Kama huridhiki mwambie, usilipize

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,810
15,398
Kama huridhiki mwambie, usilipize..........

Ni miongoni mwa makosa makubwa sana kwenye uhusiano wetu. Hebu fikiria kwamba, mumeo anashiriki tendo na wewe kwa njia ambayo aikuridhishi.

Inaweza kuwa ni njia ya matumizi makubwa ya nguvu, njia ya haraka haraka bila hata kuchokozana sana, njia ya dharau na kiburi na njia nyingine ambazo hazikuridhishi au ambazo zinakufanya ujihisi kama chombo chake cha starehe na sio mwenza.


Badala ya kumwambia, unamnunia na kuanza kumfanyia visa, badala ya kumwambia unambeza na kumdharau. Hili ni kosa kubwa sana, ni kosa ambalo hulegeza na hatimaye kuangusha ndoa.

Dawa ni kusema, kumwambia mwenzako kuhusu kile ambacho hakikuridhishi na sio kuwa bubu na klpa kisasi katika mamo menine. Mwambie kwa pendo, kwa hekima na busara.


 
wanaume wengine wakiambiwa watang'aka kuwa wake zao wanatoka wakati wanawake wakiambiwa wanatafta mbinu za kumridhisha loh
 
kama wanashindwa kuambiana harufu za midomo wataambiana haya? watu wana heshimiana kinafiki wengi sana, nakuunga mkono mkuu kuambiana huwa kunaboresha sana mahusiano, umwambie vipi! hapo ndio wengi wanashindwa, wanawake wanahisi waume zao watawaona malaya au wameona kwengine ndio maana wanawaambia
 
We Husninyo umenifanya nicheke sasa! Asipojirekibisha mi naona hapo sasa ni kazi nyingne tena! Ila ngoja wataalamu watuambie inakuwaje!
 
Back
Top Bottom