Kwa hay a wanaoshangilia serikali iliyo madarakani wanamatatizo.haya ndo maisha bora tuliyoahidiwa
Ni kweli Mkuu nilishaiweka article hii miaka ya nyuma hapa jamvini. Kinachofanyoka kuhusu rasilimali za Tanzania kinasikitisha sana na kutisha pia. Hakuna ncho yoyote duniani ambayo inaweza kuwaruhusu "wawekezaji" kuchukua almost $12 billion ya mapato yatokanayo na dhahabu ya Tanzania na kuiachia nchi $497 million tu. Huu ni wizi mkubwa sana lakini ndiyo hivyo mafisadi wameshafungua bank accounts nchi za nje na huwekewa mabilioni ya pesa na makampuni hayo hivyo mafisadi huangalia pembeni huku wizi mkubwa dhidi ya rasilimali za Tanzania ukiendelea.
DHAIFU katika kampeni zake za 2005 za Urais alidai kwamba Watanzania tunalalamikia sana mikataba ya uchimbaji wa madini kwamba haina maslahi kwa Watanzania hivyo akiwa rais angeiangalia upya ili kuhakikisha inabadilishwa ili kuinufaisha Tanzania, tangu alipoingia hakuna jipya alilolifanya zaidi ya kuongeza royalties toka 3% to 4%!!! Walitaka kuongeza hadi 5% "wawekezaji" wakagoma.
Muhongo alipoingia Nishati alitoa kauli kwamba "wawekezaji" wote katika sekta ya madini ambao wapo nchini kwa miaka mitano au zaidi watatozwa 30% ya mapato yao kama kodi asiyetaka afunge virago. Hili nalo limekufa kimya kimya baada ya "wawekezaji" kuligomea.
BAK wakulaumiwa ni watanzania wenyewe sababu ikifika 2015 wakipewa kanga na kofia basi kura zao watawapa magamba. Tunajiroga wenyewe na hakuna sababu ya kulalama
Aliyeilaani tz wala hajafa,yu hai milele yote,ni ujinga wetu tu na kufuata maamuzi ya pamoja ya kijinga.wacha nikurudishe nyuma kosa lilikotokea ingawa nina hakika sio wote walipo janvini watakubaliana na mimi,miaka hiyo tz ilikuwa na uhusiano na Israel wakahusika kutuanzishia hata jeshi la kujenga taifa,mtafaruku na vita vilipotokea mashariki ya kati kati ya israel na waparestina wakuu wa wa nchi za kiafrika wakati huo OAU wakakutana wakawa na maamuzi ya pamoja ya kuilaani israel Nyerere akiwepo kwenye huo mkutano,akaenda mbali zaidi akavunja uhusiano wa kibalozi, aaah!!kosa kubwa rudi kwenye Biblia soma vizuri usiingie kanisani na kutoka tu Ailaanie israel na Mungu atamlaani kwishaa,haijalishi utayakubali au la ni muislam au mkristo dawa ni kutubu tena kwa machozi kujutia kosa tulilofanya kisha turejeshe uhusiano na israel,maana hata leo hii ukiulizwa kwa nini hatuna ubalozi na israel kuna mtu mwenye sababu zenye mashiko au ni bla-bla tu.kama yuko member hapa janvini na anafanyia wizara ya mambo ya nje atwambie.
Duh! Ama kweli kwa hakika hii ni laana.
Lakini hata hivyo wazungu wanathubutu je kuvuna rasilimali za masikini namna hii. Wanaweza kuufurahia utajiri wao katikati ya jirani zao wanaokufa njaa? Wakifanya hivyo tatizo lao ni kubwa kuliko letu.
mi nadhani kuwa mtanzania unaetetea chama tawala kwa sasa ndo ajabu namba 1 duniani.Kuwa mtanzania ni moja ya maajabu ya dunia
Mkowapi Lumumba members kama kina ritz,ifweelo,simiyu yetu nk mje muone udhalimu wenu. Shet.a.ni wakubwa nyie