Kama kawa; CCM na rushwa Arumeru

OSOKONI

JF-Expert Member
Oct 20, 2011
10,965
5,336
CCM Arumeru waanza kuvurugana Send to a friend



SIKU moja baada ya wanachama wa CCM, Jimbo la Arumeru Mashariki kumpendekeza Sioi Sumari kuwa mgombea wake katika uchaguzi mdogo ujao, baadhi ya wanachama wa Umoja wa Vijana (UVCCM) wilayani humo, wamepinga uteuzi huo wakidai kuwa uchaguzi uligubikwa na mizengwe.

Juzi, mkutano Mkuu wa Jimbo hilo ulimchagua Sioi, mtoto wa aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo, marehemu Jeremiah Sumari kwa kura 361 akifuatiwa na William Sarakikya aliyepata kura 259, Elishilia Kaaya (176), Elirehema Kaaya (205), Anthony Musari (22) na Moses Urio (11).

Lakini jana, baadhi ya wajumbe hao wa UVCCM wakiongozwa na Mjumbe wa Baraza la Umoja Mkoani wa Arusha, K
ennedy Mpumilwa walidai kwamba uchaguzi huo ni batili kwa kuwa ulitawaliwa na misingi ya rushwa.

Mpumilwa alidai kwamba uchaguzi huo ulijaa rushwa kila kona. Hata hivyo, hakuweka bayana kama walihongwa ili wamchague nani kati ya wagombea hao sita.

Alidai kwamba kigogo mmoja wa UVCCM ngazi ya mkoa aliyeongozana na kada mmoja wa jumuiya hiyo, walikuwa ndani ya gari karibu na eneo la uchaguzi wakigawa rushwa kwa wajumbe.

“Huu uchaguzi haufai kabisa baadhi ya wajumbe walihongwa. Ilikuwa ikitolewa 150,000 kwa kila mjumbe atakayekubali. Sasa hii CCM gani kama uteuzi tu hadi ufuate rushwa,” alidai Mpumilwa.

Alisema kwa jinsi mchakato wa uchaguzi huo ulivyofanyika, ni dhahiri chama hicho kimeingia katika mpasuko mkubwa ambao kama usipoangaliwa kwa makini, unaweza kukiathiri.

Mpumilwa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi na Fedha wa UVCCM Wilaya ya Arumeru, alisema baadhi ya wanachama wa umoja huo wilayani humo wamechukizwa na mambo yaliyojitokeza katika uchaguzi huo huku wengine wakitishia kuhamia upinzani wakati wowote.

“Nakwambia vijana wamechukizwa kabisa na kilichofanyika katika mchakato wa uchaguzi, sasa wengine wametishia kwenda upinzani wakati wowote,” alieleza Mpumilwa.

 
Pia angalia hizo namba kwani kura za Elishia Kaaya176 wakati namba nne Elirehema Kaaya206! Takukuru walionya lakini nashangaa kwanini hawajachukua hatua mpaka watu wengine watuambie wakati wao wapo. Inasikitisha kwa kweli.
 
Takukuru isitegemewe ktk jambo kama hilo, haina uwezo. Hawana man power ya kutosha jimbo zima pale wana ccm watakapo sambaa kama nzige wakigawa rushwa, pia nao ni washika wa ccm.. Reff. Igunga, nilikuwepo.
 
ccm arumeru waanza kuvurugana send to a friend



siku moja baada ya wanachama wa ccm, jimbo la arumeru mashariki kumpendekeza sioi sumari kuwa mgombea wake katika uchaguzi mdogo ujao, baadhi ya wanachama wa umoja wa vijana (uvccm) wilayani humo, wamepinga uteuzi huo wakidai kuwa uchaguzi uligubikwa na mizengwe.

Juzi, mkutano mkuu wa jimbo hilo ulimchagua sioi, mtoto wa aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, marehemu jeremiah sumari kwa kura 361 akifuatiwa na william sarakikya aliyepata kura 259, elishilia kaaya (176), elirehema kaaya (205), anthony musari (22) na moses urio (11).

Lakini jana, baadhi ya wajumbe hao wa uvccm wakiongozwa na mjumbe wa baraza la umoja mkoani wa arusha, k
ennedy mpumilwa walidai kwamba uchaguzi huo ni batili kwa kuwa ulitawaliwa na misingi ya rushwa.

Mpumilwa alidai kwamba uchaguzi huo ulijaa rushwa kila kona. Hata hivyo, hakuweka bayana kama walihongwa ili wamchague nani kati ya wagombea hao sita.

Alidai kwamba kigogo mmoja wa uvccm ngazi ya mkoa aliyeongozana na kada mmoja wa jumuiya hiyo, walikuwa ndani ya gari karibu na eneo la uchaguzi wakigawa rushwa kwa wajumbe.

“huu uchaguzi haufai kabisa baadhi ya wajumbe walihongwa. Ilikuwa ikitolewa 150,000 kwa kila mjumbe atakayekubali. Sasa hii ccm gani kama uteuzi tu hadi ufuate rushwa,” alidai mpumilwa.

Alisema kwa jinsi mchakato wa uchaguzi huo ulivyofanyika, ni dhahiri chama hicho kimeingia katika mpasuko mkubwa ambao kama usipoangaliwa kwa makini, unaweza kukiathiri.

mpumilwa ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya uchumi na fedha wa uvccm wilaya ya arumeru, alisema baadhi ya wanachama wa umoja huo wilayani humo wamechukizwa na mambo yaliyojitokeza katika uchaguzi huo huku wengine wakitishia kuhamia upinzani wakati wowote.

“nakwambia vijana wamechukizwa kabisa na kilichofanyika katika mchakato wa uchaguzi, sasa wengine wametishia kwenda upinzani wakati wowote,” alieleza mpumilwa.


safi kabisa ndo tulikuwa tunataka mjichanganye tutawaangusha tu, hii meru siyo ya familia fulani
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom