Kama Hukutumia Hii Kitu Wewe sio mjanja bado!

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,706
155,225
390903_323129897714527_100000525597189_1233296_720643457_n.jpg
 
Nimetumia uturi YU for Men...mamsap huwa ananicheka...ananambia "ile pafyumu yako iliyokuwa inauzwa sh 650 za Tanzania unaikumbuka???"
 
Daaah! mkuu wewe ni noma. Yaani wakati huo utakuta kidume kimejiweka utuli wa YU halafu chupi kavaa V.I.P lo!! sasa hapo bahati mbaya V.I.P ikatike kwa chini, lazime uikamatie kifuani.
 
kishapaka hiyo kitu, kama unaenda kwenye sherehe unajipulizia na pafyumu aina ya KOBRA.
Basi unatoka bomba kabisa.
 
IPP zamani walikuwa wanatengeneza mafuta , nimeyasahau jina.
Ila bwana mambo ya zamani yalikuwa safi sana licha ya hali ngumu ya maisha iliyokuwepo enzi hizo za uhujumu uchumi, magendo na bei za kuruka
 
jua kali,kulikua na sabuni ya kufulia iliitwa "kwanga"

Iliitwa kanga bwana. siyo kwanga. yote mmesema ila mmesahau picha lazima zikapigwe studio ukiwa umeshika kiuno nyuma pazia jekundu au la bluu. na ua pembeni yako. lol nyimbo zetu zilikuwa za akina kilimanjaro jazz band na ottu jazz band.
 
Back
Top Bottom