Kama hujafanya haya wewe haujakaa uswazi. (uswahilini)

Hahahahahaha! Ezi za komborela mi nlikua natafutwa mpaka basi,mwisho wananifumania na sarah mafichoni
 
Kombolela halafu wewe na demu wako mnakuwa wa mwisho kujitokeza,kumbe mlikuwa mna ..... Longtime kitambo
 
teh teh teh, dah umenkumbusha mbaaaaaaaaaaaaali, enzi hizoo za kucheza nage na mdako, ukuti ukuti wa mnzaz unahusika pia hapa, vp kibaba na mama kwenu hamkucheza,

msosi hasa ubwabwa unawekwa kwnye sinia kubwa then mnauzunguka mduara, spidi yako ya kukata matonge ndo shibe yako, the slower you are the little you will eat! Ckilizia ubwabwa ukianza kuisha kila mtu anachota tonge lake kubwaaaaa, nlikua na binamu yangu huyo balaa tonge lake moja kwangu matatu! It was funny sana enz hizo!
 
1. Kuinda ndege makaburini. 2. Kuvua samaki mtoni. 3. Kucheza kombolela. 4. Kumtamani baba wa mwenzio awe baba yako kwa vile wana baiskeli. 5. Kudandia magari. 6. Kucheza usiku wakati wa mbalamwezi...

kha, we tulicheza wote nini?? Mbona mawazo yako kopi ryt kama yangu? Dah, am touched! Mk1
 
Enzi hizo kuangali video kwa jirani MPAKA MUOGE kwanza ndo mruhusiwe.
Na huko ndani mnaenda kukaa chini.
 
gombania goli
kukamata balale (panzi)
kulamba sukari
kucheza mpira wa makombe kama la Mchele, kombe la kuku
yanga yanga nipe kucha nyeupe (mnaikumbuka hiyo??)
 
1 kuoga na nguo kwenye mvua 2 kucheza kidali po 3 kula ni mbakishie baba yaani we acha tu 4 kupiga deo kwa kutumia spoku 5 kindumbwendumbwe daaah 6 kutembea na kipande cha kioo mpaka clas 7 kuokota nywele nakufika sehemu nyeti nakuonesha wenzio 8 kunyonya kidole 9 kujipitisha mtumzima alipo kaa vibaya dah kwa leo inatosha jf team

Kumaliza viberiti home ukitengezea baruti; kuua kuku au bata wa jirani katika harakati za kuitesti manati yako mpya..
 
gombania goli
kukamata balale (panzi)
kulamba sukari
kucheza mpira wa makombe kama la Mchele, kombe la kuku
yanga yanga nipe kucha nyeupe (mnaikumbuka hiyo??)

hiyo nyimbo imenikumbusha mbali sana. Dah! Kweli utoto una raha sana kuliko ujana.
 
Kuna mchezo mmja tulikua tunakusanya mchanga halafu pale katikati tunaweka kijiti.tuna kusanyika na kuanza kufukua pembeni huku tunaimba"tule tule tumbakizie baba"*kadhaa.atakaye angusha kijiti.tuna mpiga ila akituzidi mbio ndio salama yake.ilikuwa katiya 1985-1989.dah kitambo sana.

huu tulikua tunaita harusi.
alaf kuna ule wakufunga vidole (kama kiapo)
ukimkuta mwenzio ameinama ruhusa kumkata bonge la teke makalioni.
ulikua unaitwa tembo.
 
kutembea tumbo wazi muda wote huku suruali au kaputula ikikuvuka
 
1. kutembea peku
2. kula mchanga/udongo
3. Kucheza mpira wa makaratasi, peku...Ukivaa viatu unaambiwa uvue
4. Kuzamia sherehe zisizokuhusu ili uukamue ubweche yaani wali
5. Kula pipi gololi
6, Kuimba kinyulii nyulika..............
7. Kudhani kua yeyote aliyevaa miwani ni msomi
8. Kudandia magari.......
 
da hiyo ya kusingizia kuumwa nimefanya sana nilivyoshtukiwa mbinu hyo nikaanza kuficha nguo unachukua shati la shule unalitupa uvunguni asubuh mama analitafuta mpaka anakwambia utaenda kesho unarudi kulala,kuna cku akanipatia shati halionekani akanipa bonge la shati la bro ananiambia leo utaenda shule mbona nililitoa shati mwenyewe mama hili nimeliona mama analiweka mezani analivuta vuta anapunguza mikunjo unaenda shule.
 
kama hujafanya mambo haya hujakaa uswazi
1. Kulilia soda ya mgeni
2. Kukataa kuoga
3. Kukataa kwenda shule kwa kusingizia unaumwa
4. Kutochez mbali na nyumbani siku ya sikukuu ili ufaidi pilau
5. Kulamba kamasi
6. Kucheza kombolela/kidali au kibaba na mama
7. Kwenda kuangalia muvi kwenye mabanda ya video.
Haya wadau tuendelee na mengine ambayo nimeyasahau.

hiyo namba 1 me nilikua noma ilikuaakija mgeni lazima nifungiwe chumbani hili nisitie aibu halafu wageni nilikua lazima niwaombe hela.
 
........mji mpya moro full kumfatilia joyce wowowo,ukirud nyumbani ugali umeisha!!!!!!!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom