Kama ilishindikana kutatua tatizo la UMEME kwa miaka 17, je itawezekana kwa miezi 3?

EJM_

JF-Expert Member
Jul 8, 2011
3,836
2,091
Mi napata tabu kidogo, nimesikiliza MIKAKATI/MIPANGO NA MBIO nyingi ambazo zilikuwa na lengo la kutatua tatizo la umeme ifikapo mwaka 2015 (Miaka minne kutoka sasa) lakini juzi hapa waziri mkuu Mh. Mizengo Pinda amesema serikali inaingia kazini ili kufikia mwezi December mwaka huu tatizo la umeme liwe historia sasa mi najiuliza kidogo,
  • Je Serikali ilikuwa na nia ya dhati kutatua tatizo la umeme?
  • Kama wameshindwa kutatua tatizo kwa miaka zaidi ya kumi na saba (mgao wa kwanza wa umeme ulikuwa 1994) je wataweza kwa miezi mitatu?
  • Nani anafaidika na matatizo ya umeme hapa nchini?
Jamani hebu tulitazame hili kidogo.....
 
Majibu mengi huwa ya kisiasa, hayana ukweli...

Mh, sasa hii inamaanish kwa muda wote huo tumekuwa hatuoni kama tulikuwa tunapewa majibu ya kisiasa na na hayakuwa na lengo la kutatua tatizo la msingi? Why now?
 
Back
Top Bottom