Kama huyu ndo wakuoa!! Nishaurini jamani maana niko njia panda kwa kweli...

Hapo m2 me siöni tatizo coz wote ni wakristu tena me mwenyewe ni Anglican like u bt shda mueleweshane coz uhusiano unaonekana divine relatioship so ucmuache coz huyo ni mkeo kama isingekuwa hvyo mngeachana toka zamani.
 
Kikubwa kitakachokukwaza akiwa Mlokole ni nini?
Mzee unaona ishu sana kuacha pombe siyo?

Tatizo sio ulokole ndugu, na wala mimi si mnyaji wa pombe wala kilevi chochote kile wala dhambi yeyote si entertain kabisa. SWALA hapa ni KUSALI KWINGINE NA MIMI KWINGINE, UTOFAUTI WA IMANI, IMANI=LAZIMA IENDANE NA TABIA. Bwana PakaJimmy ikumbukwe kuwa hapa tunatengeneza familia; je nini kitatokea endapo baba na mama hawako pamoja? Je watoto watakuwa je? Au ndo kutengeneza familia yenye matabaka mawili?
 
oa kwa sababu mtu umempenda na sio sababu its covenient umri umefika na unataka watoto na mtu wa kukupikia nyumbani......mie sidhani kama huyo dada unampenda,uko naye kwa sababu na wewe unahitaji kuwa na mtu...which is wrong to me,.........
sidhani dhehebu tofauti ni kikwazo,watu wameoa waislam na bado mambo yakaenda,simpooo kila mtu abaki na dhehebu lake,kama mlivyokuwa wachumba kila mtu na dhehebu lake na kwenye ndoa mbaki hivyo hivyo.....au la tueleze nini tatizo litakalotokea iwapo kila mtu atabaki na dhehebu lake ili tukusaidie zaidi....maana tunacoment hatujui nini tofauti ya hayo madhehebu mawili endapo kuna ugumu kuuoana ..................ningekushauri badilisha dhehebu nenda la kwake oa then rudi kny dhehebu lako baada ya watoto wawili lol ila nitaonekana mie wa kuzimu buree lol .......................watu mna msimamo mikali when it comes to dini mpk mnatisha kha!

DADA NEEMA; Tatizo la kwanza ni kwamba huyu binti tulikuwa twasali pamoja Anglican na mpaka tunakubaliana kuazisha urafiki/uchumba kwa nia ya kuoana tunasali pamoja.
Pili: ukumbuke tabia huendana na imani mtu aliyo nayo kwa Mungu wake.
Tatu: Kuwa na imani tofauti kwenye familia ni msingi wa matabaka mawili au matatu kwenye familia
Nne: Ikiwa wewe ni mume au mke utajisikiaje pale ambapo weekend unataka kuwa na mumeo/mkeo yeye yuko either kanisani hadi jioni?
Mwisho: Kuna haja gani ya kuwa na mtu lakini kila mtu ana njia yake dada ukimwambia mwenzio twende kulia anakuambia twende kushoto?
 
kaka wewe ndo mbaguzi wa madhehebu maana yeye haoni tatizo kuwa na wewe mu Anglican!!mie nakushangaa maana najua unaoa mtu sio dini yake! watu mnachanganya mambo,hv unajua maana ya iman? iman ni kile unachokiamin wewe,hv ni kweli kwamba mkioana na mtu kila unachoamini wewe na mkeo ndicho atakachoamini?sasa kwann umlazimishe vyakwako?afterall mbingun kila mtu atasimama mwenyewe kujibu!kwenye iman hakuna swala la mwili mmoja!mimi ni lutheran na my partner ni r.c jpili kila mtu anaenda kwake na watoto watasali kwa baba,kwhy maisha yanaenda smoothly.kama unampenda muoe!!
 
mbona kwenye swala la dini halina shida-wote si wakristo-kwani kuna ulazima gani wa kufwata kwenye dhehebu lake?
mtulize mfunge ndoa ye nu then kama kila mtu ataendelea na dhehebu lake haina shida,kitu ni kilekile 2,Mungu ni yuleyule tu
 
Kaunga tabu ipo! Wote in wakristo, ni sawa kbs lakini hiyo ndoa itafungiwa wapi, Anglican au Assemblies, kwasababu mwanaume atataka ndoa ifungiwe Anglican na mwanamke hataki tena kuabudu Anglican so automatic mwanamke atataka ndoa ifungiwe Assemblies of God wakati mwanaume hataki kwenda kuabudu huko.
Kingine ni suala la kuabudu baada ya kuoana, sikashifu dhehebu la mtu kwa sababu nia yetu wote tunamtafuta Mungu lakin haya madhehebu ya kilokole yamasababisha ndoa za watu wengi kuingia kwenye migogoro na wengine wameachana kabisa sababu ya ulokole. Kwako Godliver, ushauri wangu kwako, kwsbb umeshaongea nae vya kutosha na bado ameshilia uamzi wake huo, tafuta ndugu zake na ndugu zako wa karibu jaribu kuwashirikisha juu ya jambo hili tena mkiwa wote, kila mtu aseme kilichoujaza moyo wake. Baada ya hicho kikao, na ushauri wa MMU ukichanganya na zako utapata jibu kwamba umuoe au utafute mwanamke mwingine.
Kila la heri!

Duh
Wote ni wakristu; utofauti wa madhehebu ndio uvunjd uchumba wenu? Yaani mimi sioni shida kabisa hap.
 
Duh
Wote ni wakristu; utofauti wa madhehebu ndio uvunjd uchumba wenu? Yaani mimi sioni shida kabisa hap.

mkuu shida ipo tena kubwa sana hapo. Achana kabisa na walokole ndugu, hapo huyo dada anaona 'image ya shetani, ndani ya mshikaji ndo maana napata wakati mgumu. Na hao waumini wenzake huko assemblies watamparura usoni kama atawaambia eti ana mchumba muanglikana.

Mkuu mpe 'ultimatum' huyo dada, akikuzingua mpige chini. Miaka minne ndugu yangu kama ni mtoto angekuwa chekechea sasa. We endelea kusubiri mwenzio akipata mlokole mwenzake ndo utaisoma kwa nyuma. Hapo ana baitaimu tu kwa kuwa hajapata mlokole mwenzake mkuu.
 
sikushuri ubadili imani yako kwa sababu ya mwanamke maana leo mlokole, kesho akiwa muislamu utabadili tena? Kama mwanaume msimamo ni muhimu sana. PR yako itashuka sana ingawa sio kosa
 
Ndugu zangu wana JF; Kiukweli nilichokieleza hapo kwenye mada kuu ni kijisehemu tu cha mlolongo wa mambo mengi; niweke tu wazi kuwa hata mimi mwenyewe namcha Mungu na nakubaliana kabisa na imani hiyo ya kilikole. Ila sikuwa tayari kuhamia dhehebu lingine kwa kuwa imani yangu ni kubwa sana kwa Mungu wangu ukizingatia kwamba ULOKOLE SI DHEHEBU bali NI KUACHA DHAMBI NA KUMCHA MUNGU HUKU UKIMWAMINI YESU KRISTO KAMA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YAKO.

LAKINI TATIZO: NI KAMA NILIVYOANISHA HAPO JUU KWA DADA NEEMA.......................
Mwenzangu alibadili dhehebu bila hata kunishirikisha nikashangaa namwambia twende kanisani ananiambia siendi leo naenda tag hadi siku nilivyogundu nikamuuliiza akagoma kusema amehamia na siku zilivyozidi na mimi kumbia twende kasani ikabidi tu aseme ukweli yuko TAG. Nilimfundisha sana na kuelimishana sana kuazia 2010 had 2011 (ni miaka 2) mara narudi mara sirudi yakawa ni maisha ya malumbano tu (nikimwambia tuachane basi maana tutapotezeana muda JIBU sikuachi na siko tayari kuachana na wewe.) NDUGU WANA NDOA NI MWILI MMOJA SASA KAMA HAMUENDI SAWA SAWA (AMOSI 3:3) JE NI MWILI MMOJA AU NI VIPANDE? JE HAKUTAKUWA NA MAKWAZO KATIKA NDOA KWELI? LABDA WALE AMBAO NI WANANDOA NA WAKO NA IMANI TOFAUTI ZA DINI/MADHEHEBU WANIPE UZOEFU JAMANI KABLA SIJAINGIA MAISHA YAO YAKO JE NDANI YA NDOA? MPANGILIO WA MAJUKUMU NA WATOTO WAO JE? Jamani mwenzenu mimi naamini upendo ndani ya nyumba ni pamoja na kuwa na umoja kwa kila jambo.


