Kama hujafanya haya wewe haujakaa uswazi. (uswahilini)

Wa Kishua Wanaona WTF is this tehtehteh.

1. KUCHEZA MPIRA PEKU AU KIATU CHA RAFIKI YAKO CHA KUSHOTO KUVAA KULIA UCHEZEE MPIRA.

2. KUSUKUMA MA TAIRI YA GARI NA MARINGI YA BESKELI NA KIJITI.

3. KUKIMBIZA KUKU WA JIRANI.

4. KUPELEKA TABIA ZA USWAZI MITAA SIO YA USWAZI NA KUANZA KUJISAIDIA PWANI AU NYUMBA ZINAZOJENGWA.

5. KUTIZAMA WATOTO MOVIE NJE YA MADIRISHA KUJIPANGA MWENYEWE NDIO ALIPOWARUHUSU.

6. UKIENDA KUUZA MKAA NA GARI LA MKAA MITAA YA SIO WASWAZI TUNAITWA PAKA MWEUSIIIIII AU MAJI YAMEKATIKAAAA.

7. KULALAMIKA KWA MJUMBE WA NYUMBA 10 KUMI KILA SIKU.

8. WAKINA DADA NA KINA MAMA KUVAA MAKANGA YA USHARI WAKIENDA KUTEKA MAJI BOMBANI NA KUANZA KURUSHIANA NGUMI.

9. NYUMBA ZA TRAIN MILANGO KUTIZAMANA KILA MTU KAFUNGULIA RADIO KWA SAUTI HUYU TAARABU HUYU BONGO FLAVA TEHTEH.

10. MPANGAJI AKIHAMA LAZIMA AONDOKE NA TAA ZA MWENYE NYUMBA(CHUMBA) AU UTAKUTA BETRI NATIONAL ZIMEEGESHWA NJE YA MATOFALI ZIPATE JUA TEHTEH!

UKIWEZA KUISHI NA JAMAA TOFAUTI NA PANDE ZOTE MBILI RAHISI KUISHI KOKOTE NA WATU WA TABIA NYINGI RAHA SANA. CHA MUHIMU KUPENDANA NA KUTOA ZARAU.
 
Nimekumbuka Uswazi ukijikojolea Kitandani utakoma Kidumbwedumbwe Nyimbo mtaani ndio inakuwa mwisho wa ukikojozi kudadadeki.
 
kama hujafanya mambo haya hujakaa uswazi
1. Kulilia soda ya mgeni
2. Kukataa kuoga
3. Kukataa kwenda shule kwa kusingizia unaumwa
4. Kutochez mbali na nyumbani siku ya sikukuu ili ufaidi pilau
5. Kulamba kamasi
6. Kucheza kombolela/kidali au kibaba na mama
7. Kwenda kuangalia muvi kwenye mabanda ya video.
Haya wadau tuendelee na mengine ambayo nimeyasahau.[/QUOTE kula kwa watu alafu unajifuta mikono na mchanga.
 
kasichana kanafunua sketi kwa mbali alafu kanaonyesha kachupi kwa mbali alafu kanakwambia umeona....? picha.....?
 
1 Kukimbilia gari na kunusa moshi wake,
2 kusokota sigara za makaratasi,
3. kuogelea mtoni, na kwenda kutafuta maembe na ngweda
4.kufuga sungura,sili na njiwa halafu unauza hela unanunulia pipi gololi na biskuti
5..kuficha plate za kulia kande shuleni chini ya dawati sehemu ya kukalia,kutumia makopo yaliyoisha dawa za paracetamol kama bakuli kulia kande/ugali skonga
6. Kuchora kwenye begi la shule,dawati,daftari chata za reebok,fila,na nike
7 kutembea na begi kuubwa la dinosauri ndani umeweka daftari mbili
8.kulilia kunuliwa mfuko wa sport na njumu za maradona/romario kwa ajili ya kuendea shule
9. Kuvaa nguo mpya hadi skukuu suruali za bioct,bigsam,tokyo
10.. Kurudi nyumbani wenzako wanaporudishwa ada hata kama umelipa

8 & 10 nimo.
Searching...100%
Loading...100%
Network Connected !
 
Enzi hizo kuangali video kwa jirani MPAKA MUOGE kwanza ndo mruhusiwe.
Na huko ndani mnaenda kukaa chini.
uwiii ndo ulikuwa mchezo wetu mpaka baba akakasirika akaamua kutununulia tv hme ..........nasi tukalipiza kisasi kama haujaoga hauingii na ukiingia unakaa chini...........na akna kuongea ukiongea unatolewa nje.
 
1) kujipikilisha
2) kudaka panzi
3) shule kwa wasichana kuwekewa kioo chini na ,mvulana wanachungulia chupi uliyovaa
4) kuwekewa bigijii kwenye dawati hafu unakalia
5) kulilia nguo ya sikukuu kama ya fulani
6) kukimbilia mdundiko mpaka mnapotea hamjui mko wapi........hii nilichapwa sikurudia tena
 
uwiiiiiii nimecheka sana na kunikumbusha utoto......loh natamani kurudia utoto jamani ni raha sana
 
Kutoka na nyama nje baada ya kula ili wenzako watamani, kutiana migombani au mferejini
 
1. Ukikojoa kitandan wanakuimbia kidedea mtaa mzima
2.Kujipikilisha
3.Kuna michezo kama kifimbo cheza,bento,ngumi nyuma ilikuwa balaa
4.Mkipika wali,chapat au nyama hamuendi kucheza na pia rafiki yako akija kwenu
unamfukuza arudi kwao
5.kumwekea mwenzako kitu kichwani kisha mtu wangu ana kidengele kesho kutwa ntamnyoa nywele
6.bolibo
7.tikli
8.harusi kubitika
9.ana ana do kapasuka........
10.kujifanya unasinzia siku ya ubwabwa
 
5.kumwekea mwenzako kitu kichwani kisha mtu wangu ana kidengele kesho kutwa ntamnyoa nywele
6.bolibo
7.tikli
8.harusi kubitika
9.ana ana do kapasuka........
10.kujifanya unasinzia siku ya ubwabwa

# 10. Noma

Near by Shaba pub Mbeya.
 
kimbiakuoga.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom