wakati huo huo hawako tayari kwa majukumu ya uzazi.Kwa vile wako pamoja kwa mda mrefu,wanaaminiana na wengine huwa wanapima kuhakikisha wote wako salama,swala la ukimwi linakuwa limekingwa.Swala la mimba linakuwa halijakingwa kwani wengi wanafikiri wana weza kujizuia kwa njia zingine (ndefu kidogo kuzieleza) ambazo mara nyingi wanashindwa kuzifata au hawana elimu ya kutosha kujua kwamba uwezo bado upo wa kupata mimba hata wakitumia njia hizo.


Kundi lingine ndio ambalo halijali,wazembe,dharau au wanashindwa kujizuia matamanio yao mpaka wawe na kondomu hili kukamilisha tendo.Hawajali kitachotokea mbeleni na hili ndio kundi linalopata ukimwi na hizi mimba zinazotolewa hovyo hovyo.
 
Maadam vitendo vya utoaji mimba hufanywa ndani ya mahospitali kama ilivyogundulika huko Mwananyamala ( kwenye shimo la taka kumekutwa vitoto zaidi ya kumi vimetupwa), inapelekea kuamini kwamba idara ya afya haifanyi kazi ipasavyo kupeleka huduma na elimu ya uzazi wa mpango na kuzuia maabukizi ya UKIMWI.

Taasis na vitengo husika kwenye Wizara ya Afya, TACAIDS, NGOs etc wanaweza kutoa maelezo gani kuhusu hili swala?

Hili suala la " KUAMINIANA" nadhani ni kikwazo kikubwa sana kwenye harakati za kupambana na UKIMWI."KUAMINIANA" ndio msingi wa mahusiano ya mapenzi/ndoa..... lakini je kuaminiana ni pamoja na kuweka maisha ya mtu hatarini? Wanandoa wengi wamefungwa na hii dhana ya kuaminiana japo wanajua kabisa uaminifu ni kitu kigumu kukipima. Kama hakuna kipimo cha uaminifu... je ni sahihi kuendelea kukumbatia tafsiri ya "UAMINIFU" kwa mtizamo wa zama zile za kabla ya UKIMWI?
 
Nadhani statistic ya watumiaji kondom kwa siku ni ndogo thats why mimba zinatungwa,ila pia tujiulize sababu za utoaji.
 
Back
Top Bottom