Kama hii ni Tanzania; Basi tumelaaniwa, na aliyetulaani kafa

Jamani wale mnaofanya maanadamano huko Washington hiyo ni nondo nyingine ya kummalizia Vasco Da Gama atakapofika huko
 
Nmefarijika sana baada ya kuona hii post imefika hapa!nlijtahd sana kutafuta njia ya kupost hii k2 especially to the geita side ila nikafell simply bcz natumia simu,nmefurahi kwa sababu dunia sasa inaelewa nn kinachoendelea maeneo ya migodi,wakazi wanaonekana hapo wa geita,nmeanza kuwaona tangu nikiwa form one 2005 had leo bado wapo pale,napta mara nyng pale coz ni njia tunayotumia kwenda kanisani kusali,kiukweli ni watu wanaotia huruma sana tofaut na mtu anavyodhani,tena ukizingatia now n kpnd cha mvua ndio usiseme,mahema yamebomoka wanajisitiri kwenye jumba la katibu tarafa kaya zaidi ya 20,just imagine,pembeni tu ya hapo kuna ofisi ya ardhi mita kama kumi tu,wanawapta palepale,viongozi waliopo wakiwilaya wanadai watu hao walishalipwa kama walidhulumika aliewadhulum kahamisha.ni hayo tu wakubwa.
 
Hali hii inasikitisha sana maana hawajamaa wameamua kutuibia bila huruma kwa kushirikiana na viongozi wetu "tuliowachagua" wenyewe na wasio na huruma hata chembe
 
Hili linasikitisha mno. Tatizo kubwa linalotusumbua ni ubinafsi, viongozi wenye thamana wanafanya hili rasilimali kama vile tanzania inaisha leo na hamna next generation. wanaingia mikata mibovu kwa ajili ya manufaa ya wachache huku wengi wakitaabika, Bei ya dhahabu haitofautiana sana kwenye soko la dunia ila kinachotokea tanzania watu wetu wanafanyishwa kazi ngumu za shurba kwa malipo kidogo mno(cheap labor) angali nchi nyingine hata serikali wamedhibiti uingizaji wa machine kubwa za uchimbaji ili kupunguza kasi ya uchimbaji ili waweze kunufaika kwa muda mrefu kwa kodi na kupanda pia kwa bei ya madini. Laana ipo kama unaweza kutoa tax relief kwa mwekezaji anayechukua rasilimali zako anakuachia mashimo du hii ni hatari. Tax relief kwa viwanda ni acceptable kwa sababu mwekezaji atakapoondoka tutabaki na viwanda
 
I stil believe brotherz kwamba hakuna kisicho na mwisho.mana kila nikifikiria nafikir kama ntachanganyikiwa.IN GOD I TRUST THAT ALL THIS WIL COME TO END
 
Back
Top Bottom