WENYE NDOA TAFADHALI MNIJUZE KATIKA HILI NANYI MSIKAE KIMYA TU TAFADHALINI.
 
kwani huyo mtu mlizaliwa pamoja? isitoshe hata hujamdo sasa kinachokusumbua nini wewe? Tafuta mchumba mwingine uoe. Kama unadhani watu wengine wataleta suluhu ujue umekwisha maana ikiwa nyie wa2 hamuwezi kuelewana, hao wa pembeni mchango wao ni mdogo sana coz mwishowe nyie wawili ndo mtakaoishi pamoja
 
Pole sana ndugu yangu.
Nafikiri hapo jambo la kufanya ni kukaa chini kama kweli manpendana na mlishapanga kuoana. Kaa nae chini muulize kama yuko tayari kuwa nawewe na akikubali naamini inawezekana. Tatizo ninaloliona lipo kwako baada ya huyu binti kuanza kusali dhehebu lingine ila km yeye anakubali basi fanyeni taratibu za ndoa. ila itategemea utayari wako maana naona tatizo ni wewe kukubali dhehebu lake.
Nakutakia mafanikio
 
Pole sana kaka, lakini kumbuka, Madhehebu si mpango wa Mungu. Jali sana imani.
 
DADA NEEMA; Tatizo la kwanza ni kwamba huyu binti tulikuwa twasali pamoja Anglican na mpaka tunakubaliana kuazisha urafiki/uchumba kwa nia ya kuoana tunasali pamoja.
Pili: ukumbuke tabia huendana na imani mtu aliyo nayo kwa Mungu wake.
Tatu: Kuwa na imani tofauti kwenye familia ni msingi wa matabaka mawili au matatu kwenye familia
Nne: Ikiwa wewe ni mume au mke utajisikiaje pale ambapo weekend unataka kuwa na mumeo/mkeo yeye yuko either kanisani hadi jioni?
Mwisho: Kuna haja gani ya kuwa na mtu lakini kila mtu ana njia yake dada ukimwambia mwenzio twende kulia anakuambia twende kushoto?

Kaka yangu mimi sioni tatizo hapo kama msichana mwenyewe anakubali kuolewa na wewe.kwani mwanglikana na mlokole si ni imani moja?? nijuacho mimi anglikana na assemblies wote wanamwamini YESU,sasa labda useme kuwa hauko tayari kuoa mlokole ila mlokole ni mtu tu kama watu wengine.
Sidhani kama huyo dada angekuwa mzinzi au mlevi ungetamani hata kumuoa lakini ninaamini ni kwa tabia njema aliyokuwa nayo ndio ukampenda na ndio maana hata mlikutana huko kanisani anglikana na kuchumbiana. mshukuru MUNGU na umuombe akupe hekima katika kuliamua hili ili usije kujuta katika lolote utakaloamua.
 
hivi Yesu wa Anglican na Yesu wa Assemblies of God ni tofauti? nionavyo mie Yesu ni huyo huyo, bado sijaona tatizo linalowafanya mshindwe kuoana. afterall Yesu hakutuletea madhehebu, hebu kaoaneni,
 
Kashapata mlokole mwenzie ndo mana nyodo zimeanza. Maisha ya ndoa c mchezo ujue na inahtaj ful comitment. We kaza moyo mmwage, songa mbele, mwanamke asiku drive crazy mzee. Gud luck
 
yaani wote wakristo na bado mnabaguana?mbona wapo waliooa waislamu and vice versa?
 
ongea nae mfunge ndoa anglican ila kila mtu abaki na iman yake zen watoto mtagawana wa kwanza anglican wa pili assemblis ivyo ivyo mpaka mtoto wa mwisho zen wakikua wataamua wenyewe, pia ongea nae majukumu yake kama mke ayajue asije akaacha kupika,kufua,usafi kwa kisingizio cha fellowship au akakunyima haki yako akidai udini akikataa vyote hivyo basi itabid muachane maana mtaja sumbuana mbele
 
Ndugu hebu oa huyo binti mlokole kwanza atakukuza kiimani ,ndoa yenu itajengwa kwenye misingi imara mungu atawasimamia ,mie sioni tatizo kabisa,
Mwambie mfungie ndoa kanisani kwenu kisha aendelee na dini yake ...au na hilo hataki?
all the best
 
Back
Top Bottom